Biashara Tanzania ni pasua kichwa. Ukiondolewa kwenye reli, kurudi na kukaa sawa si rahisi

Hapo angechinja tu mkuu
 
Mimi mshahara wangu unanitosha... Napata pesa najenga nyumba zangu mdogo mdogo... Nikikaribia kustafu nyumba zangu mbili tatu na fremu zitanilisha...
Biashara ni kipaji sio kila mtu anacho... Na sio kila mtu anaweza kufanya biashara... WaTz wengi mnafilisika kwasabab ya kuiga kufanya biashara kama fulani... WaTz wengi wakiona biashara fulani ina trend basi wote wanaitaka... WaTz wengi sana wanafanya biashara ili waonekana tu wakat ukweli hakuna faida wanayoingiza... WaTz wengi biashara zao ndogo wanataka ziwalipie kodi zisomeshe watoto wale bata na kuhudumia ndug, jambo ambalo haliwezekani kiuchumi ktk biashara...
 
Dah! Huu uzi kama unatutisha vile sisi wengine tuliokimbia kazi za kuajiriwa na kuingia kwenye biashara. All in all, nilichogundua, biashara inahitaji muda wote kichwa kiwe active.
Kwenye kazi za kuajiriwa Boss wako anakukumbusha na kukusukuma uwe unawahi kazini mapema lakini unapokuwa na biashara yako masaa 24 inabidi kichwa kiwe kinawaza ubunifu mpya na wakati huo unawaza ubunifu kuna wapinzani wako pia hawalali wanabadili mbinu kila siku ili kukupiga gepu.
Biashara ndio inataka hivi uipende,utafute na kubadilisha mbinu mpya kila wakati bila kusukumwa na mtu.
Ukianzisha biashara kisha ukawa umekaa unangoja wateja na pesa zije automatic hapo jua biashara imeshakushinda.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Dah! Huu uzi kama unatutisha vile sisi wengine tuliokimbia kazi za kuajiriwa na kuingia kwenye biashara. All in all, nilichogundua, biashara inahitaji muda wote kichwa kiwe active.
Kwenye kazi za kuajiriwa Boss wako anakukumbusha na kukusukuma uwe unawahi kazini mapema lakini unapokuwa na biashara yako masaa 24 inabidi kichwa kiwe kinawaza ubunifu mpya na wakati huo unawaza ubunifu kuna wapinzani wako pia hawalali wanabadili mbinu kila siku ili kukupiga gepu.
Biashara ndio inataka hivi uipende,utafute na kubadilisha mbinu mpya kila wakati bila kusukumwa na mtu.
Ukianzisha biashara kisha ukawa umekaa unangoja wateja na pesa zije automatic hapo jua biashara imeshakushinda.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Sahihi kabisa. Biashara inataka muda wote kichwa kiwe kinachaji. Ukikiacha kilale tu, basi lazima utashindwa mapema kabisa.
 
Biahsra nazo Ni Siri Sana Kuna biashara nafanya hapa ila duh Kweli najiuukiza HV nikiiuliawa nimetoa wapi mtaji nitasema nn ,mnk mtaji hauendani kbsa na duka

Anyway biashra nyingi Ni Siri na mm Nina Siri fln siwezi kuweka hadharani snaaa
Daah nakuja basi piemu kuzichukua hizo siri
 
Wote mnaongea ila hutakaa uone makanjibai na warabu humu wanalia biashara imefilisika..

Nadhani kuna sehemu tuna kosea wasfrica sie..
Wanafukiza ubani kila asubuhi. Wabongo badala ya kuombea biashara kila siku tunawekeza kwenye kula tunda kimasihala tunaondoka na mikosi.
 
Bonge la Uzi.Uzi huu ni mfupi lkn umebeba kitu Muhimu sana kwa Wafanyabiashara wetu.
 
Yaani wee acha tu.
 
Daaaah Wakuu ,sitaki kukumbuka ila haina jinsi ku share na kunikumbusha mbali japo sio mbali sana,2016 kipindi cha mwenda zake,yupo kwenye high peak ,Mshua bhana alijilupua kwa kuchukua mkopo au hela za watu Bank ,kwa ajili ya kuzungulishia kwenye biashara zake za mafuta,HFO au kwa lugha ya malkia Heavy Fuel oils, ni mafuta ambayo yanatumika viwandani kwenye ma Boiler, alinunua HFO zipato litre 150,000 kwa ajili ya masoko yake nche ya nchi ya Kenya.
Akafanya biashara na mkenya baada ya kuja yard na kuukagua mzigo na kuona mnzurii sana,akalipa advance nyingine mpka mzigo ufike ndio atalipia kwa njia ya bank,..Mshua akatafuta semi tatu za kukodi Tanker,na unzuri Mshua alikuwa na Mende mbili Scania pulling na trailer zake ,vyuma vikapakia mafuta yrd,vikatoka Dar es salaam vinzuri tu mpaka boarder ya Namanga, Changamoto ndio ikaanzia hapo bhana,tumeonyesha documents na vibali vyote vya mzigo,wale majamaa ya wanaohusika kuvusha magari upande wa Kenya ,
wakawa wanakaza ,wakawa wasema mambo ambayo sisi tulijua wanataka chochote kitu lakini wapii ,wanasema mmbo yamebadilika kutokana na mfumo wa Sera za nchi,Tukawa wapole tukaona ngoja tuvumulie pale mpakani Namanga mambo yanawenza kuubadilika lakini wapii,tulikaa kalibia miezi miwili tukaona mambo yamekuwa sio mambo,
fikilia gharama za kupark na ulinzi wa magari,plus madereva ma turn boy ,escorter wa mzigo ,mkenya naye anataka aludishiwe hela yake ,Bank nayo hawaelewi wanataka marejesho yao ilikuwa Mshua anapitia kwenye kipindi kigumu sana mpaka ikafikia sukari kupanda na presure juu, Ila tunamshukuru Mungu alirudi kukaa sawa ,japo sio kama mwanzo ku recover ni ngumu mno,Aliunza baadhi za nyumba,mzigo bei ya hasara na magari pia ili ikawe sawa,
 
Duh pole sana,vipi madeni ya benki alimaliza?na je baada ya hapo aliendelea tena na hiyo biashara au ameachana nayo kabisa

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Biashara kipindi cha mwenda zake hususani ya nje ilikua risky sana, wengi tulihamisha mitaji au kubadili biashara ambazo ni less risky kama real estate guests na parks biashara ya Tanzania ni unpredictable sana usiweke mtaji wote sehemu moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…