Biashara ya Kamari: Mbadala wa Dawa za Kulevya?

Biashara ya Kamari: Mbadala wa Dawa za Kulevya?

usijaribu mkuu.., nenda kafanye uzalishaji Mali na huduma tafadhali, taifa linakutegemea!

Wakafanye uzalishaji wapi hawana creativity ya business idea, Any profitable project, Hawana mitaji hata akibett akapata 10m ataenda samaki samaki after one week atarudi betting tena.
 
Wewe dogo miyayusho na mpotoshaji kuna siku uliandika hapa watu wa kamari za betting hizi tulizonazo wanavuna zaidi ya bilion kwa siku

ule ulikua uongo dogo jumapili mojawapo nilifika pale kariakoo kwenye premium betting hapa kushoto ukiingia ndio kuna kompyuta kubwa nikaangalia mauzo yalikua ni milion 20 hapo ndio top haya ya jumamosi siku ambayo mauzo ndio huwa juu nikaangalia siku hiyo walilipa milion 30+ hapo wale wa kawaida acha wale wa juu kuanzia milioni na kuendelea

na kuhusu addicted nilianza kubet online kabla ya mashine hizi kuja ila nimeacha sio kama unavyotaka kuamimisha watu.

Hakyanani hujaacha,wewe unajifaragua tuu.
 
Kwa wale ambao mmeshawahi kusikia namna 'punda' wa 'sembe ya mwakyembe' wanavyo 'packiwa' mizigo ya kusafirisha mtakubaliana na mimi kwamba biashara hii 'takatifu' ina faida kubwa iliyotukuka(Muulizeni first boy). Ni ukweli unaosikitisha kwamba 'pipi' za 'sembe' hushindiliwa kupitia njia ya nyuma mpaka tumbo lijae kisawa sawa, udhalilishaji!

Sasa turudi kwenye mada, habari za uhakika kutoka kwa mmoja wa wazungu wanaomiliki makampuni ya kamari hapa nchini, zimevujisha kwamba, Kamari ya mpira ni 'addiction' mpya ambayo imekuwa purposely introduced globally ku-replace madawa ya kulevya, biashara hii ya kamari ina faida mara tatu kuliko madawa ya kulevya, na gharama za uendeshaji pia ni robo tu ya gharama ya kusafirisha na kuuza madawa. (And its just as addictive as madawa, ukianza huachi mpaka kufa!)

Mzungu huyo ameweka wazi kwamba, biashara ya madawa kote duniani (hata Tanzania) hufanyika with the full knowledge and support ya vigogo wa serikali, kuanzia Rais mpaka mawaziri husika, ilimradi tu unapeleka due deligence kwa hao vigogo wanaokulinda, na kwamba wale wanaokamatwa hufanya biashara hii bila kupeleka ada (due deligence) kwa wahusika wenye dhamana ndani ya nchi husika, amesema kwa hili, hata Obama hawezi kukwepa (Gharama za uchaguzi ni kubwa mno!).

Mtandao huO wa 'kingpins' ulifanya uchunguzi hivi karibuni na kugundua kwamba, addiction kupitia madawa japo inawatajirisha madhara yake kwa dunia ni kubwa mno kiujumla!, nguvu kazi inapotea kiasi kwamba hizo fedha nyingi huishia kutibu madhara yaliyosababishwa na madawa (Mfano ukikabwa na teja akakutoa utumbo kwa sababu ya Iphone,ili yeye akapate dawa), hivyo biashara hii imepoteza viability. Amevujisha kwamba ma 'king pin' wa biashara hii wameamua ku-eradicate 'addiction' ya madawa hapa duniana na ku-'re enslave' the masses kwa kutumia addiction mpya iliyoboreshwa ya mpira na michezo kiujumla. (its better in every perspective).

Katika kutekeleza hili, matrillioni ya pesa yametengwa ili kuongeza idadi ya vituo vya kugawa 'methadone' kwa gharama nafuu kabisa, ili nguvu kazi hii iache kutumia madawa na badala yake waende kwenye 'addiction' ya kamari. (Kama hujaanza mshukuru unaemwabudu, na akulinde usiingie huko, naapa kwa jina la unaemwamini, utajuta, kwani huwezi kuacha!), YOU WILL BE ENSLAVED!

Kwa sasa tunaweza tukajifariji, kwani amenihakikishia, baada ya miaka mitano, hakuna mtu atakaweza kupata access ya madawa popote pale duniani, kwani hakuna kitu kinafanyika bila wa kujua, na badala yake, 65% ya vijana watakuwa wakijishughulisha na 'kusuka mikeka' badala ya kufanya shughuli za uzalishaji bidhaa na huduma. Consequently uchumi wa mataifa (hasa vichwa vya panzi kama 'wadanganyika', stupid kabisa!) utayumba kutokana na watu kutofanya kazi, lakini uchumi wa mataifa yanayomiliki hizi betting systems (hasa wazungu) utapaa kama mbayuwayu. YOU'VE BEEN WARNED!

DON FRANCIS

Kitaalum aina yoyote ya mchezo wa kamari unapoucheza kwa muda mrefu na ikiwa ndo kipaumbele chako kwa kila sekunde, saa, siku, wiki, mwezi, miezi, mwaka n.k tayari unakuwa umeathirika na unakuwa tegemezi wa kamari, hapo ndo mtu tunasema amekuwa na "GAMBLING ADDICTION" na inatibiwa kama aina ya ADDICTION YOYOTE kama ulivyotoa mfano wa dawa za kulevya, na mi naongezea pombe (alcohol), ngono (sex), sigara (nicotine), wizi, umbea, ulafi (greed), kiherere (co-dependency), chuki (jealousy), hasira (anger), manunuzi na matumizi (buying & spending), kazi (work), matumizi ya kahawa (caffeine), ugomvi (violence), dini (spititually), wasiwasi (worry), mawazo mgando (riggid thinking), chakula (food), mapenzi (love), nk mengine unaweza kuongezea.

Kuhusu "methadone" hii ni dawa inayotumiwa wa waathirikiwa wa madaya ya kulevya hasa cocaine na heroine kupunguza hamu (craving) ya dawa hizo, pia kitaalum nazo ziko katika mfumo wa dawa (drug) so ukitumia kwa muda mrefu pia nazo ugeuka kuwa tegemezi kwa mgonjwa na kusababisha ADDICTION, kwa maana hiyo nazo zinatakiwa kutumiwa kwa uangalifu na kwa usimamizi kwa hali ya juu toka kwa mtu mwenye taaluma hasa ya masuala ya utegemezi wa vitu (addiction) kwa bahati mbaya hapa nchini watu wanatumia hizo dawa bila ya hiyo tahadhari matokeo yake baada ya muda tutegemee WATU WALIOACHA DAWA ZA KULEVYA LAKINI WAKIWA TEGEMEZI WA DAWA YA "METHADONE" KWA MAISHA YAO YOTE.

Mwisho kwa mwathirika wa michezo ya kamari "GAMBLING ADDICTION" huyu hutumii methadone, bali anahitaji kitu kiitwacho recovery program from gambling addiction kutoka kwa wataalum wa saikolojia ambao kwa nchi za wenzetu wanapatika katika hospital za rufaa au vituo vya maalum vya uangalizi wa watu kwa muda maalum (sober house or rehabilitation centres)
 
Ndiyo nilimwambia mleta uzi Mwanzoni Kuwa uwe teja, mchezo kamari, kufuta sigara, kupiga chabo, kupiga nyeto,kula sana. ..addiction zote hizo Ktk recovery program watibiwa Au kupewa somo wakiwa pamoja.
 
Wakafanye uzalishaji wapi hawana creativity ya business idea, Any profitable project, Hawana mitaji hata akibett akapata 10m ataenda samaki samaki after one week atarudi betting tena.
Hiyo ni kawaida kwao ni kama ajira kwao
Na syo betting tu hiyo ya mpira, Kuna watu wanacheza kamali za makasino wanapiga hela ndefu wanaishi maisha ghali wanafilisika wa narudi tena...hayo Ndiyo maisha waliyoyachagua
 
Mrangi
Maisha waliyoyachagua? Sidhani. Wengi waliingia kwa bahati mbaya tu. Wakajikuta wanashindwa kutoka.

Nenda pale las vegas, legrande, new africa, princess, sea cliff, etc, uone watu walivyoathirika na compulsive gambling. Kamari ni janga. Hizo betting za mpira hela yake ni ndogo. Kwenye makasino ni habari nyingine.
 
Ninabet, ninafanya kazi na sioni kama kuna addiction yoyote hapo. Kwa mfano, teja hawezi maliza siku bila kubwia unga, ila mimi naweza nikakaa hata wiki sijabet na sioni athari zozote zile..

Ukila unga unakuwa affected healthily and psychologically lakini kubet sioni kama ina athiri chochote unless ufanye kubet kama ni kazi yako ya msingi na si mchezo kama michezo mingine.. Anyway katika kubet pesa niliyopata ninakaribia kununua kavits sasahivi. Kubet kunanisaidia sana kiafya na kiuchumi, sababu nime divert yale matumizi ya weekend ya bia na nyama na kuhonga wahudumu na marafiki kule bar nimeamishia hilo fungu kwenye betting na huwa linanipa faida. Mwanzoni weekend ilikua inanimalizia hadi laki kwa kima cha chini lakini sasa napata zaidi ya laki kama faida kila weekend.

All in All kubet sio mashindano wala full time job, ukiendekeza unafilisika na utaishia kubwia unga

Hongera kwa kutokuwa mraibu bado.

Ila tofautisha uraibu na matumizi, unaweza kuwa mtumiaji wa kamari, sigara, madawa, pombe na usiwe mraibu. Uraibu huanza polepole hadi gari inakolea... Mahali ninapoishi niko na sehemu ya kubet jirani na kwa vile mimi ni mpenzi wa soka tunakutana na makamaria mabandani.

Kuna watu wameathirika mwanangu, muda wote wanawaza mikeka, wanashinda huko na hawataki kazi za nguvu kwa kuwa kamari ile ina ahadi ya fedha kubwa bila jasho.

Kamari inaleta matumaini ya 'ipo siku' hivyo kuwafanya vijana kutoheshimu fedha ndogondogo wanazopata hapo kwa imani kuwa ipo siku mkeka utajibu atapata milioni kadhaa!
 
my point exactly..!
 
Mrangi
Maisha waliyoyachagua? Sidhani. Wengi waliingia kwa bahati mbaya tu. Wakajikuta wanashindwa kutoka.

Nenda pale las vegas, legrande, new africa, princess, sea cliff, etc, uone watu walivyoathirika na compulsive gambling. Kamari ni janga. Hizo betting za mpira hela yake ni ndogo. Kwenye makasino ni habari nyingine.

Huko ni balaa watu wanaacha mpaka magari na wanaweza nyumba bond kamari hiyo
 
Hongera kwa kutokuwa mraibu bado.

Ila tofautisha uraibu na matumizi, unaweza kuwa mtumiaji wa kamari, sigara, madawa, pombe na usiwe mraibu. Uraibu huanza polepole hadi gari inakolea... Mahali ninapoishi niko na sehemu ya kubet jirani na kwa vile mimi ni mpenzi wa soka tunakutana na makamaria mabandani.

Kuna watu wameathirika mwanangu, muda wote wanawaza mikeka, wanashinda huko na hawataki kazi za nguvu kwa kuwa kamari ile ina ahadi ya fedha kubwa bila jasho.

Kamari inaleta matumaini ya 'ipo siku' hivyo kuwafanya vijana kutoheshimu fedha ndogondogo wanazopata hapo kwa imani kuwa ipo siku mkeka utajibu atapata milioni kadhaa!
Ni kawaida kwa addicts kujifariji.., we muelewe tu..
 
Wewe dogo miyayusho na mpotoshaji kuna siku uliandika hapa watu wa kamari za betting hizi tulizonazo wanavuna zaidi ya bilion kwa siku

ule ulikua uongo dogo jumapili mojawapo nilifika pale kariakoo kwenye premium betting hapa kushoto ukiingia ndio kuna kompyuta kubwa nikaangalia mauzo yalikua ni milion 20 hapo ndio top haya ya jumamosi siku ambayo mauzo ndio huwa juu nikaangalia siku hiyo walilipa milion 30+ hapo wale wa kawaida acha wale wa juu kuanzia milioni na kuendelea

na kuhusu addicted nilianza kubet online kabla ya mashine hizi kuja ila nimeacha sio kama unavyotaka kuamimisha watu.
Yaan walikupa wewe access ya database zao uangalie mauzo yao na wewe ukaamini.., kwa hesabu za haraka haraka tu, hizo data ni za uongo!
 
Yaan walikupa wewe access ya database zao uangalie mauzo yao na wewe ukaamini.., kwa hesabu za haraka haraka tu, hizo data ni za uongo!

wewe dogo hata hujui unaongelea nini utajua mwenyewe kaombe tra data zao kama unabisha
 
Mwenye masikio na asikie!

Hapo zamani, alikuwepo mfalme wa nchi moja. Mfalme huyu aliwaita watu wote wenye busara kwenye nchi yake na kuwaambia naamini nyinyi ndio mna busara sana, nataka make chini na mtengeneze falsafa ya maisha ambayo kila mtu kwenye ufalme wangu ataishi nayo na itamletea mafanikio.
Watu wale wenye busara walikwenda kukaa na baada ya muda wakarudi kwa mfalme wakiwa na vitabu 12 vilivyoelezea kila kitu kuhusu falsafa ya maisha. Mfalme aliwaambia naamini mlichoandika kwenye vitabu hivyo ni kizuri sana, lakini watu hawawezi kusoma vitabu 12, ni vingi mno. Nendeni mkapunguze ili iwe rahisi kwa watu kusoma. Watu wale waikwenda kukaa tena wakarudi na vitabu sita, mfalme aliwaambia bado ni vingi mno. Wakaenda kukaa na kurudi na kitabu kimoja, bado mfalme akawaambia ni kirefu. Wakaena kukifanyia kazi na wakarudi na sura moja, bado mfalme hakukubali, alisema ni ndefu mno. Wakaenda kukaa na kuja na aya moja, bado mfalme hakuikubali. Walirudi tena kukaa na safari hii walikuja na sentensi moja tu. Mfalme alipoipokea sentensi ile na kuisoma alitikisa kichwa kwa kukubali na kusema hii ndio falsafa ya maisha ambayo kila mwananchi kwenye ufalme wangu anapaswa kuishi nayo.

Sentensi yenyewe ilikuwa inasema HAKUNA KITU CHA BURE. Kama kila mtu angeweza kuishi kw afalsafa hii, hakika tusingekuwa na matatizo makubwa ambayo yanatusumbua sasa. Hakuna kitu cha bure, ili upate kitu ni lazima ulipe gharama.

SOMA; Barua Ya Wazi Kwa Vijana Wanaotafuta Ajira. Soma Hapa Uone Fursa Unazoweza Kutumia.

Sasa kwa sababu ambazo hazieleweki sasa hivi watu wanaamini kwmaba wanaweza kupata kitu bila ya kutoa kitu. Watu wanaamini kwamba wanaweza kupata fedha bila ya kufanya kazi yenye kuzalisha thamani kwa wengine.

Kuna biashara moja ambayo inakua kwa kasi sana hapa Tanzania. Biashara hii inawaoa faida wachache na kuwaumiza wengi. Biashara hii inakwenda kinyume kabisa na falsafa hiyo muhimu ya maisha kwamba hakuna kitu cha bure.

Biashara ninayozungumzia hapa ni kamari iliyohalalishwa na kupewa jina la BETING. Beting ni kamari na biashara hii au mchezo huu unaliangamiza taifa. Tunahitaji kuwa makini sana, vinginjevyo tunakwenda kutengeneza taifa la ajabu sana.

Kwa nini beting ni biashara hatari sana?

1. Hakuna thamani yoyote inayozalishwa.

Ili biashara iwe halali, inahitaji kuwa inazalisha thamani kwa watu wengine. Kwa mfano mtu analima shamba, anaweka mbegu, anapalilia, anaweka mbolea anavuna kisha anauza mazao yake, huu wote ni mzunguko wa thamani. Lakini ukija kwenye beting, mtu anabashiri kwamba mchezo kati ya arsenal na liverpool, arsenal watashinda, sasa hebu niambie wewe kusema arsenal watashinda umetengeneza thamani gani?

2. Biashara hii inatengeneza uteja.
Tatizo kubwa sana la biashara hii hasa kwa wale ambao wanabet ni kwmaba kuna uwezekano mkubwa sana wa kutengeneza uteja. Kwa mfano mtu anaweka shilingi mia tano na kutabiri michezo kumi na nne, kama akipatia yote basi anapata shilingi laki moja. Baada ya michezo hiyo 14 aliyobashiri, anapatia michezo 13 na kukosea mmoja. Mtu anaona dah, nilikuwa karibu sana kuipata laki moja, ngoja nijaribu tena najua nitashinda. Hali ya namna hii inamfanya mtu kuendelea kuwa mteja na wakati mwingine kushindwa kujizuia.

SOMA; Katika Kula Ujana Usifanye Mambo Haya Matano, Utajutia Maisha Yako Yote.

3. Vijana wameanza kuichukulia kama sehemu ya kuingiza kipato.

Sasa hivi vijana wanachukulia beting kama sehemu ya kujiingizia kipato. Kijana anaitafuta shilingi elfu mbili na kwenda kubet akijua kwamba anaweza kuondoka na fedha nyingi hata mamilioni. Hizi ni akili za ajabu sana, beting haiwezi kuwa sehemu ya kipato hata siku moja. Mtu pekee mwenye uhakika wa kuingiza kipato kupitia beting ni yule anayechezesha. Yeye anachofanya ni kukusanya fedha zenu, kuondoa gharama zake za kuendesha na faida yake kisha kuwagawia wachache kile kinachobaki.

4. Biashara hii sasa inafanyika kila mahali.
Kitu kingine kinachofanya biashara hii kuwa hatari sana ni kwamba inafanyika kila mahali mpaka kwenye mitaa ya ndani kabisa. Eneo ninaloishi mimi kuna sehemu hizi za kubet kama nne na hazipo kwenye umbali mkubwa. Hii inatoa nafasi kwa kila mtu kujiingiza kwenye mchezo huu hatarishi. Na kadiri watu wanavyosimuliana kwamba unaweza kushinda fedha nyingi, ndivyo wanavyozidi kufurika kwenye biashara hii.

Najua biashara hii sio mpya hapa Tanzania, lakini zamani ilikuwa inafanyika kwenye kumbi kubwa za starehe, Casino, na hivyo waliokuwa wanacheza hii michezo ni watu ambao wanastareheka. Ila sasa hivi imeletwa mitaani kabisa na hata asiye na uhakika wa kipato cha kesho anakwenda kubet.

SOMA; BIASHARA LEO; Usitupigie Kelele, Tupe Sababu.

5. Watoto nao wanajiingiza kwenye huu mchezo.
Ni hali ya kusikitisha sana kwamba sasa hivi hata watoto wa shule nao wanacheza mchezo huu wa kubet. Kumbuka huyu mtoto hana chanzo chochote cha kipato, ila fedha kidogo anayopewa anashawishika kwamba anaweza kuizalisha na ikawa nyingi. Sasa hatari kubwa itakuja pale ambapo watakuwa wameshakuwa wateja na wakose fedha ya kwenda kucheza, wataiba.
Hatari nyingine kwa watoto, hivi kama mtoto anafikiria kwamba anaweza kuweka mia tano, akatabiri vizuri kisha akapata laki moja au mpaka milioni, ana sababu gani ya kwenda kukaa darasani na kusoma kwa juhudi ili aweze kutengeneza kipato chake mwenyewe? Mchezo huu unaua kabisa msingi wa uwajibikaji ambao watoto wanatakiwa kujengewa. Kama mtoto atakua kwa msingi kwamba anaweza kupata fedha bila hata ya kufanya kazi, ni vigumu sana kuja kumwaminisha tofauti baadae na tunatengeneza taifa la watu wazembe kupitiliza.
Biashara hii ni hatari sana tena sana, na sababu za uhatari wake zipo nyingi sana.
SOMA; Vitu VIWILI Ambavyo Tayari Unavyo Na Vinavyoweza Kukufikisha Popote Unapotaka KWENDA.
Tufanye nini sasa ili kujiokoa na janga hili?
1. Epuka kabisa kujihusisha na biashara hii. Usibet na pia usifungue biashara ya watu kubet, utapata faida ila utaharibu taifa. Usije ukashawishika kwa namna yoyote ile kwamba unaweza kufaidika kwa kubet. Hakuna.
2. Tuwasaidie wenzetu ambao wameshaingia kwenye mchezo huu. Hii ni kazi ngumu sana lakini tusiache kuifanya. Nimekuwa nikiongea sana na vijana ninaowakuta wakibet, wengi wao wana imani kubwa sana na chochote unachomwambia kuhusu ubaya wa mchezo huu hakuamini kabisa. Huyu ni mtu ambaye amewahi kushinda mara moja au mara chache lakini ukilinganisha na idadi aliyoshindwa ni kwamba anapoteza.
3. Tupinge biashara hii. Kila mmoja wetu kwa uwezo wake, tupinge biashara hii. Tuitake serikali iondoe hii biashara mitaani na irudishwe kwenye maeneo maalumu ambayo wanaokwenda kucheza ni wale ambao wananielewa kweli. Kuiacha huku mitaani inaendelea kuharibu kabisa taifa.
Hakuna kitu cha bure, ni lazima utoe kitu ndio uweze kupata kitu. Biashara yoyote unayofikiria kufanya hakikisha inatoa thamani kwa watu wengine na kwako pia. Kinyume na hapo hiyo siyo biashara bali ni kitu hatari kinachoweza kuwaangamiza wengine.
Mafanikio hayaji kwa kukaa chini na kutabiri timu gani itashinda, mafanikio yanakuja kwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa na kuzalisha thamani. Nawatakia kila la kheri wale wote ambao wanajua kazi ndio msingi wa maendeleo. Tusikubali kuondolewa kwenye falsafa yetu hii.
TUPO PAMOJA,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Hongera kwa kutokuwa mraibu bado.

Ila tofautisha uraibu na matumizi, unaweza kuwa mtumiaji wa kamari, sigara, madawa, pombe na usiwe mraibu. Uraibu huanza polepole hadi gari inakolea... Mahali ninapoishi niko na sehemu ya kubet jirani na kwa vile mimi ni mpenzi wa soka tunakutana na makamaria mabandani.

Kuna watu wameathirika mwanangu, muda wote wanawaza mikeka, wanashinda huko na hawataki kazi za nguvu kwa kuwa kamari ile ina ahadi ya fedha kubwa bila jasho.

Kamari inaleta matumaini ya 'ipo siku' hivyo kuwafanya vijana kutoheshimu fedha ndogondogo wanazopata hapo kwa imani kuwa ipo siku mkeka utajibu atapata milioni kadhaa!
mkuu huo ni ukweli kabisa hata mimi nimekua ni muhanga wa hii kitu
 
Back
Top Bottom