Biashara imenishinda, nimerudisha fremu ya watu

Biashara imenishinda, nimerudisha fremu ya watu

then, ulitakiwa kujua biashara yake kabla ya kuhitimisha kwamba mil 10 ni mtaji mdogo.,,
Sure bro!

Mwisho nimesoma post zake baada ya post yangu akisema ilikuwa biashara ya spare za magari incl tyre&batteries kwa biashara hii ukisoma post yangu #4 yenye mzizi wa mabishano haya utagundua nilichokiandika kwamba ilikuwa lazima faida ya biashara hii iendelee kuzunguka ndani ya mtaji wake.

Ukweli biashara hiyo 10mill ni ndogo,ukisema hiyo hela uigawanye uchukue tairi japo size tatu pc mbili mbili uchukue betr aina tatu N40 2 N50 mbili N70 mbili uchukue na spare hata kila item pcs mbili mbili bado huwezi kusema million kumi ni nyingi,Ila mdau anguko lake (hakujua) lipo ktk style aliyoanza nayo kwanza kuweka mtu kabla biashara haijaimarika pili kuanza ktk step kubwa kianzio kikiwa kidogo.
 
M 10 upati boda boda 5 mkuu,tvs/boxer zinakimbilia m 2.9 kwa sasa na mkataba si elfu 15 kwa siku kwa miezi,ni elfu 10 kwa siku

Ukiangalia Vzr nmegusia mda utakao enda kuchukua hyo boda ila juz kuna jamaa yang kachukua boxer bm 125 kwa 2.4m kachukua 10 at once

Mwez uliopita TVS Imechukuiwa mpya 2.5m

Ishu ya mkatab n ww mwenyewe na inatofautian maeneo na maeneo mwengne yes hyo elf 10 kwa cku either miez 12,13-14 inategemea ww utaka chombo yako ikuletee faida ya kias gan
 
Boda boda hawa hawa wa mtaani ambaye anakaa wiki tatu bila kukuletea hesabu,,,,ukiwa nayo moja utaona ni rahisi ila ongezea mbili au tatu ndipo utaona mziki vijana wengi siyo waaminifu watakutia stress utauza boda zote vijana waaminifu ni mmoja kati ya kumi

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app

Mpaka inafika wk 3 ww unakuwa wap..?
Hesabu nzur n ile ya kila cku na asikupe mkononi alete risiti ya bank ambayo tayal kalipa na wakat huo we tayal kila muamala unapo ingia unapata notification ya txt
 
Ndugu usha wahi fanya biashara yyt ile ...? Or usha fatilia bznes yyt ambayo ushawah isikia or ??

Wacha nikisaidie kitu kukufungua zaid


Bishara znazoongza dunian zenye kuleta faida

[emoji2389]biashara ya uuzaji wa silaha( usiniulze ikoje hii)
[emoji2390]biashara ya Madawa
[emoji2391]bishara ya usafr
[emoji2392]bishara ya chakula
[emoji2393]biashara ya Pesa kwa pesa

So ukichambua Vzr no2 iko poa san hapaa n dawa za hospotal na c Madawa ya kulevya nooo Nasemea Phamcy or duka la dawa muhim

No3 faida yake inahitaj mda kdg ndo utaiona Vzr
Haijalish km n boda bajaj or daladala
Haijalish spair vyovyot vile

No3 nayo haijalisha utauza chakula, au utalima, Au utanunua na kuweka stock or utafanya km vinywaj or namna yyt ile ila faida yake c kubwa sanaa inategemea na mzunguko wa eneo husika

No5 nayo hvyo hvyo ukichambua Vzr hazitofaitian

NB: mtaji mkubwa faida kubwa sas km unatak faida kubwa at once ndugu yang utaona biashra n ngum na hutoweza fanya

Be patient
 
Ukiangalia Vzr nmegusia mda utakao enda kuchukua hyo boda ila juz kuna jamaa yang kachukua boxer bm 125 kwa 2.4m kachukua 10 at once

Mwez uliopita TVS Imechukuiwa mpya 2.5m

Ishu ya mkatab n ww mwenyewe na inatofautian maeneo na maeneo mwengne yes hyo elf 10 kwa cku either miez 12,13-14 inategemea ww utaka chombo yako ikuletee faida ya kias gan
Usiseme jamaa wako ingiza mtaji wako ndio utajua bodaboda ikoje hyo biashara ni pasua kichwa wanaoiweza ni matajiri unakuta ananunua bodaboda 300 alaf anazigawa kwa vijana na hela anazo za kutosha ukileta zengwe anachukua chombo chake na wewe ukiendelea kuleta mdomo unajikuta upo polisi.
Wenzangu na sisi bora ufungue tu biashara nyingne utapata nafuu sio hyo.
 
Kuna mtu ana uzoefu mkubwa sana kwenye biashara aliwahi kutoa ushauri wa namna ya kuanzisha biashara.
Alisema hata kama una mtaji mkubwa vipi usianze nao wote anza angalau na 10% ya mtaji then utakavyozidi kuelewa mwenendo wa biashara yako utakuwa unaongeza polepole mtaji.
 
Huu ndio uanaume.. Mimi nilimuweka kijana akawa Kama anaifix pesa nimemtoa..
Hawa vijana nao ambao huwekwa madukani huwa ni sababu ya kukwambia Kwa biashara,kuna siku moja nilienda mkuranga nikawa sehemu napata msosi Kwa mama lishe,basi tukawa na kijana mmoja tunakula nae,baada ya kuondoka yeye wale wadada wakawa wanamuongelea kuwa jamaa wakija washikaji zake anawanunulia vitu ovyo ovyo na anapenda Kula ovyo ovyo kifupi anatumia hela ya Dukani vibaya,je Duka kama Hilo litapata faida saa ngapi.

Kuna mdogo wangu alikuwa na frame kariakoo anauza nguo za ndani za wanawake,naye ni ke basi akawa anamwachia binti mmoja auze,baadae anakuja kujua binti nae kafunguo Goli uswahili anauza,ina maana alikuwa anachukua ktk kila dazeni nguo kadhaa,kwahiyo usimamizi nao muhimu sana
 
Siri ya biashara yoyote kufanikiwa ni kuwa na nidhamu ya pesa. Haijalishi unaanza na mtaji gani. Weka rekodi kwa kila hela inayoingia na kuroka kwenye biashara na je hiyo inayotoka inaenda wapi? Nidhamu ya fedha ndo mchawi.
 
Siri ya biashara yoyote kufanikiwa ni kuwa na nidhamu ya pesa. Haijalishi unaanza na mtaji gani. Weka rekodi kwa kila hela inayoingia na kuroka kwenye biashara na je hiyo inayotoka inaenda wapi? Nidhamu ya fedha ndo mchawi.
Hiii kitu ndo ngumu sana kwa watanzania.
 
Pole sana mdau, biashara inataka utulivu na uvumilivu.

Inawezekana kuna mistake uliifanya bila kujua, biashara ya mtaji wa 10mill kama ulikuwa unaitegemea hiyo hiyo kuendeshea maisha ni uongo isinge-survive maana ilibidi faida inayopatikana humo ndani ya hiyo miaka mitatu izidi kuiimarisha ndo uanze kula faida.

So ni kusema faida yake ungeanza kuitegemea baada ya miaka mitano mtaji ukiwa umeshakuwa, ni changamoto sana mtaji wa biashara ukiwa mdogo.
Sio kwel hata kidogo yan asubirie 5years ndo aanze kula faida ....km mambo yangekua hv bhac biashara zingekua ngumu sana
 
Sio kwel hata kidogo yan asubirie 5years ndo aanze kula faida ....km mambo yangekua hv bhac biashara zingekua ngumu sana
Sikupingi mkuu,but sijui unaitafsiri vipi maana ya biashara ila muhimu tujue maana ya kupata faida ktk biashara ni pale unaweza kuchukua hela cash iliyotokana na biashara husika ukaenda kuiweka sehemu tofauti na bado ukawa stable sokoni,kuchukua 1,000/= ya vocha au 3,000/= ya kula kwa siku hiyo hujala faida.

Tuna mitazamo tofauti mimi sikusoma sana wala sijasomea hayo mambo ila nipo kwenye game najua nachokisema otherwise kwa upande wako uko sawa.
 
Hizi biashara za uchuuzi zisikie tu...kama sehemu ulipo mzunguko ni mdogo lazima uangukie pua hasa ikiwa kila kitu unategemea hapo hapo...

Mimi baada ya biashara yangu ya hardware kufa, nimekaa pemben kwa muda sasa hata nikirudi nitafanya biashara ya kutoa services.
 
Mpaka inafika wk 3 ww unakuwa wap..?
Hesabu nzur n ile ya kila cku na asikupe mkononi alete risiti ya bank ambayo tayal kalipa na wakat huo we tayal kila muamala unapo ingia unapata notification ya txt
Kila jioni anaenda benki kupanga foleni ku deposit 15,000/= ???
 
Mimi nilianza na laki 7 bidhaa za nyumbn na miamala 2.5...jamaa mmoja swahiba wangu akaniambia nijiunge na biashara ya forever..nikatoa laki 7...hela angu ikazama....

Mtaji wa miamala nilionao Sasa Ni m1 na kamisheni huwa napata above laki2 per month...

10m ni mtaji mkubwa Sana ...inategemea unafanyia wap na biashara gani..
Mtaji kiasi gani unafaa kuanza nao kwa duka la mahitaji ya nyumbani?
 
Mkuu, miezi mitatu ya mwanzo nilikuwa nakaa mwenyewe. Nikawa na shughuli nyingine ya kufanya, nikamleta mdogo wangu wa damu kutoka mkoani, ndio kuja kushtuka duka limebaki 3.2m
Duh mlikua mnakopesha na mmeshindwa kulipwa? Mlikua mnatunza hesabu vizuri? Je matumizi binafsi pia yalikua yanatumia pesa ya dukani pia? Gharama za uendeshaji zilikuaje? Pole ila jichunguze ulipokosea unaweza kufanya biz nyingine(lesson learned)
 
Back
Top Bottom