Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake


Matengenezo ya injini ni mil.120!!!!!!! Halafu ziliharibika zote kwa pamoja?
 
Nakushauri hiyo gari bebea watoto wa shule nursery wala hutoona haya wanayokufanyia hawa madereva kwani utakuwa umeingia mkataba na wenye shule ambayo utakuwa umeingia tenda nayo

achana na kubeba abiria wa kawaida fanya hii ndo nzuiri kwako haitkupa stress za hovyo
 
Mkuu sijakuelewa kabisa labda uandike kwa ufupi kidogo nielewe
 
Mm pia nipo kwenye biashara hii ya Daladala,kwa kifupi ukiogopa changamoto biashara hii utaona ni chungu sana,Ngoja ni share nanyi changamoto nilizopitia katika biashara hii,mara ya kwanza kabisa kununua hiace nikafanya taratibu zote vya vibali kisha nikaingiza barabarani gari ikafanya kazi siku mbili ya tatu ikapata ajali mbaya sana na baada ya hapo ikakaa gereji mwezi mzima niligharimu kama 1m kunyoosha bodi na mambo mengine,baada ya hapo gari ikaingia tena barabarani ikafanya kazi miezi mitatu ikaanza kula oil nikaifanyia overhaul ikagharimu kama Laki7,baada ya hapo gari ikaingia tena mzigoni ikafanya kazi miezi miwili ikanok engine ni mengi tu nayoweza kushare na ninyi lkn kwasababu ya muda naachia hapo,lkn hadi sasa nipo kwenye hii biashara ya Daladala
 
Mkuu mimi binafsi nakushauri uchukue toyota hiace naona kama itadumu kuliko nissan
 

Una maelezo mazuri sana ila hapo kwa Nissan ungetia Rz ungekuja na maelezo tofauti mkuu. . . . Uliza madereva wako kama njia yao ina Petrol engines watakueleza
 
Natumaini ni wazima wa afya,

Naomba mwenye uzoefu wa biashara ya daladala anipe japo mawli matatu ya kuanzia na wapi ntaweza kupata Gari zuri kwa bei nzuri. Me mfukoni ninayo Milioni 6 kesho.
 
Duu Mkuu hiyo pesa ndogo sana utapata Hiace iliyochoka sana maana hata Noah huwezi pata maana ni bora ungeiongeza ukanunua Noah ukaifanya Daladala ukala 50 kwa siku sio mbaya ngoja waje wataalam
 
Dah! Mistake kubwa watu wanayofanya katika business ni kuingia kichwakichwa kwny biashara(bila experience) na kutoinvest muda wako ktk hiyo business
Kama wewe ndo utakuwa kinda/dereva wa hiyo gari na kila gereji upo am sure itakutoa
Otherwise its a waste of ur money and time, Fanya mengine sio busness
 
mkuu milion 6 biashara ya daladala!!!???? upo mkoa gan
 

Ndio mahna nimekuja huku nipate mawli matatu mkuu tuangalie tunafanyaje
 
Duu Mkuu hiyo pesa ndogo sana utapata Hiace iliyochoka sana maana hata Noah huwezi pata maana ni bora ungeiongeza ukanunua Noah ukaifanya Daladala ukala 50 kwa siku sio mbaya ngoja waje wataalam

Noah yaweza kunitoa kweli mkuu
 
Kwanza nakupongeza kwa kuweza kuzichanga pesa kufikia hadi hapo na kuwa na ndoto yako. Bei ya gari haiangalii mkoa uliopo,maana unapoongelea gari lolote lazima lihusiane na Dar es Salaam.

Sasa kwa bei hiyo huwezi kupata gari,jipange uongeze pesa kiasi. Halafu ukubali changamoto za Magari,maana ukijua kupokea pesa ujue na kuitoa pesa.
Wengi wanalaza magari kwa kuona wanapokea pesa na muda fulani ikitakiwa kutoa pesa basi mtu anaona kwamba biashara ngum na haifai.Lakini ukweli ni jinsi utakavyojipanga ndio utakavyoiweza hii biashara.

Wengi wanakatishana tamaa ya biashara za magari ni wale wenye mentality za kwamba Magari sio biashara ya kufanya,maana presha tupu,lakini mie nakumbuka hii kauli ipo tangu Baba yangu yupo kijana na mpaka uzee tumempeleka kaburini bado watu wanakauli ya kwamba sio bisahara nzuri.
Tatizo lililojitokeza enzi hizo na wale wenye mentality hizo ni kwamba,wengi wetu tunaopata gari hizi ni vijana,Sasa ukipata gari lazima watu wakukome na madem wakujue kwamba wewe ndio mwenye mali,na masifa tele na matumizi makubwa sana kuliko kipato.

Mwisho wa siku unakwama,na unaweza kukuta ghalfa siku moja gari inakuambia inahitaji milioni moja kutatua tatizo hapo ndio wengie wanaona bora waache.
Kama ni mara ya mwanzo kumiliki gari fanya hivi;

a) Kama ni mwaka wa mwanzo wa gari, Ukipata 50,000, basi weka akiba 30,000

b) Kama ni mwaka wa pili wa biashara, Ukipata 50,000 basi weka akiba 20,000

Hapo utakuwa umeweza kuvuka maana hata likitokea tatizo kubwa vipi basi uwezo wa pesa unakuwa nao.

Muhimu: Kuwa makini na ununuzi wa magari,mtafute fundi mzuri ndio umtumie akushauri,na pia ongeza pesa. Hata 10m bado huwezi kupata gari ya biashara kama ndio mara ya mwanzo.

Kwa wale wazoefu ndio wanaweza kuanza kwa pesa hiyo,maana wapo watu hata huku Zanzibar,anaweze kukuuzia gari bodi ipo safi sana kwa 10m hadi 8,ila Engine utajua pa kuipata,sasa wajanja wanaungaunga hadi gari inatoka.Ila ni wale ambao tayari wanauzoefu wa magari na pia wanayo magari kama hayo kwenye mzunguuko wao wa biashara.

Maana nikitizama wewe ni lazima uanzie na Dungu,ambapo Dungu used kibongo ni ghali pia.
 
Mm nipo kwenye hii biashara kitambo lkn sio sana kihivyo! Wengi wanadhani kununua gari bei kubwa ndio uzima wa gari wakati sio! unaweza ukanunua hiace 25ml na bado ikawa kimeo! Ngoja ni share jinsi mm navyoendesha biashara hii.

Kwa kifupi mm huwa sinunui hiace mpya ila nachofanya huwa nanunua bodi nzuri ya hiace kisha nafunga engine mpya pamoja na gear box yake kisha matairi mapya na service za bodi gari inasimamia 10-12ml, miezi sita tu kishaeleweka,kwa uzoefu wangu sitanunua Hiace mpya milele! Kama gari ni engine na engine complete ni 7.5ml, je ukinunua hiace 25ml ukitoa 7.5ml bodi utakuwa umenunua bei gani?

Japokuwa wapo wataoponda mchango huu lkn mm kila mwaka naona mambo yanajipa.....ni hayo2
 
Mtoto Tajiri,
Hii point yako ni ya msingi sana.
Maana mie mdogo wangu nae pia aliwahi kununua gari kimeo ikamtesa sana ndio watu wakampa njia.
Uimara wa gari ni engine na mfumo wake na bodi.Kuna gari bodi zake ni nzuri sana ila Engine ndio tatizo.
Na unakuta tajiri imeishamlipa na anaona kununuea Engine bora anunue jipya,hapo ndio unakuta mtu unapenyea.
Ni Idea nzuri,nakubaliana na wewe
 
Shukrani kaka kwa kunielewa!kwa kifupi biashara hii ukishapata uzoefu wa kutosha huwezi kuimba tena ule wimbo wa kuwa biashara ya magari ni pasua kichwa,wapo wanaopenda biashara lkn wanachukia changamoto!,jua ya kwamba biashara ni kama shule kuna test,mitihani na n.k,Juhudi,uvumilivu,maarifa yatakufikisha hadi kwenye ndoto yako na ndoto yako kuwa kwenye hali ya Uhasilia!
 

Asante kwa ushauri me nawaza bas ninunue maindi na maharage kwa mara y mwsho naweza pata zaidi y m 10 then ntakutafuta mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…