Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

Hizi hesabu za jamaa na mtizamo wake sio mbayal.
Lakini kuna watu wana gari karibia 20 njiani na huna la kuwaambia kuacha kazi hii.
Kwa ufupi inalipa.Huwezi kusema kwamba Services ya gari na kodi ndio tatizo,vyote hivyo ni wajibu.Wewe mwenyewe unahitaji ufanyie services baadhi ya siku itakuwa gari.
Tatizo ni kwamba mtu akiona 20m anona pesa nyingi sana akitaka imlipe mapema.Ndio maana watu wanakwama hapo.Na wengine mkinunua kigari basi madem wote wajue unagari.
Kwa ufupi hakuna daladala amabayo inafika mwaka haijarejesha Pesa.
Mie ninauzoefu kwenye Vi Carry na Bodaboda.
Yaani miezi 11 pesa yote imerudi,sasa jamaa sijui hesabu zako unazitoa wapi.
 
Jameni naomba kujuzwa mwenye ujuzi biashara ya daladala hapa mjini... Kabla mtu hajaingia choo cha kike
 
Kuna uzi upo humu jukwan wataalam walisha ueleza jitahdi utafute ukufunguo ubongo zaid-
 
Biashara ya Daladala inalipa vizuri sana

Nimepitia uzi huuu kurasa zooote na nimejifunza mengi sana, aidha mengine nimekutana nayo sana katika biashara hiii ya Daladala, ambayo mpaka sasa ninaifanya.

Kwasababu nina hamu ya ku share nanyi uzoefu wangu basi nitaomba mnivumilie kidogo ili niweze kuandaaa notes kidogo, kama mnavyojua kudonyoa donyoa hizi computer sio vipaji vyetu ila ingekuwa kuongea fasta tungemaliza.

Tatizo wengi wanaoanza biashara hiii wanafanyia kazi pesa badala ya pesa kuwafanyia kazi wao "they work for money" instead of "Their money work for them".

Naandaa Notes kidogo na Nitakuja Hapa na Uzoefu wangu, Jinsi Biashara ya DalaDala Nlivyoanza, Changamoto nilizopitia mapa hapa nlipofika.

La msingi hapa ni kuwa Watu wanahamu sana ya Kuwa matajiri bila kupitia changamoto, wanafanya hesabu za mezani wanataka kuziweke kwenye uhalisai. Theory na Practicle vina tofauti kubwa sana. Hii pia Nilifanya mimi kwa miaka Miwili.

Unapowaona Matajiri waliofanikiwa ndani na nje ya nchi ujue wamepitia changamoto nyingi na kubwa sana.Na pengine ilifika Pahala wakafilisika Kabisa, Wakajiiinua na wakaanza tena.

Nikisikia Mmmoja wetu kuwa kapata/kakusanya hela kanunua Hiace/Daladala then kafanya miezi 3 kakutana na changamoto, na kaamua kuuza na kuachana na biashara hiyo, napata picha iliyonikumba mimi, na namwona huyo bwana kama mimi.

Hapa kuna Mambo Kadhaa huwa yanasabasha;

1. Wengi tunaingia kwenye biashara kama kubahatisha kwasababu unahisi ina hela au fulani anafanya, Hatui- Study Biashara japo kidunchuuu

2.Wengi waliochangia hapa inonekana ni watumishi/waajiriwa (kama mimi) kwahiyo wanalo tawi la kushika na kumsitisri mambo yakiharibika, nayo ni kazi,

3.Wengi wanaogopa Changamoto au Hawakuzitarajia ama Hawataki kukutana nazo, na wakikutana nazo wanachanganyikiwa kabisaaa.

Kubwa Kuliko Yoote wengi kama nlivyokuwa mimi Tunafanyia kazi Pesa badala Pesa Zangu zinifanyie kazi

Tukisikia Hesabu ya Hiace ni 30,000-50,000 mathalani, baaasi tunapiga hesabu haraka haraka kuwa mwezi unajiona una 900,000/-1,5000,000/, Kama tumefanikiwa Kupata Mtaji basi huo mtaji Utufanyie sisi kazi ili tupate Pesa na Sio Tuna Mtaji Halafu tena Tuufanyie kazi huo Mtaji.

Naweza Kuwa Sieleweki wadau Ila Taratiiibu Tutaelewana; Hata Mimi sijafanikiwa Saaana lakini I see the way, na Mambo yanaenda Smooth na Hela sasa naziona Zikitengenezwa na Mtaji Nilioutafuta.

Nawasilisha wakuu, Ngoja sasa niweze kuwaandalia Ka notes kidogo, Nitakuja tena Hapa sooon tuendeleze huuu Uzi.

Thanx
 
Mkuu nimekubali Nondo zako za maana sana.

Kwenye hii biashara lazima ukubali yote,na ujua kwanini unaifanya.Na kwa bahari nzuri wala haina study ya muda mrefu ila wewe muhisika ndio inabidi ujitambue.Unakuta mtu anapiga hesabu ya mwenzi huku mambo kibao yanamsubiri kati,sas aikitokea hali ni tofauti anaona ngum,na wengine husema kwamba hivi pesa yangu itarudi kweli?hapo ndio safari ya kuacha inapoanza.

Mie naweza kushare na wewe kwenye Biashara ya Carry,mfano kama ukinunua Carry nzima,basi jua utaenda vizuri sana kwenye hesabu,na services zake ni za kawaida sana,na mie husimamia services mwenyewe,yaani ndugu yangu ndio anasimamia.Muhim ni kujua ile pesa yake inawekwa au inatumika kwenye njia ipi mbadala.
Wapo wanaonunua gari kwa lengo la pesa yake isomeshe watoto,na wapo kwa ajili ya ujenzi,nk.
Sasa mfano ni kwamba kama ni Carry,basi jitahid kwanza uwe na kama 1m ndani kw aajili ya dharura,na kama ni Hiace basi weka kama 3m ndani kwa ajili ya dharura,hapo utaona wepesi sana.

Mie Carry yangu ya mwanzo,iligongwa mbele na iliuwa imepaki sehem ,jamaa alikwepa mtu wa baiskeli akaenda kuifumua mbele,sasa wakati nasubiri a bima kulipa,mie nilikuwa na akiba yake ndani na kwenda kuitengeneza ili ianze kazi mapema.

Kwa ufupi inalipa,we nenda mbagal uone zile Daladala za ndani kule zilivyotaabani,yaani ukiingalia inatisha,lakini wanakula hesabu nzuri kweli.Na wapo makini sana kwenye Services,yaani amini usiamini gari ni Engine na sio bodi.
Ndio maana unaweza kuuziwa hata Prado ya 45m kwa 5m bodi tupu.
 
Hizi hesabu za jamaa na mtizamo wake sio mbayal.
Lakini kuna watu wana gari karibia 20 njiani na huna la kuwaambia kuacha kazi hii.
Kwa ufupi inalipa.Huwezi kusema kwamba Services ya gari na kodi ndio tatizo,vyote hivyo ni wajibu.Wewe mwenyewe unahitaji ufanyie services baadhi ya siku itakuwa gari.
Tatizo ni kwamba mtu akiona 20m anona pesa nyingi sana akitaka imlipe mapema.Ndio maana watu wanakwama hapo.Na wengine mkinunua kigari basi madem wote wajue unagari.
Kwa ufupi hakuna daladala amabayo inafika mwaka haijarejesha Pesa.
Mie ninauzoefu kwenye Vi Carry na Bodaboda.
Yaani miezi 11 pesa yote imerudi,sasa jamaa sijui hesabu zako unazitoa wapi.

umesahau kumsoma vizuri, tatizo lake moja tu: NI MHASIBU! Sikumbuki mara ya mwisho niliskia lini mhasibu anasema biashara yake ina faida kubwa, ni hawahawa wanaokokotolea wafanyabiashara marejesho hasi kila mwaka!
no offense op
 
na wewe hujamsoma vizuri,sio mhasibu ni mchumi,kwenye kukokota faida ni wachumi pekee wanaotoa mshahara wa mjasiriamali,huwa kuna tofauti ya faida kokotozi kati ya wachumi na wahasibu
 
na wewe hujamsoma vizuri,sio mhasibu ni mchumi,kwenye kukokota faida ni wachumi pekee wanaotoa mshahara wa mjasiriamali,huwa kuna tofauti ya faida kokotozi kati ya wachumi na wahasibu

hahahaa, ama kweli sikumsoma vizuri, lakini wote familia moja tu...wanakokotoa vitu hao hadi unaogopa, sisi wengine huwa tunaangalia tu hii kujumlisha hii kutoa hii nabaki na hii mwanaume unajitumbukiza!
 
Ni kweli ni humo humo tu.
Maana Pale IFM wote wanaingia Darasa moja wanaachiana mbele kwa mbele.
 
Na boost tena.

Wakuu hivi Route zipi Sumatra wamezuia Leseni kwa Hiace Super roof?ni kuingia mjini tu au nje ya mji zinaeendelea kutoka?
 
Mleta uzi unawazo zuri sn na Tata is the best, pia kwa ushauri wangu sioni km kwa dar zitakulipa zaid ya gari kuchoka tu, kuna njia ambzo unaweza enda fanya iyo kazi ikakulipa mpaka ukashangaa, ila inahitaji uamuzi wa kwenda kuishi nje ya dar. Njia km Mbeya-Mjombe-Songea inalipa, Njombe-Iringa mjini ni pesa tupu nk. Life si bongo tu!

Hii biashara hata mimi ninaotolea macho. Nadhani uko sahihi zaidi, mikoani inaweza kulipa zaidi kuliko hapa Dar.
 
Tata ndio mwisho wa matatizo kwa uimara wake-ila bei yake imesimama kweli kweli...70mil (uhakika miaka 7 -10)linganisha na Eiches ni 45m-50m...kazi kwako

Eicher skyline, una uhakika na hio bei mkuu???
 
Tata ndio mwisho wa matatizo kwa uimara wake-ila bei yake imesimama kweli kweli...70mil (uhakika miaka 7 -10)linganisha na Eiches ni 45m-50m...kazi kwako

Sio mtaalam wa haya mabasi, ila naongea kwa kuwa huwa nayaona na kupanda, Eicher nyingi mida ya asubuhi hapa Dar zikijaza watu, zinabonyea, yaani upande mmoja unashuka chini, ila Tata mwendo huwa ni mdundo.
 
Mleta uzi unawazo zuri sn na Tata is the best, pia kwa ushauri wangu sioni km kwa dar zitakulipa zaid ya gari kuchoka tu, kuna njia ambzo unaweza enda fanya iyo kazi ikakulipa mpaka ukashangaa, ila inahitaji uamuzi wa kwenda kuishi nje ya dar. Njia km Mbeya-Mjombe-Songea inalipa, Njombe-Iringa mjini ni pesa tupu nk. Life si bongo tu!

Kuna jamaa yangu yeye kachukua TATA Marcopolo kaipeleka mkoani kule morogoro wilayani kilombero. Anapiga route za ifakara mahenge. Ni kama km 80 hivi. Kwa @ kichwa anapiga 8000/=!
 
images

Hii biashara ni pasua kichwa sana! nilinunua coaster 2 mpya hzo hapo juu nilizifuatilia mwenyewe kutoka Japan nilichokutana nacho siyo kabisa! nilipata rout ya moro dar madereva hesabu siiyoni mara unapigiwa simu gari imedakwa hata wiki haijaisha natoa hela nyingi zaidi ya zinazoingia nakaisaliti hyo biashara! nikajaribu tena njia nyingine ya kubeba watalili bahati nzuri nikafanikiwa kupata rout ya Arusha gari kule zilitakiwa zikae huko wiki 2 sijakaa vizuri simu ikaingia ujumbe mfupi kuwa gari zimeharibika kwenye engine matengenezo ni Million 120 hapo ndipo nilipo pata hasara ya ajabu hela sikuipata ya kukodi gari maana watu niliowachukua walitakiwa warudi ndipo nichukue changu hawakurudi walikodishiwa gari nyingne! Ndiyo ikawa mwisho wa hii biashara! gari zote nimeuza! Tena niliweka hadi bandiko hapa jf gari aina ya coaster inauzwa! Biashara ya kichaa sifanyi!
 
Back
Top Bottom