kawombe
JF-Expert Member
- Mar 26, 2015
- 14,239
- 15,876
Cc: Sport pesa
Tunalipia kodi mkuu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Cc: Sport pesa
Nyie ni mateja tu, ukweli ndio huo.., kulipiwa kodi sio sababuTunalipia kodi mkuu
News Alert: - Wazee Arosto la kubeti halina tofauti na kuvuta unga (cocaine)Miyeyusho mingine bwana,mtu anatunga stori,anaitupia huku ila kutaka attention zetu
Nakubaliana na wewe michezo ya Bahati na Nasibu na Kamali, hutengeneza tajiri mmoja na maskini wengi.Kwa wale ambao mmeshawahi kusikia namna 'punda' wa 'sembe ya mwakyembe' wanavyo 'packiwa' mizigo ya kusafirisha mtakubaliana na mimi kwamba biashara hii 'takatifu' ina faida kubwa iliyotukuka. Ni ukweli unaosikitisha kwamba 'pipi' za 'sembe' hushindiliwa kupitia njia ya nyuma mpaka tumbo lijae kisawa sawa, udhalilishaji!
Sasa turudi kwenye mada, habari za uhakika kutoka kwa mmoja wa wazungu wanaomiliki makampuni ya kamari hapa nchini, zimevujisha kwamba, Kamari ya mpira ni 'addiction' mpya ambayo imekuwa purposely introduced globally ku-replace madawa ya kulevya, biashara hii ya kamari ina faida mara tatu kuliko madawa ya kulevya, na gharama za uendeshaji pia ni robo tu ya gharama ya kusafirisha na kuuza madawa. (And its just as addictive as madawa, ukianza huachi mpaka kufa!)
Mtandao huo wa 'kingpins' ulifanya uchunguzi hivi karibuni na kugundua kwamba, addiction kupitia madawa japo inawatajirisha madhara yake kwa dunia ni kubwa mno kiujumla!, nguvu kazi inapotea kiasi kwamba hizo fedha nyingi huishia kutibu madhara yaliyosababishwa na madawa (Mfano ukikabwa na teja akakutoa utumbo kwa sababu ya Iphone,ili yeye akapate dawa), hivyo biashara hii imepoteza viability. Amevujisha kwamba ma 'king pin' wa biashara hii wameamua ku-eradicate 'addiction' ya madawa hapa duniana na ku-'re enslave' the masses kwa kutumia addiction mpya iliyoboreshwa ya mpira na michezo kiujumla. (its better in every perspective).
(Kama hujaanza mshukuru Mungu na akulinde usiingie huko, ukiingia huko utajuta, kwani huwezi kuacha!), YOU WILL BE ENSLAVED!
Baada ya miaka mitano,65% ya vijana watakuwa wakijishughulisha na 'kusuka mikeka' badala ya kufanya shughuli za uzalishaji bidhaa na huduma. Consequently uchumi wa mataifa (hasa vichwa vya panzi kama 'wadanganyika', stupid kabisa!) utayumba kutokana na watu kutofanya kazi, lakini uchumi wa mataifa yanayomiliki hizi betting systems (hasa wazungu) utapaa kama mbayuwayu.
YOU'VE BEEN WARNED!
DON FRANCIS
==================================
18/05/2018
Update: News Alert: - Wazee Arosto la kubeti halina tofauti na kuvuta unga (cocaine)
Kamari ni mbadala madawa ya kulevyaMsipotoshe watu kwa maneno yenu hayo. Hivi betting na cocaine ni wapi na wapi jamani?
Hizo ni sayari mbili tofauti. Issue ya msingi ni kujua kuwa kila tabia ikizoeleka huwa addictive kwa namna moja ama nyingine.
Sio betting tu ambayo ni addictive. Kila kitu ukikizoea, mimi naweza nisilale hata siku tatu nikiwa naangalia mechi tu hata recorded. Kuna mdogo wangu alikua anakesha anacheza pool kila siku.
Kuna watu wanapiga pull kila siku hata kama wameoa au wana wapenzi. Ulevi wa pombe, sigara, umalaya (kwa wanaume na wanawake) zote hizi ni addictions.
Kuna mtu mwingine bila kunywa gahawa kila siku jioni basi halali. Hivyo tusipotoshane kuhusu haya mambo.
Betting ni kitu cha kawaida ila cha muhimu ni kuzingatia tu kanuni mbili kuu.
1. Do not stake what you can't afford to lose. (Usiweke pesa ambayo unajua hutaki kuipoteza au haumudu kuipoteza)
Maana yake, ukite unasoma chuo labda umepewa ada na mzazi million ukaacha kwenda kulipa ada ukaenda kubet. Hapo una stake pesa ambayo haupo tayari kuipoteza na mwishowe utalia.
Bet pesa ambayo hata ikiliwa unakuwa upo mikono salama. Ndio tafsiri yake hii
2. Do not bet your life away. Maana yake usiwe desparate sana kisa umeona fulani anashinda kila siku, wewe ukapoteza ukaanza kuchukua hela zako za akiba kwa matumaini ya kushinda matokeo yake unajikuta umebakia na boxer tu.
Nyongeza: KAMA HAUNA HELA HATA SIKU MOJA HUWEZI KUSHINDA HELA. UKIBET VIMIKEKA VYA JERO SIJUI BUKU HUTAKAA USHINDE PESA NI ZALI SANA MARA MOJA KWA MWAKA ANATOKEA MMOJA.
UKITAKA KULA PESA KUNA NA PESA ANGALAU KUAMZIA LAKI 2 MPAKA MILLIONS ALAFU UTAFURAHIA BETTING
Hata viroba vilikuwa vinalipiwa kodi ila tukaviondoa, tusiogope kurekebisha makosaKamari wanalipa kodi katika nchi ya viwonder. Je dawa za kulevya zinalipa kodi?
Poa mkuu ngoja tuendelee sisi kupiga pesa bila kulewaKamari ni mbadala madawa ya kulevya
Wanaokuwa na alosto ni wengi na wanaongezeka kila kukichaPoa mkuu ngoja tuendelee sisi kupiga pesa bila kulewa
Wachangiaji wachache lakini wasomaji ni wengi, hahah, wanaona aibu hata kuchangia.., aibu imewajaa...!Thread nzuri wachangiaji wachache
Huyu BAHATI NASEEB atakuwa ndo alianzisha kamari Tanzania???