Biashara ya Kuonesha Mpira wa Miguu (Kibanda-umiza): Fahamu Kiasi cha Mtaji, Vifaa na Mbinu za Uendeshaji

Biashara ya Kuonesha Mpira wa Miguu (Kibanda-umiza): Fahamu Kiasi cha Mtaji, Vifaa na Mbinu za Uendeshaji

Habari. Kuna ndugu yangu kaniomba nimfungulie banda la kuonyeshea mpira. sehemu ipo shida sijajua vipengele Muhimu vya kufata. mfano tv ziwe size ngapi na aina gani na kutokana na kukatikakati kwa umeme ninatakiwa kununua generator la ukubwa gani na mwenye kujua price anaweza akanisaidia ili niweze kutengeneza budget. Naomba mnisaidie najua huku jamii forum ni kisiwa cha wajuzi wa vitu mbali mbali. TV Ziwe za mtumba au new?
 
Generator kuanzia kv4
Mabenchi + viti
Tv kuanzia laki 9 used nchi 50
Banda
Birika la tangawizi
Friji la soda za pepsi
Karanga
Taa za nyuma na mbele
Feni za ukutani 2
Vinga'muzi 3 Azam ,Dstv, na startimes
Cables

Gharama ni milioni...??
 
Habari. Kuna ndugu yangu kaniomba nimfungulie banda la kuonyeshea mpira. sehemu ipo shida sijajua vipengele Muhimu vya kufata. mfano tv ziwe size ngapi na aina gani na kutokana na kukatikakati kwa umeme ninatakiwa kununua generator la ukubwa gani na mwenye kujua price anaweza akanisaidia ili niweze kutengeneza budget. Naomba mnisaidie najua huku jamii forum ni kisiwa cha wajuzi wa vitu mbali mbali. TV Ziwe za mtumba au new?
Take it from me
Mimi ndo biashara ninayoifanya maeneo ya Chanika nina flatscreen 2 za mtumba inch 43 bei 1*600,000/= nina banda kubwa mabenchi nina Generator kingMax 5500 dx ving'amuzi ninavyo saba dstv 3 azam 2 startmes 2
 
asante
Generator ya ukubwa huo ni bei gani?
 
Mkuu Mimi hii ni moja wapo ya biashara zangu
Ingawa kwa sasa natumia dish mbili tu

Dstv natumia extra view malipo laki moja na nusu
Na kingine hizi za ndani decoder ya Azam

TV ninazo flat mbili na projector moja
Na jenerator plus sabufa mbili basi

Bei star x mbili nilinunua laki Tisa kila moja 450000
Sabyfa mbili

Moja 200000
Nyingine 90000
Ving'amuzi Azam 145000+ ufundi 30000+malipo ya mwezi 15000

Dstv nilinunua 80000 + ufundi 30000
Kifurushi 150000 kwa mwezi

Ila kabla ya Dstv nilikuwa natumia receiver ya alphabox hii nilinunua 250000 pamoja na Vifaa + ufundi
Dish 200000
Basi
Na banda laki saba tu kulijenga

ILa usiogope anza na ulivyo navyo
Asante ndg yngu kw mchanganuo mzr hata Mm nmetoka na kitu japo cjauliza swali
 
Heshima kwa wote,

Naomamba kujua mawazo ya wajuvi wa biashara kwenye jambo la namna hii;

Nilipanga kufungua banda la kuonyesha mpira katika eneo langu fulani center fulani. Lakini wakati nasubiri msimu uanze katokea jamaa kanunua kiwanja cha pili kutoka hapo kwangu na sasa anajenga naye anapanga kuweka banda la mpira.

Kwa upande wangu kuna nyumba nilishajenga siku nyingi ndio nilikuwa nataka kuitumia kwa shughuri za kuonyesha mpira maana ina vyumba vikubwa tu kwa mbele vinafaa kwa shughuli hiyo.

Swali langu ni je nifanyeje baada ya hali hiyo kujitokeza?

Je niendelee na mpango wangu tushindanie wateja au nibadili mawazo nitafute biashara nyingine ya kufanya?

Natanguliza shukurani kwa mawazo yenu mtakayotoa.
 
Kwamba uachane nao kwa kuhofia utaonekana umeiga au?

Endelea tu Mkuu na huo mpango muhimu kama hiyo sehemu umeiona potential kibiashara
 
Kwamba uachane nao kwa kuhofia utaonekana umeiga au?

Endelea tu Mkuu na huo mpango muhimu kama hiyo sehemu umeiona potential kibiashara
Asante kwa ushauri wako mkuu. Bado napokea maoni, kweli la kwanza ni kuona kama nimeiga la pili naona kama anayekuja ana nguvu kubwa ya kiuchumi kunishinda la tatu ni kuhusu kuwa na wateja wachache.

Sijui unayaonaje hayo mkuu
 
Kama kuna uwezekano wa kutoka hapo na kwenda sehemu nyingine ambapo hakuna business kama hiyo basi itakuwa vizuri sababu utakuwa peke yako na ukizingatia utakuwa na uhakika wa domination hata akija mwingine baadae.

Lakini kama hakuna uwezekano wa kutoka hapo basi itabidi uwe mbunifu zaidi, kuboresha na kupendezesha ili kuvutia wateja sababu ushindani wa kibiashara kati yenu utakuwa mkubwa. Na hiyo challenge ndio point nzima ya business.

Ila ngoja nikupe hint moja ni kwamba kila aina ya ubunifu utakaoufanya au kuongeza chochote na kuboresha chochote kwenye business ni lazima wewe uwe wa kwanza.
 
Kwamba uachane nao kwa kuhofia utaonekana umeiga au?

Endelea tu Mkuu na huo mpango muhimu kama hiyo sehemu umeiona potential kibiashara
Well mkuu kwenye ulimwengu wa biashara hakuna kitu kinachoitwa kuiga bali kuna ushindani wa kibiashara hiyo ndio challenge kuu kwenye kufanya business moja karibu au sehemu moja. Sababu probability of income assurance reduces.

Siku zote kufanya kitu kimoja sehemu moja kunapunguza uwezekano wa wewe kupata faida na ili kupambana na hilo litahitaji pesa, nguvu na ubunifu zaidi. na kujenga wateja wa kudumu, loyal customers kitu ambacho kitachukua muda kidogo.
 
Nashukuru kwa maoni yenu, ila kwenda kufanya sehemu nyingine ni wazo zuri isipokuwa litanigharimu zaidi na itachukua muda kidogo kulitimiza.

Ngoja niendelee kuchanganua ili nikitoa maamuzi niyasimamie kwa nguvu zote.

Naendelea kupokea maoni ili niweze kuwa well informed nitakapotoa maamuzi.
 
Back
Top Bottom