Bernard Membe usibishane na Maaskofu, samehe tu. Yule ni kichaa anastahili msamaha, hakujua atendalo

Sio kichaa sema vimeumana.
 
Hapana!, Membe kaza kamba uko sahihi , wakati unafedheheshwa hakuna Askofu Wala Mchungaji aliyemsihi Msiba aache usheitwani wake kutaka kuwaangamiza wenziwe bila huruma huyo hastahili hata kuishi na Bin Adam, alivimba kichwa sana akitoa shutuma kwa aliodhani tu hawa hawastahili kuishi , alivimbishwa bichwa na utawala dhalim uliofutwa na Muumba, anatakaje huruma wakati yeye huruma hajawahi kuisikia ?!, Msimtafutie lawama Membe Yuko sahihi , ilikuwa busara akiri na atoke hadharani kujutia uzushi na unafiqi aliokuwa akiuzusha Kila kukicha kabla ya kwenda mahakamani ambako alijua atashinda kwa sababu aliyekuwa akimtuma hakutarajia ataondoka na atabaki mwenyewe , Sasa madhal hukumu imeshaelekeza basi HAKI itekelezwe
 
Dawa ya moto ni moto, Membe shikilia uzi huo huo mpaka akome ndio itakua funzo na kwa wengine, kutukana na kudhalilisha watu hiyo sio demokrasia
 
Pascal,ndo umeandika kitu Gani asibishane na maaskofu? Nilitegemea ungeandika samehe tu kama MUNGU anavyotusamehe SIsi wanadamu ningekuelewa,sio usibishane na maaskofu.
 
Kwa wamuaminio bwana "mateso humpunguzia mtu dhambi"
"Dhahabu hupitishwa kwenye moto mkali kabisa ili iwe na thamani"
"Mgonjwa anapochomwa Sindano si adhabu bali ndio njia yakuondosha maradhi aliyonayo",
Anachopitia Musiba hivi sasa si Uonevu bali ni haki yake na ndio njia sahihi yakumrejesha kwenye UTIMAMU wake wa afya ya akili na mwili pia.
"KARMA" akitoroka kwa Membe atakamatwa kwa Karume na aliowaumiza ni wengi, wengi sana hawatakuwa tayari kumuona akiwa huru,kurukaruka kutampelekea afe taratiiibu maumivu yatakuwa makali nayamuda mrefu.
 
haya maisha Yana Siri kubwa sana pale unapo PATA nafasi ya kuishi tenda Yale yanayofaa mbele za mwenyezi Mungu ikiwa ni pamoja kusamehe kutubu nk
Maisha ya mwanadamu ni mafupi sanaa na hayana Thamani kabisa hapa Duniani yanini kiburi, dharau kutoheshim watu.

RIP Membe mchango ulotoa kwenye Taifa utakumbuka vizazi na vizazi
 
Amekaidi maaskofu... kwakweli Kul nafsi zaikatul maut
 
Maaskofu wasio na sifa kwa mujibu wa 1tim 3:1-7 kwa hili watajizolea sifa kedekede. Wataogopwa, watajitamgazia utukufu.

Mimi nitabaki kuamini Mh Membe amekufa kifo kilicho halali kwake, yaani Mungu amehitimisha maisha yake.

Si kwa sababu amewagomea maaskofu hao matapeli matapeli(hakuna aliyeomba Membe aadhibiwe pamoja na mapungufu yao) wala si kwa sababu ya uchawi wa wajita, wakerewe na wakara kwa pamoja, bali Mungu kapendezwa maisha yake yaishe leo.
 
Humu JF kuna watu huwa tunawasoma kimzaha ila si wa kawaida!
Kifo Cha membe kinatufundisha mengi Sana

Membe hata Kama alidhalilishwa lakin na yeye alikuwa na mabaya mengi, je Ni uongo hakuwa genge Moja na kina makamba wakimtukana JPM? ,Yeye alilipishwa nin?


Kwanini hakutaka kusamehe tu na maisha yaendelee,

Kifo hakina hodi,ukifa hujasamehana na mtu ,unakuwa upande mbaya


Tuombeni mwisho mwema
 
PASCAL ULIONGEA UKWELI,AMESHAKUFA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe Pascal Mayala Pascal Mayalla sio binadamu wa kawaida. Mambo yako mengi unayayaona rohoni au pengine kwa macho ya kimwili hutimia kwa namna ya kutisha.
Au labda wewe ni msemaji ukweli na ukweli una tabia ya kujitetea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…