Biashara ya Dagaa: Mjadala wa Uendeshaji, Masoko, Faida, Hasara na Changamoto zake

Biashara ya Dagaa: Mjadala wa Uendeshaji, Masoko, Faida, Hasara na Changamoto zake

Mimi niko mwanza lakin nataka kuanza biashara ya dagaa niwe natoa mwanza napeleka dodoma wenye kujua soko la dagaa dodoma wanijuze
 
Mimi niko mwanza lakin nataka kuanza biashara ya dagaa niwe natoa mwanza napeleka dodoma wenye kujua soko la dagaa dodoma wanijuze
Subiri kwanza serikali ihamie ndio utapga hela maana dom hawana ziwa wale
 
Unakuja kupambana na warangi sio,karibu sana aisee sokoni ila tafta wasokoni kwanza wakupe muongozo kabla hujaleta huo mzigo jamaangu.
 
Wana jf nafanya biashara hii ya dagaa miaka mitatu sasa, muda wote huo nilikuwa nachukulia hapa hapa Arusha sokoni... Kwa wale wanaoleta na kuuza kwa bei ya jumla. Sasa nataka nianze kununulia visiwani harafu nawasafirisha hadi kwenye kiringe changu cha kuuzia hapa arusha...km kuna mtu aliyeko kisiwa chochote cha dagaa wakavu wazuri (grade one)tuwasiliane 0762742349.Bei ya debe moja isizidi 10,000/= maana hapa Arusha tunapima debe tisa ndo gunia la Dagaa.
 
Mkuu ningependa kuuliza , hao dagaa wa hizo sehemu tatu wana tofauti gani ? na ni wapi wanasoko zuri na pia ubora zaidi ?
ningependa kufanya hii biashara naomba ushauri .
 
Wote ni wazuri sema maandalizi ndo yanatofautiana wengine wanaanikwa kwenye michanga wengine kwenye nyasi wengine kwenye mazuria
 
Asante kwa ushauri. Bei zao sokoni zikoje Saivi!
wa bukoba wako juu kwa bei ya kuwanunua na kuwauza maana hawana mchanga,Musoma pia wanafata mwisho wa mwanza maana wana mchanga sana.Bei pia hutegemea na soko la sehemu husika...watu wa pale wanapenda dagaa wa wapi haswa...
 
Habari wanaJF.
Natamani sana kuwa huru kifedha na kufika mbali kimaisha kupitia biashara ya kujiajiri, sipendi ajira ya mtu.
Naomba kabla sijaanza rasmi nipate mwanga kidogo kutoka kwa wataalamu wa hizi kazi ila nina mtaji wa laki mbili tu.
Success people help others to reach where they are.
Karibuni sana
 
Habari ndugu zangu, natumaini mu wazima wa afya.
Mimi mdogo wenu nahitaji kujihusisha na biashara ya dagaa ila sijawa na maarifa ya kutosha hivyo naomba mwenye ujuzi wa anajihusisha na biashara hii anisaidie maarifa ili nisijekujikuta napatwa na changamoto kidogo nakimbia..
Nipo tayari hata kulala nje au ziwani mradi nifanikishe malengo japo mtaji wangu ni laki mbili nikijitahidi sana inaweza kuwa 220,000.
Naomba mchanganuo kidogo na MUNGU Awabariki wenye kunipa mwanga,,, (wale wa matusi na kejeli najua mtajitokeza ila leo kwangu kesho kwenu kila mtu anafungu la wajibu anaoutenda.)

Ahsante na karibu kwa maoni yenu wakuu.
Kwa mawasiliano ya direct/WhatsApp 0769321005
 
08aa541868404c18c32d642ec4b91197.jpg
 
Back
Top Bottom