MoseKing
JF-Expert Member
- Jul 5, 2017
- 4,928
- 8,976
Kivevele mpigwa mitiHuna akili
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kivevele mpigwa mitiHuna akili
Milion 5 ndio nyumba iuzwe jaman? Ina maana ameshindwa hata kuongea Na huyo mwajuri wake amkopeshe.View attachment 2436797
Nyumba hii ambayo ni mali ya Mary Victor Mahundi, mwandishi wa habari wa Gazeti la Raia Mwema la Dar es Salaam imepigwa mnada kwa Tsh. Milioni 30 ili kufidia deni la benki la Tsh. Milioni 5.2 ambalo alikuwa akidaiwa mume wa mwanahabari huyo.
Inaelezwa kuwa nyumba hiyo iliyopo Tabata, Kata ya Kinyerezi, Mtaa wa Kichangani ilipigwa mnada siku chache zilizopita na tayari mwandishi huyo na familia yake wametakiwa kutoka ndani ya nyumba ndani ya siku 14, leo Desemba 5, 2022 ikiwa ni siku ya 9 kati ya siku alizopewa kuhama.
Mary amesema taarifa hiyo ni ya ukweli na kudai kuwa alikuwa akifahamu juu ya deni hilo la mumewe lakini hakuwa anajua kilichokuwa kikiendelea hadi kufikia hatua ya nyumba hiyo kupigwa mnada.
“Nilikuwa Dodoma katika shughuli zangu za uandishi wa habari, nikapokea simu kutoka Serikali ya Mtaa kunijulisha kuwa nyumba yangu inapigwa mnada.
“Niliporejea nikapata nakala ya barua ya taratibu za nyumba kupigwa mnada moja ikiwa imetumwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya na benki wamefuata taratibu nyingine zote inavyotakiwa, lakini hilo deni ni la mume wangu ambaye kwa sasa hatupo naye pamoja.
View attachment 2436799
“Nimewasiliana na Mkuu wa Wilaya kumueleza hali ninayopitia kwa kuwa hii nyumba si ya mume wangu peke yake ni mali ya familia, yeye (mume) kwa sasa hayupo nasi anaishi sehemu nyingine, inamaanisha kuwa tutatakiwa kuondoka ndani ya siku hizo 14, na kuwa watatuletea mabaunsa na kututoa kwa nguvu. Mkuu wa Wilaya ameniambia anashughulikia suala langu.
“Wakati huohuo, napambana kutafuta msaada wa kisheria ili kuweka zuio kabla ya hakimu na Majaji kwenda likizo ya kufunga mwaka, kwa kuwa sikushirikishwa katika huo mchakato wao wa mnada,” anasema Mary.
Nyaraka za benki zinaonesha kuwa deni lililosalia ni Tsh. 4,759,368 (Milioni 4.7), asilimia 10 ya deni ni Tsh. 475,936, hivyo jumla deni ni Tsh. 5,235,304.
Mary ameongeza kuwa: "Naomba kama kuna yeyote ambaye anaweza kunipa msaada wa kisheria anisaidie katika hilo kwa kuwa hapa nawazi nitaishi vipi na wanangu, kwanu hata huyo mume bado nina kesi naye kwa kuwa alibadili nyaraka na kuofanya nyumba ionekane ya kwake peke yake wakati hii nyumba ni ya familia, nina watoto, nitaenda wapi mimi na watoto wangu!
View attachment 2436800
View attachment 2436801
Mwandishi wa habari wa Raia Mwema wamemkalia kooni kisa hapendi vitisho.
Yeye anafanya kazi zake kwa weledi bila woga. Mfumo unataka kumtoa roho. Wakati ana kesi ya mahakamani ya 2020 aloandika kuhusu Tanzania kuwa na wagonjwa wa Corona, leo nyumba yake inataka kuuzwa na mahakama kufidia deni la mumewe aliyefariki.
Uhuru wa vyombo vya habari upo wapi?
Awali alikamatwa Mei 2020 na kukaa mahabusu ya Polisi Central kwa siku 14 kwa amri ya utawala wa awamu ya tano kwa tuhuma za kuposti taarifa za wagonjwa wa Covid19 kukimbia Amana Hospital. Akapekuliwa nyumbani kwake kana kwamba ndio mwenye kutunza corona.
Hadi sasa simu za Maria Victor, bado ipo polisi kwa miaka miwili sasa.
Pia soma;
Dar: Kundi la WhatsAppp lamfikisha Mwanahabari Maria Victor Mahundi mahakamani
Alikamatwa Mei 2020 na kukaa mahabusu ya polisi Central kwa siku 14 kwa amri ya utawala wa awamu ya tano kwa tuhuma za kuposti taarifa za wagonjwa wa Covid19 kukimbia Amana Hospital. Pamoja naye Mhariri na Mkurugenzi wa Raia Mwema Mbaraka Islam naye alikamatwa na wote walipekuliwa nyumbani...www.jamiiforums.com
Benki yapiga mnada nyumba ya mwandishi wa habari wa Gazeti la RAIA MWEMA kisa deni la Tsh. Milioni 5.2
Nyumba hii ambayo ni mali ya Mary Victor Mahundi, mwandishi wa habari wa Gazeti la Raia Mwema la Dar es Salaam imepigwa mnada kwa Tsh. Milioni 30 ili kufidia deni la benki la Tsh. Milioni 5.2 ambalo alikuwa akidaiwa mume wa mwanahabari huyo. Inaelezwa kuwa nyumba hiyo iliyopo Tabata, Kata ya...www.jamiiforums.com
Mwajiri ni Gazeti la RAIA MWEMA anaishi NHC.Milion 5 ndio nyumba iuzwe jaman? Ina maana ameshindwa hata kuongea Na huyo mwajuri wake amkopeshe.
Asipokimbilia mahakamani kuweka CAVET atakuta mnunuzi alisha maliza kufanya transfer kama ina hati, mwisho wa siku atafanya kesi na wanunuzi hata sita au atakuta mnunuzi alishaibomoa na kujenga nyingine.Nyumba ya family hapo nadhan ndo anatakiwa kuanza napo
Ndugu shukuru sana wewe ni mtoto wa hao walio kuzaa na pia unaishi hayo maisha unayo yaishi.Kwani watu wanapitia maisha gani mpka wanakopa mbona mpka leo sijawahi kopa ili nifanye jambo bora nijichange na kubana matumizi nikiwekeza kwa jambo langu lijalo.
Sasa hapo watakaoteseka ni watoto mke anaweza akapata jibwana likamtuliza
Ndiyo mwanamke unasmaje?Wanaume wanaume
Ndiyo mwanamke unasmaje?
Ndio, wenyewe wanachukua chao ilobak wanakupatiaHivi hyo hela inayozidi wakipiga mnada wanakurudishia au... Assume deni ni 5.2m nyumba imeuzwa 30m hyo 24+m wanarudisha au?
Watu wabaya sana nyieNdiyo mwanamke unasmaje?
Una umri gani kijana!?Kwani watu wanapitia maisha gani mpka wanakopa mbona mpka leo sijawahi kopa ili nifanye jambo bora nijichange na kubana matumizi nikiwekeza kwa jambo langu lijalo.
Sasa hapo watakaoteseka ni watoto mke anaweza akapata jibwana likamtuliza
Kwa taratibu za kifedha, inabidi arudishiwe baada ya kukata gharama zote na sehem zingine anazodaiwa ambako nyumba ilikuwa attachedHivi hyo hela inayozidi wakipiga mnada wanakurudishia au... Assume deni ni 5.2m nyumba imeuzwa 30m hyo 24+m wanarudisha au?
Wanawake wanamatatizo. Na huenda mwanamke kasababisha yote hayo.Wanaume wanaume
Kisheria bank haiwezi kuuza collateral ya marehemu kuna insurance ambayo huwa inafanya kazi pale mkopaji anapofariki au kupata ulemavu au magonjwa ya kudumu labda km alikopa kwenye micro credit