Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

Mkuu kama una 40mil nipigie simu nikuunganishe upate tata abiria 45 kwa mkopo ambapo unakuwa unarejesha milioni6 kwa mwezi na kwa mwaka mmoja
 
Mkuu kama una 40mil nipigie simu nikuunganishe upate tata abiria 45 kwa mkopo ambapo unakuwa unarejesha milioni6 kwa mwezi na kwa mwaka mmoja
Shukrani mkuu, mimi bado ni wa hiace tu bado sijafikia budget ya 40 mil
 
Mimi pia wa Kigoma njoo nikuuzie hii yangu iko shinyanga inapiga kazi. Kwa ruti ya kibondo to Is hapo ngoja niifiatilie ili nami niiweke hapo kama sikupata mteja wa haraka maana nahitaji pesa ya haraka na huko iliko nilifuata ubora wa barabara ili gari idumu ila sasa mzunguko sio mzuri. Kama ukiamua kuagiza nje safi hata Mimi nimeagiza mwaka Jana. Sikupenda za Dar huwa wanaleta muozo. Nilishangaa nikiwa Temeke gereji kufunga siti wateja wanaitaka na wakanambia kuwa hii sio ya showroom za hapa, ila uwe makini ukifuaya bei chee Italia alafu petrol ni nzuri injini haichemki na ukipata 2rz utatisha. Kazi njema ukipenda njoo nikuuzie maana hapo kgm wanaiogopa upya wanahisi being akua juu sana. Kgm wananinua used yoka mwanza na kahama zilizo choka. Vinginevyo asante kunionesha ruti ya kibondo hii ndege ndio inamudu izo mambo. Picha hii tukutane road babu.,
Mkuu Mzalendowadamu, kwa nini gari umelipeleka huko? Vumbi si hoja mkuu, kama dereva wako ni mzuri haina shida kabisa. Pia ruti za kigoma ni nzuri kwa sababu zina nauli kubwa.

Pia bado nipo kwenye stage ya kufanya tafiti ya biashara hii ili ikinipendeza ninyofoe hela sehemu na kuagiza japan. Shukrani kwa offer ya kutaka kuniuzia.
 
Toyota Hiace Van 1997

Mkuu, kama unataka kufanya biashara ya Hiace, chukua hii gari. Gari bado mbichi kabisa. Nimejaribu kuchek kwenye mitandao mbali mbali, gari nyingi zimetembea kuanzia km 250,000.
Kwa gari hii ukipata dereva mzuri itapiga kazi hata kwa zaidi ya miaka mitano! Ila chonde chonde baba, kumbuka kukata bima kubwa.
Pesa ukiwaomba jamaa wakutumie profoma watakutumia ukalipie pesa benki. Usimpe mtu yeyote pesa mkononi isipokuwa zile clearing fees za kumpa agent. Gari ikifika jitahidi ushuru ukalipe mwenyewe. All in all kila la kheri.
Mkuu Nichumu Nibebike , nashukuru sana kwa ushauri mkuu. I hope nitapata niingie katika biashara hii japo watu wa JF wanapenda sana kusema kwamba ni pasua kichwa.
Mpango wangu research yangu ikikamilima na kuona kuwa inalipa vizuri nategemea kuagiza toka Japan.
 
Rekebisha hapo kwenye Usaforishaji iwe Usafirishaji; unaandika bila kuhakiki, aaaah bhana usiwe na haraka kama mchomoko wako
Mkuu Mungu Mweusi hiyo heading ukikosea huwezi kurekebisha mpaka mods. Ntaomba mods msaidie.

Pia naomba uchangie kujibu baadhi ya maswali yangu mkuu.

Thanks kwa masahihisho!
 
Umuofia kwenu!

Jamani mimi ni employee katika private sector. Katika kufikiria namna ya kujiongezea kipato nimewaza kukopa pesa benki ili niagize hiace na nianze kupiga ruti za Kasulu-kigoma au kasulu-kibondo. Hii Biashara sijawahi kuifanya ila nategemea kuisimamia baada ya kutafuta dereva anayeweza kuaminika.
Ningependa kujua yafuatayo;
1. Hiace aina gani inayofaa?
2. Kwa mazingira ya Kigoma engine gani inafaa? CC zake pia aina ya mafuta (diesel/petrol)
3. Profit margin ya huku ikoje, katika misimu ya mvua na kiangazi?
4. Ningependa kujua pia kuhusu bima ya gari ya Biashara kama hii ya hiace, especially comprehensive/premium ikoje?
5. Kama nimenunua from Japan, gharama ya kuweka viti vya abiria ikoje?
6. Pia ningependa pia kujua chochote kile kinachohusiana na biashara hii kutoka kwa wazoefu/majongwe wa biashara hii.

NB:
Kasulu-kigoma ni 90 km na nauli ni Tsh. 5,000/= na
Kasulu -Kibondo ni 150 km na nauli ni Tsh. 10,000/=.
Barabara zote ni za vumbi na gari linaweza likaenda na kurudi kwa siku bila shida.

Thanks!
Mkuu hivi hice shingapi?
 
Mkuu hivi hice shingapi?
Ukicheki kwenye mitandao ya japan bei zake zinaweza kukugharimu kuanzia 18 mil mpaka 30 mil. Tofauti hiyo ya bei ni kutokana na ubora wake.
Hizi ni gharama mpaka unaiweka barabarani.
 
kwa mahesabu m ya haraka kama gari nenda rudi hadi anafunga kazi ukitoa ela ya mafuta dereva mkononi ana 150000 hiyo ruti ya km 90
na gari hiyo ruti ya km 150 kwa gari ya mkopo pesa toka bank haikufai japokuwa ina faida zaidi
swari je ataweza kuleta hesabu ya laki moja kira siku kumbuka kwa dsm hiyo ni hesabu ya costa na hiace kwa dar mpya ni hesabu ni kati ya 50 mpk 60 kumbuka hiyo njia ya vumbi hivyo hesabu lazima iwe kubwa 7bu unaiua gari haraka lkn faida inakuja na kwa gari ya mkopo ili uone matunda inakupasa mkopo uwe wa mwaka mmoja tu
je ulivyofanya survey yako inawezekana dereva kuleta hesabu laki 1 ?
 
Mkuu kama una 40mil nipigie simu nikuunganishe upate tata abiria 45 kwa mkopo ambapo unakuwa unarejesha milioni6 kwa mwezi na kwa mwaka mmoja
Kaka hv tata marcopolo mpya being gan plz?
 
kwa mahesabu m ya haraka kama gari nenda rudi hadi anafunga kazi ukitoa ela ya mafuta dereva mkononi ana 150000 hiyo ruti ya km 90
na gari hiyo ruti ya km 150 kwa gari ya mkopo pesa toka bank haikufai japokuwa ina faida zaidi
swari je ataweza kuleta hesabu ya laki moja kira siku kumbuka kwa dsm hiyo ni hesabu ya costa na hiace kwa dar mpya ni hesabu ni kati ya 50 mpk 60 kumbuka hiyo njia ya vumbi hivyo hesabu lazima iwe kubwa 7bu unaiua gari haraka lkn faida inakuja na kwa gari ya mkopo ili uone matunda inakupasa mkopo uwe wa mwaka mmoja tu
je ulivyofanya survey yako inawezekana dereva kuleta hesabu laki 1 ?
Mkuu, kitabakilo ufuatiliaji wa mwanzo unaonyesha kupata 100,000 kila siku inawezekana kabisa tena hayo ni makadirio ya chini. So long as unawafanya kazi wazuri na ukawa manage vizuri.
 
Mkuu, kitabakilo ufuatiliaji wa mwanzo unaonyesha kupata 100,000 kila siku inawezekana kabisa tena hayo ni makadirio ya chini. So long as unawafanya kazi wazuri na ukawa manage vizuri.
PATA UZOEFU HUU
Mkuu biashara ya HIACE nzuri ila ubaya unakuja ukiwa una kazi ya ziada na unategemea hiace halafu umempa dereva gari ukitegemea kila siku hataleta pesa kama ulivyopanga HIACE nzuri ya kuagiza mpk kufika mkononi na kufanya kazi ni kati ya mln 25 mpk 30 katika biashara ya daladala ukiwa unaanza zingatia mambo haya hasa kama ya mkopo ili ufikie malengo bila kufeli.

Katika siku 365 za mwaka toa siku 52 kuwa gari haitafanya kazi inamaana katika wiki siku 1 haifanyi kazi(hapa unielewe haimaanishi kila wiki ipumzike ila kuna service(kumbuka service bora ni ya kilomita sio kuhesabu siku)
kuna kuharibika pakubwa gari ikakaa hata siku tatu inatengenezwa kuna kukamatwa ikakaa police na dharura nyingne ) hivyo piga hesabu gari itafanya kazi na kuleta pesa siku 300 tu katika mwaka

Ina maana kwa mkopo wa kuweza kupata HIACE nzuri ili umalize mkopo kwa mwaka 1 rejesho kwa mwenzi ni ni km mln 2.7 ina maana kwa uwiano wa kila siku kwa mahesabu ya juu hapo ni 115000/= ndio maana nikauliza dereva anaweza kuleta laki kwa siku.

HIACE ya DIESEL manual ni nzuri kibiashara ila HIACE ya petlor ni nzuri kwa kudumu ila itakuumiza kwnye mafuta

lkn kumbuka gari kudumu si kukaa miaka mitano au mitatu ni kilomita inazotembea ndo maana nikakwambia kwa hiace ya mkopo usiipelele ruti ya kilomita nyingi itakucost mbele coz utapotaka kuuza isiwe imechoka sana

nyingne kumbuka barbara yoyote ya vumbi inaua gari halaka hivyo kuwa na tagert fupi yaan ukimaliza mkopo gari ifanye kazi muda fulani uuze uongeze pesa ununue mpya

huko kasulu sipajui ila nina uzoefu tu wa barabara nyingi za tanzania zinafanana ni kiwango cha kokoto vishiringi kibao bodi inachezacheza
 
Salute wakuu,

Nahitaji kufanya biashara ya daladala hapa mjini DSM.

Nijuzeni bei za hiace na coaster mpya, ama kama imetembea mwaka mmoja ama miwili.

Kati ya kununulia tanzania na nje wapi pako poa?

Na changamoto kubwa za hii biashara.



Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom