Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Biashara inataka watu wenye roho ngumu, fikiria nimewekeza 300M+ napata 5M kama faida Kwa mwezi

Kuna mda unaweza kuwa kichaa kwenye haya mambo ya biashara.

Nimewekeza Tsh million mia tatu ( 300m+) nimeanza biashara faida ndio napata 5m yaani million tano Kwa mwezi.

Hapo sijatoa mishahara ya wafanyakazi na gharama za kuendeshea ofisi.

Wafanyabiashara mna roho ngumu sana, presha nje nje
Mwenye milioni 300 anakuwaga hivi?
 
Walengaji tuko nao kitaa huku na kila siku tunawanunulia k-vant Sasa sjui hesabu hizo hawazionagi au la?😄😄

Kulenga gari uwe na bahati sana.. kulenga labda ulenge kiwanja ama nyumba kabisa. Na viwanja vya kulenga ukauza haraka ni vile vya prime area vya milioni 50 ama milioni 100. Sehemu zimeshaendelea tayari.. sio ulenge viwanja vya milioni 3 ama 5 mbali na mji. Uuziii haraka.. hadi usubiri mji ukue miaka mbele
 
Pole sana mkuu!!!Nadhani choice ya aina ya biashara, Mimi ninewekeza sh M7 kwenye kisteshenari changu napata faida ya laki 900,000 kwa mwezi,nawaza kununua mashine kubwa ya kuchapa mabango Mungu akinijaria uzima ndani ya miaka mitano ijayo, ambapo nimeulizia nikaambiwa mashine hiyo Ni zaidi ya 10M.

Hakika mtu akiniuliza biashara ipi inalipa Mimi nitamwambia steshenanari, hasara Ni ndogo Sana, na tena naweza sema Ni zero
 
Duh brother, sikubaliani na wewe:
300m x 12% = 36m
36m/12 = 3m paid annually.
Scenario ya pili
300m x 15 = 45m
45m/12 = 3.75m paid after 6 months 22.5m
Hizi zote ni risk free investment.

Yeye amesema anapata 5m/m lakini bado ana obligation ya kulipa wafanyakazi na hela yake anaipata kila mwezi.
Miezi 6 unasubiri hela ya BOT utajikuta umeishakopa kwingine au umekula mtaji kwingine.
Kwa mtu wa mahesabu kupata 5m/m from 300m investment inaoonyesha hakuwa makini kuchagua wapi awekeze hela yake.
There are better investment opportunities with higher ROI than the one he went for.
Idea ya bond ni kumuondoa kwenye risk anayocheza nayo saa hii ,
 
Biashara ni ngumu sana nikiwaza nasema tu wacha wafanyabiashara tuitwe risk takers

Nina biashara 3
Moja mtaji laki 3 ila kila siku napokea feturn ya avarage ya 9000
Nyingine ina mtaji 2,000,000 return yake monthly hata laki na nusu haifikishi (though ni eneo la kimkakati huko mbele italeta return nzuri tu I hope)
Biashara ya 3 Mtaji milion 2 , daily return wastan ni sh 10,000

Cha kushangaza eti naogopa kupoteza ile location ya biashara ya pili nikiamini nikiiacha nitakuja kuililia huko mbele maana ni potential area sana huko mbele miaka mitano baadae

Na zote tatu ni biashara zisizo na mwingiliano yaani ni biashara tofauti kabisa.

Biashara ni ngumu sana for sure
Una mtazamo chanya sana, moja ya kanuni kuu ni kuwa usitage mayai yote kwenye kiota kimoja.
Kama una biashara tatu na haziingiliani ni, mfumo mzuri sana umejiwekea .
 
Challenge kwa kutupia uzoefu mkuu faida kwa wote..me mwenyewe najichanga nianze na scania 113 ya kuvua mtu [emoji16] niko kwenye hiyo circle naona tender zinavolipa..tupe uzoefu wako Boss [emoji120]!
Usiguse mkuu, utakufa na presha ndugu yangu
 
Anaepata 5m per month kwa mtaji wa 300m, anapata faida nzuri.
Hasa kama anatoa ajira kwa watu, hiyo pia ni faida.
Nope, kwa maelezo aliyoyatoa ni vigumu kumpa ushauri. Hajaeleza anafanya biashara gani, ana muda gani katika hiyo biashara, yupo eneo gani na stock anapata wapi. Wateja wake ni akina nani. Issue za kodi yupo vizuri?
Ndio maana sijamshauri. Ni biashara inayotegemea misimu(seasonal).
Simshagai, watanzania bado tuna changamoto nyingi mojawapo ikiwa kama hii. How could you put such a huge amount of money in a business that is New to you?
 
Back
Top Bottom