Waafrica na hasa Watanzania tunashida na tuahitaji msaada
Tunahitaji ukombozi na ukombozi tunaouhitaji sio wa kubadirisha Chama, hiyo haitatusaidia, ukombozi wetu ni akiri ya kuona mbali na kukingojea hicho cha mbali licha ya kwamba kabla ya kukifikia kile cha mbali hapa katikati tunaweza kupitia mateso makali, lakini tu tukipate kile cha thamani kiletacho ukombozi wetu kamili
Mkuu, inaonyesha umesahau tena, 2015 tuliimba nyimbo hizihizi, kwamba hata kule CCM watakuwa wamekichoka Chama Chao, tutamweka Lowasa ilimradi Tu, tunawatoa CCM
Tukaingia ulingoni tukiwa na turufu hiyo ya watu lundo kutoka CCM, lakini kilichotokea kila mtu ni shahidi
Leo tena unakuja na ngonjera ileile? Hivi mmelogwa? Unamsema Membe, ambaye hata ule umarufu wake haufikii hata robo ya Lowasa?
Membe, hafikii hata umarufu wa Lisu?
Tukijua kwamba kuchukua Dola ni mipango na shabaha mathubuti?
Yesu, Baada ya kufanya huduma yake Kwa muda, aliwauliza wanafunzi wake kuwa, hivi! Watu wananisemaje huko mitaani? Aliuliza hivyo ili kutathimini namna gani jamii inamchukulia,
Inawezekana hata hiyo tathimini nyie hamfanyii kazi mnajiendea Tu kama nyumbu
Membe ni Nani?? Membe mbele ya upepo mkali wa JPM, Mtajiona kama mapanzi mbele ya jabali JPM