Biashara ya Kuonesha Mpira wa Miguu (Kibanda-umiza): Fahamu Kiasi cha Mtaji, Vifaa na Mbinu za Uendeshaji

Biashara ya Kuonesha Mpira wa Miguu (Kibanda-umiza): Fahamu Kiasi cha Mtaji, Vifaa na Mbinu za Uendeshaji

Kuhusu biashara hiyo kiukweli inalipa sana,ushauri wangu,nunua decorder za Q-sat,hizi sanasana kwa tanzania unaweza kuzipata zanzibar,au pia huku nilipo U.A.E zinapatikans na ndio zinazotumika 95%
Ukiwa na dish la FTA utaweza kupata channel zaidi ya mia tatu,na pia utaona ligi zote kubwa duniani ikiwemo EPL.
hapa utazipata kupitia bein sport,,changamoto kubwa ni kwenye matangazo ya mpira utayapata kwa lugha ya kiarabu.

Gharama zake kununua decorder ni USD 65. Registration online ni usd 50 kwa mwaka..hii ina maana kila mwaka utalipia usd 50tu.
Hapa hakuna longolongo na signal zao ni HD.
Ukiwa interested na hili nicheki whatsapp no +97455783566 kwa maelezo zaidi na pia narudi tz by 10 may..
 
Njoo TZ kwanza tuonane live.. sasa zinazotangaza kwa kingereza inakuje.. zinapatkanaje
 
Mimi pia ni mfanya biashara wa viewing centre huku Mombasa, Kenya. Niliamua kuchukua beIN kwa sababu DSTV imepata competition kutoka kwa Kwese. Kwese ndiyo inayo onyesha EFL. Na ingawa unaweza kuangalia Kwese kwa Muda wa siku 3 for just $4, niliona ni usumbufu! Besides, natumia decoder ya beIN PVR ambayo hurekodi movies halafu natumia kuonyesha watu. Watu huja kutazama ligue 1, serie A na Bundesliga pia - kitu ambacho DSTV hawana
Vp decoda ya beIN naweza ipata wap? Vp malipo yake yakoje nipo Tz
 
Nahitaji mwongozo kwa anayefahamu hii biashara. Nampango wa kufungua banda la mpira Tabora ila uhalisia wa vitu muhimu kwenye hii biashara ndo sifahamu kama gharama za kufungua banda,faida na hasara zake.Ahsanteni
 
Ķwanza uwe na dstv nakushauri.
Tv nzuri.
Mazingira ya uswahilini yanalipa zaidi
 
Angalia mzunguko wa watu?.Je utatumoa viti vya plastic au ma bench?.then tv nzuri au hata projector na dstv.
Kumbuka thamani unayowekeza linganisha na bei utayowachaji raia wa eneo lako ukizingatia hali za kiuchumi za hapo
 
Angalia mzunguko wa watu?.Je utatumoa viti vya plastic au ma bench?.then tv nzuri au hata projector na dstv.
Kumbuka thamani unayowekeza linganisha na bei utayowachaji raia wa eneo lako ukizingatia hali za kiuchumi za hapo
asante ndugu
 
Ni biashara inayolipa sana na sana ila make sure unasimamia wewe mwenyewe na si kumpa rafiki au ndugu. Unatakiwa uwe na vyote Azam for VPL na DSTV na Projector ili iwe rahisi kwa watazamaji kuona + viti vya mbao au mabenchi then umemaliza
 
Ndio. Karibu
1. A 2 z Soccer Hall .Tupo Kibaha mkabara na kanisa la TAG
2. Vijana Stadium . Tupo Tandale kwa tumbo.

Huduma zetu ni nzuri sana. Kumbi za kisasa zenye kila kitu cha kisasa. Usalama wa uhakika muda wote. Sreen Tv ziko zaidi ta tatu na zimefungwa mahara sahihi kila mtu kuona. Huduma zote zipo: Vocha na vinywaji baridi. Hatutaki ushabiki wa kishamba, wa ulimbukeni na hatutaki vurugu!.

Karibuni wote. Njoo na marafiki zako; njoo na familia yako; njoo na mpenzi wako kumbi zote zetu ni mahara salama pa kupumzikia; kupunguzia stress na kuburudika ki soccer!
mkuu wewe unatumia tv za inch ngapi? na kwa nini hautumii projectors
 
Nimekereka na vitu vikubwa viwili:-
1. Kutojua tofauti ya 'R' na 'L' kumenifanya nishindwe kumalizia kusoma mpaka mwisho.
2. "Kuuza vocha hasa za Halotel maana ndio zina wateja wengi" huyu mtu sijui anakaa wapi/mkoa gani?

PONGEZI
Mtoa mada anaonekana hajapita shule kubwa lakini ukimfutilia utaona anajua kupambana sana na maisha,hata wanaotoka vyuoni na degree zao anaweza kuwaacha mbali kwa ubunifu/udhubutu.
umemkosoa mwenzako juu ya kushindwa kiuandishi, hususani katika kukosea baadhi ya herufi, lakini na wewe umekosea vibaya sana, ni udhubutu au uthubutu (assertively)?
 
Back
Top Bottom