biashara ya daladala inalipa vizuri sana
nimepitia uzi huuu kurasa zooote na nimejifunza mengi sana, aidha mengine nimekutana nayo sana katika biashara hiii ya daladala, ambayo mpaka sasa ninaifanya.
Kwasababu nina hamu ya ku share nanyi uzoefu wangu basi nitaomba mnivumilie kidogo ili niweze kuandaaa notes kidogo, kama mnavyojua kudonyoa donyoa hizi computer sio vipaji vyetu ila ingekuwa kuongea fasta tungemaliza.
[font=&]tatizo wengi wanaoanza biashara hiii wanafanyia kazi pesa badala ya pesa kuwafanyia kazi wao "they work for money" instead of "their money work for them". [/font]
naandaa notes kidogo na nitakuja hapa na uzoefu wangu, jinsi biashara ya daladala nlivyoanza, changamoto nilizopitia mapa hapa nlipofika.
La msingi hapa ni kuwa watu wanahamu sana ya kuwa matajiri bila kupitia changamoto, wanafanya hesabu za mezani wanataka kuziweke kwenye uhalisai. Theory na practicle vina tofauti kubwa sana. Hii pia nilifanya mimi kwa miaka miwili.
Unapowaona matajiri waliofanikiwa ndani na nje ya nchi ujue wamepitia changamoto nyingi na kubwa sana.na pengine ilifika pahala wakafilisika kabisa, wakajiiinua na wakaanza tena.
Nikisikia mmmoja wetu kuwa kapata/kakusanya hela kanunua hiace/daladala then kafanya miezi 3 kakutana na changamoto, na kaamua kuuza na kuachana na biashara hiyo, napata picha iliyonikumba mimi, na namwona huyo bwana kama mimi.
Hapa kuna mambo kadhaa huwa yanasabasha;
1. Wengi tunaingia kwenye biashara kama kubahatisha kwasababu unahisi ina hela au fulani anafanya, hatui- study biashara japo kidunchuuu
2.wengi waliochangia hapa inonekana ni watumishi/waajiriwa (kama mimi) kwahiyo wanalo tawi la kushika na kumsitisri mambo yakiharibika, nayo ni kazi,
3.wengi wanaogopa changamoto au hawakuzitarajia ama hawataki kukutana nazo, na wakikutana nazo wanachanganyikiwa kabisaaa.
Kubwa kuliko yoote wengi kama nlivyokuwa mimi tunafanyia kazi pesa badala pesa zangu zinifanyie kazi
tukisikia hesabu ya hiace ni 30,000-50,000 mathalani, baaasi tunapiga hesabu haraka haraka kuwa mwezi unajiona una 900,000/-1,5000,000/, kama tumefanikiwa kupata mtaji basi huo mtaji utufanyie sisi kazi ili tupate pesa na sio tuna mtaji halafu tena tuufanyie kazi huo mtaji.
Naweza kuwa sieleweki wadau ila taratiiibu tutaelewana; hata mimi sijafanikiwa saaana lakini i see the way, na mambo yanaenda smooth na hela sasa naziona zikitengenezwa na mtaji nilioutafuta.
Nawasilisha wakuu, ngoja sasa niweze kuwaandalia ka notes kidogo, nitakuja tena hapa sooon tuendeleze huuu uzi.
Thanx