Biashara Tanzania ni pasua kichwa. Ukiondolewa kwenye reli, kurudi na kukaa sawa si rahisi

Umeelezea kitaalamu sana. Kuna mama mmoja wa Arusha alikuwa na vibanda kibao vya simu mwanzoni mwa miaka ya 2000 na pia alikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kuuza simu za kutoka Dubai ila baada tu ya watu kuwa wengi akahamia kwenye mambo mengine na kuachana kabisa na ishu za kuuza simu. Watu walidhani maza kalost mara kaibukia kwenye malori ya mchanga na kuanza kuwa muuza matofali (blocks) maarufu. Kuna watu wana vipaji hadi wanatisha..
 
Watu wanasema mohamed trans kafirisika!! Hivi mtu akifa anafirisika?

Mfano leo mzee tashrifu kafariki kaacha Bus zinapiga kazi mwakani kampuni ife utasema tashrifu kafirisika?

Ukweli ni kwamba waarabu au watu wenye asili ya Asia wanajua sana biashara kwa hapa bongo.

Mfano yule mwarabu wa shinyanga alivuma sana na kampuni ya allys sport bus miaka ya 2009 baadae akawa kimya amekuja kurudi upya na kampuni ya mpya ally star bus na ndo kaishikilia njia ya dar mwanza anatoa gari nyingi kwenda na kurudi kila siku kwenye njia hiyo.

Mtu anachukua nauli 120k dar to mwanza na gari inajaa kila siku hata ukienda kukata tickets unaambiwa kesho VVIP Bus imejaa!! Gari yenyewe sasa hata sio VVIP
 
huyu Allys alifariki hizo basi pia zikagawanwya mke mkubwa na watoto wake na mke mdogo na watoto wake, ila wengine wamashafilisika yule allys star ndo kabaki peke yaje, na watoto wa Muhammad transi wengi wamefilisika mpaka kuuza migodi ya halmasi. Kwa ufupi na waarabu wengi wanafilisika ila wanafichiana siri hawasemane kama sisi wa makonde, wengi walisha filisika kokoo ni omba omba ila huwezi kugundua jinsi wanavo fichana siri.
 
tatizo la wengi tukishafanikiwa kwa aina fulani ya biashara tunaona kama hiyo biashara tutadumu nayo milele.
hatuwazi kabisa kutengeneza binary za kibiashara, kwamba biashara moja ni mtaji wa biashara nyingine.

na tunajisahau sana kwenye starehe sera za TRA ni kwa uchache sana zitakuathiri ila tatizo kubwa lipo kwetu.

kwa mfano unamiliki bus dar moro then unaona kabisa SGR inapita route yako, si upeleke gari mbeya. Mchawi wa biashara ni wewe mwenyewe.
 
Zamani nilikua najiuuliza kwanini wafanya biashara wengi wana punguza mitaji yao na kujenga majumba, kumbe ni security yao biashara hapa kwetu ni unpredictable, kwa sera moja ya TRA mtaji unakatika kwa siku moja
Ni kweli biashara Ina badilika lazima uwe na assets za kutosha.
Sor nje ya mada hivi mkiwa mnastorisha mkafikia kwenye gari hiyo harrier na upo na mtu unamuheshimu utamwambia " harrier Tako la nyani" Kwa mfano baba mkwe
 
Sijamaliza kusoma ila hapo kwenye MUNGU yaani Mungu ndo Kila kitu
 
Ni kweli biashara Ina badilika lazima uwe na assets za kutosha.
Sor nje ya mada hivi mkiwa mnastorisha mkafikia kwenye gari hiyo harrier na upo na mtu unamuheshimu utamwambia " harrier Tako la nyani" Kwa mfano baba mkwe
Neno tako kwa mswahili sio tusi hata mama mkwe hulitamia bila aibu........labda kwa watu wa bara baadhi
 

Goodwill ya Biashara ia built with time na inakuwa recovered kwa time kama nilipotea, sasa ukitoka kwenye Biashara, kurudi ni Ngumu maana mifumo, mabadiliko etc hubadilika, lazima uwe mbunifu sana, Capital can be recovered, not Goodwill au wateja, wanakuwa wamemove on!

Ukivurugikiwa na Biashara wakati umeoa, kuinuka kunaitaji roho ngumu sana na determination ya hali ya juu, sio rahisi, na ndo mda wa kutosikiliza mtu zaidi ya determination zako.

Kama unaweza, hudumia watoto na mke na kaa mbali kabisa ili iwe rahisi kuanza upya kufanya bidii, hao wanaweza wasiinuke milele, Amina, Haleluya! Wanaweza ishia kufa na sonona.
 
Muhamed trans hajafilisika.. mpaka leo bado ni tajiri..

Waarabu huwa wanabadilisha biashara. Kama sumry alivyoua ma bus na kwenda kwenye large scale agliculture.

Mohammed trans mpaka leo wana malori kibao. Na sheli wanazo za kutosha tu
Yah story ya mohamed trans niliisikia nasikia alichukua mkopo wa pesa nyingi akaweka bond baadhi ya mali kumbe ilikua ni trick yale mabasi yalipigwa mnada na pesa ya mkopo ameinvest,naskia sku iz amehamia mwanza ?
 
Mkuu ulishawahi kupitia hiyo hali au unatoa tu ushauri kwa kutumia uzoefu wako?
Jamaa alichokiongea ni sahihi na kina uhalisia.
Unapojikuta umeanguka tumia hicho hicho kidogo ulichonacho kujikongoja hadi ufikie level unayotaka,shida iliyopo wengi huwa wanaona aibu kushuka chini kutokana na status waliyojiwekea.
Wewe huoni wale wachina wamekwea pipa kutoka kwao kuja TZ kisha wanauza viatu kwenye meza sasa wale ndio real enterpreneur wala hawana muda wa kuwaza kwamba watachekwa as long as their plan is to be a future millionaires/billionaires.
Pia usisahau ya kwamba mtaji namba moja ni ideas ulizonazo kichwani.
 
Afadhali hao Ndugu zako mitaji yao ilikuwa inapukutika kidogo kidogo, mimi rafiki yangu alienda kuchukua nguruwe 200 mbeya wenyewe thamani ya mil 50,kumbe homa ya nguruwe ilikuwa imeanza kuingia kimya kimya anafika dar anawaswaga zizini kesho yake asubuhi anakuta nguruwe zote zimekufa.
Napewa taarifa rafiki yako amepoteza fahamu yupo rabinisia baada kupata fahamu akasema mapambano yanaendelea😄
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…