Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Achana na retail, Panga mlango mku kuu nje kidogo ya jiji (hauna gharama kubwa) nenda kwa wahindi nunua compressor mpya kubwa ya kujazia upepo tairi za magari (mara ya mwisho kuuliza bei ilikuwa ni laki 850) nunua machine ya kuchajisha betry (laki nne na nusu nadhani) nunua chupa za maji ya petri na oil chupa ndogo ndogo ongeza na oil chafu kidogo. Nunua tairi kuu kuu saizi ya madaladala yanayofanya roots sehemu ilipo fremua yako (hizi zitakusaidia daladala inakuja na pancha unamuazima tire zako aendelee na biashara wakati unaziba ya kwake kujenga mahusiano mazuri), Nunua tire rippers, ajiri kijana mmoja anza kazi iwe 24hrs. Baada ya miezi sita leta mrejesho hapa.
Safi kaka a kompresa nimeipendd

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hii biashara unaijua vizuri nimekukubali, sema ndugu yangu hakuna biashara rahisi. Kwa mfano hyo ya genge nayo ni pasua kichwa kinoma. Vitu vinaharibika sana usipokua na wateja wa kutosha.
Hapana mkuu bimafsi nimekuwa nafanya biashara ya genge,linalipa kwa nqmna yake,ila ukitaka kulifa ya lipate faida hiyo ni ww uwe wa kufata mzigo directly kwa mkulima
 
Habari zenu wakuu

Kwa wakazi wa songea mjini ,Nina wazo la kutaka kuanzisha duka la rejareja vitu vya matumizi ya nyumbani .
Tatizo Mimi sio mwenyeji sana songea hii , nilikuwa naomba kama kuna mwenyeji aniambie location nzuri nayoweza kufanyia biashara hii na frame pia ziwe zinapatikana.
Lakini pia kama Una idea nzuri tofauti na hili unaweza nishauri.
Asanteni wakuu .

Mtaji wangu ni mil 1.5
Mkuu ulifanikiwa kupata Fremu Songea
 
Kila kitu kinategemeana hao wachuuzi ndo wanaosaidia bidhaa za viwandani kuwafikia walaji so msi discourage watu na idea zao. Wachaga wanakuwa mabilionea kwa maduka hayo hayo ya reja reja cha muhimu nidhamu
 
Habarin ndugu naomba ushauri kwa wenye ujuzi na uzoefu,nahitaji kufungua duka la bidhaa kwa jumla na lejeleja sasa naomba msaada wa maligafi za mahitaji ya kununua Especially vyakula.
 
Habarin ndugu naomba ushauri kwa wenye ujuzi na uzoefu,nahitaji kufungua duka la bidhaa kwa jumla na lejeleja sasa naomba msaada wa maligafi za mahitaji ya kununua Especially vyakula.
Uko wapi?
Bajet ?
Ushasajili
 
Mkuu kama umefanikiwa,naomba kwa unyenyekevu uliotukuka,unimegee na mm ujuz huo
 
Mkuu kama umefanikiwa,naomba kwa unyenyekevu uliotukuka,unimegee na mm ujuz huo
Nilifanikiwa mkuu naendelea mdogo mdogo. Kifupi bidhaa huwa nanunulia maduka ya jumla pale Manzese Tip top na darajani na ndo nilienda kuna wauzaji waungwana sana wakanipa list zote na utaratibu wa kupanga bei.

Kuna jamaa walijitokeza humu kunisaidia ambao nilitaka niwape elfu 40,000 ila nikaona wazugaji tu. Mara tuma kwanza pesa mara njoo tuonane hii kasi sio rahisi kama unavyofikiri na wakati mimi nilitaka mtu aniandalie excel file yenye bidhaa zote na bei ya kununulia na kuuzia na wapi nikanunue alafu nampa hiyo 40,000 simple tu. Watu wagumu kweli. Baada ya kuona longo longo hizi na mimi ni mtu aisiyetaka complication na mtu wa kuyaona mambo hata magumu kuwa ni marahisi nikaachana nao nikaingia mwenyewe chimbo madukani na kwenye maduka ya akina mangi na kuulizia. Wengine walinifukuza na wengine walikataa kata kata hata kwa kuwalipa. Ila kwa vile penye nia pana njia nilifanikiwa. Na kwa vile sina hiyana na tamani watanzania wenzangu watamanio kuifanya hii biashara waifanye bila longo longo nyingi nimeweka hapa baadhi ya bidhaa ambazo nimezidowload kwenye accounting software ninayotumia dukani. So far so good nilianza na mauzo ya siku ya kwanza ya shilingi 10,200 nikala faida ya buku mbili kwa siku na kwa sasa in average mauzo ni 70,000 kwa siku with average profit ya 30% ambayo ni 21,000 kwa siku.

Nenda kafungue mkuu na niulize nikwambie ninayoyajua so far kwa hii experience ya miezi mitatu.

Karibu sana

Mkomamazu
 

Attachments

Back
Top Bottom