Biashara ipi rahisi kuiendesha hata ukiwa mbali?

Mkuu jitahidi sana kupunguza mawazo HASI mtu anapo omba ushauri

Biashara yoyote ile ni risk taking.... hata ukiwa na passion na ukasimama mwenyewe bado sio guarantee kwamba utafanikiwa

Kila nikikumbuka jinsi watu kama wewe walivyonikatisha tamaa nilipotaka kuanzisha biashara yangu nikiwa kibaruani huwa nabaki nacheka tu........ leo hii nina vibiashara vyangu zaidi ya 5 napiga simu tu na maisha ya songa kiroho safi
 
Kama una kiwanja maeneo fikika..
Jenga vikota vyako viwili, weka wapangaji, nenda kashinde huko unakoshindaga. Au ujenge nyumba moja yenye unit tatu za wapangaji.

Hakikisha unaujua ujenzi. Hiyo hela inatosha, ila kama huujui, utagalagazwa uache mapagale.
 
Mkuu hili swali huwa ni gumu sana kwasababu linategemea mambo mengi sana

Kama ndio unaanza jaribu kufanya utafiti eneo unalotaka kuanzisha hiyo biashara kwa sababu ukikosea tu itakula kwako

Biashara zote zinalipa ni juhudi zako za kutanbua fursa ipo eneo gani na kupata mtu sahihi wa kusimamia

Mimi biashara yangu ya kwanza Ilikua hardware kwasababu eneo nililojenga wakati huo ujenzi ndio ulikua umepamba moto na cement tulikua tunafuata mbali sana
Nilianza na mifuko 70 tu..... the rest is history
 
Bora uchukue ela yako uweke utt maana bila uwepo wako utakuja kulia kilio cha mbwa aliyepigwa jiwe. Watu si waaminifu haijalishi ni ndugu wala marafiki.
 
Acha vitisho na kutisha watu mnakuwa na mentality za kuwaaminisha watu kuwa Biashara ni za watu fulani .
Sio za watu fulani zina principa zake, sio ukiwa na pesa tu unawaza Biashara, Ndio maana kuna wengine wanaamua tu kuwekeza kwenye kununua hisa za makampuni au Bond za Serikali na wanakula mdogomdogo.
 
πŸ™πŸ™πŸ™
 
Sasa tufanyaje na hii mitaji yetu?
 
Nashukuruni kwa mawazo na michango yenu! Lakini bado najiuliza, kama ni lazima niisimamie kwa karibu sana, inawezekanaje watu wengine wakawa na biashara karibia kila mkoa? Inawezekanaje watu wengine wanamiliki biashara hata chi za nje na bado zikafanya vizuri bila uwepo wao mahali pa biashara? Au kwa vile biashara zao ni biashara kubwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…