Biashara ya Kamari: Mbadala wa Dawa za Kulevya?

News Alert: - Wazee Arosto la kubeti halina tofauti na kuvuta unga (cocaine)

Wakuu,
Nimeona nisikae kimya kwenye hill kwani limenifikirisha kwa muda mrefu....wazee kubeti hakuna tofauti na kubwia unga!!

Vijana wengi (siku hizi hata wazee) hasa wa maeneo ya mjini wamejiingiza katika mchezo huu wa kubeti (michezo ya kubashiri )
Wakiwa na matumaini ya kupata fedha nyingi na za haraka jambo linalowapelekea kuwa na msongo mkubwa wa mawazo pale wanaposhindwa (kuchana mikeka) ..

Watu hawa wanapokosa Pesa ya kubeti huhisi kuumwa ama kwa hakika siku yao haiwezi kukamilika pasipo kubeti (kuweka mkeka) binafsi Nina mdogo wangu wa kiume nadhani huyu ni zaidi ya teja kwenye kubeti kila akiniomba Pesa basi ni ya kubeti yupo radhi ashinde na njaa.....So sad!!

Huko mtaani ndio usiseme vijana wapo camp hawajishughulishi zaidi ya kubeti kutwa nzima kuhangaika na makaratasi makuukuu Loh!.......unakuta kijana yupo radhi aibe ama apige fix (miziinga) ili tu spate buku LA kubetia na anapoliwa ile buku hugeuka kuwa kama kichaa aliyedata kwa stress...siku wakibahatisha kula vihela basi hata bar hakukaliki kila mtu atajua kuwa mkeka umetiki...

Wadau, kama hujaanza au huujui huu mchezo bora ukae hivyohivyo kwani sio mzuri kwa afya yako (kiuchumi...stay safe don't try this.....arosto LA kukosa hela ya kubeti ni sawa na lile la teja kukosa chenji za kete.

Wahaadhah assalaam aleykum!!!!
 
Kamari wanalipa kodi katika nchi ya viwonder. Je dawa za kulevya zinalipa kodi?
 
Nakubaliana na wewe michezo ya Bahati na Nasibu na Kamali, hutengeneza tajiri mmoja na maskini wengi.

Nchi tajiri ni matajiri walio na pesa ya ziada ndio hushiriki, lakini hata huko hatimaye Kamali hula mitaji yao na kufilisika.
 
Msipotoshe watu kwa maneno yenu hayo. Hivi betting na cocaine ni wapi na wapi jamani?

Hizo ni sayari mbili tofauti. Issue ya msingi ni kujua kuwa kila tabia ikizoeleka huwa addictive kwa namna moja ama nyingine.

Sio betting tu ambayo ni addictive. Kila kitu ukikizoea, mimi naweza nisilale hata siku tatu nikiwa naangalia mechi tu hata recorded. Kuna mdogo wangu alikua anakesha anacheza pool kila siku.

Kuna watu wanapiga pull kila siku hata kama wameoa au wana wapenzi. Ulevi wa pombe, sigara, umalaya (kwa wanaume na wanawake) zote hizi ni addictions.

Kuna mtu mwingine bila kunywa gahawa kila siku jioni basi halali. Hivyo tusipotoshane kuhusu haya mambo.

Betting ni kitu cha kawaida ila cha muhimu ni kuzingatia tu kanuni mbili kuu.

1. Do not stake what you can't afford to lose. (Usiweke pesa ambayo unajua hutaki kuipoteza au haumudu kuipoteza)

Maana yake, ukite unasoma chuo labda umepewa ada na mzazi million ukaacha kwenda kulipa ada ukaenda kubet. Hapo una stake pesa ambayo haupo tayari kuipoteza na mwishowe utalia.

Bet pesa ambayo hata ikiliwa unakuwa upo mikono salama. Ndio tafsiri yake hii

2. Do not bet your life away. Maana yake usiwe desparate sana kisa umeona fulani anashinda kila siku, wewe ukapoteza ukaanza kuchukua hela zako za akiba kwa matumaini ya kushinda matokeo yake unajikuta umebakia na boxer tu.

Nyongeza: KAMA HAUNA HELA HATA SIKU MOJA HUWEZI KUSHINDA HELA. UKIBET VIMIKEKA VYA JERO SIJUI BUKU HUTAKAA USHINDE PESA NI ZALI SANA MARA MOJA KWA MWAKA ANATOKEA MMOJA.

UKITAKA KULA PESA KUNA NA PESA ANGALAU KUAMZIA LAKI 2 MPAKA MILLIONS ALAFU UTAFURAHIA BETTING
 
Kamari ni mbadala madawa ya kulevya
 
MBEYA: Mwanafunzi wa Chuo ajinyonga kufuatia matokeo ya mpira Kombe la UEFA

Kijana wa Chuo cha S. Agustine Mbeya amekutwa akiwa amejinyonga kwa kile ambacho tetesi zinazotaja ni kwa sababu ya matokeo ya mpira katika mtanange wa Kombe la UEFA, baina ya Real Madrid na Liverpool.

Pichani ni baadhi ya majirani wa Kijana huyo pamoja na uongozi wa Serikali za mtaa wa maendeleo uliopo jijini Mbeya wakiambatana na Jeshi la Polisi muda huu kuupeleka mwili huo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Habari kamili kuhusiana na tukio hilo, zitafuata baada ya ripoti rasmi.

======

Mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo cha Saint Agustine Mbeya, Moses Mashaka amejinyonga kwa mujibu wa mashuhuda wa eneo analoishi wamesema Mwanafunzi huyo alikuwa shabiki Klabu ya Liverpool na inadaiwa kuwa kitendo cha kufungwa kwa Klabu hiyo goli 3-1 ndio sababu.

Hata hivyo wengine wamesema Mwanafunzi huyo alijiingiza katika mchezo wa Kamari maarufu kama Betting na kitendo cha kuliwa inawezekana ikawa sababu

Akithibitisha kutokea kifo hicho Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya Mussa Taibu amesema ni kweli amejinyonga kwa kutumia kanga chumbani kwake na aliyegundua kuwa kujinyonga ni Baba mwenye nyumba.
 
Thread nzuri wachangiaji wachache


Huyu BAHATI NASEEB atakuwa ndo alianzisha kamari Tanzania???
 
Kwa utafiti uliofanyika mpaka sasa, ukikopa pesa bank na kucheza hizo kamali ushindi uko nje nje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…