Biashara ya mashine ya kusaga na kukoboa nafaka- Fahamu bei zake, uendeshaji wa biashara hii pamoja na faida na hasara zake

Biashara ya mashine ya kusaga na kukoboa nafaka- Fahamu bei zake, uendeshaji wa biashara hii pamoja na faida na hasara zake

asant sana mwanaifm, nimekuta sana kaka.kama inawezekana naomba conduct no ili siku moja nikutembelee huko dom.
 
Baba JJ Gharama za Mashine inategemea unanunua wapi. Kimsingi ziko kutoka china na nyingine zinatengenezwa na local vendors mbali mbali ingawa kwa ubora tofauti. Tatizo kubwa la Mashine za mitaani ni kushindwa kupunguza mtetemeko wa Mashine (mitigating vibration level) na wengine wanatengeneza kwa bati nyepesi sana (2mm thick) kwa kinu cha kusaga na 0.8 t0 1.2mm kwa kinu cha kukoboa. Matokea yake vinaharibika mapema sana. Nakushauri kanunua katika karakana ya SIDO Moshi. wanatengeneza vinu imara sana kwa kutumia plate ya 6mm thick. Bei zake kwa mwaka jana ilikuwa kama ifuatavyo;
- Kinu cha kusaga 75 Tshs. 3,500,000
- Kinu cha kukoboa Roller 3 Tshs. 3,200,000
Vinu hivyo unapewa na Mota ya 25 Horse power, starter pamoja fremu.
Kama unataka Mota tu zinauzwa morogoro road kwa Dsm. ni za kutoka china lakini ni nzuri tu. Ukitaka Mota ya kutoka UK ya Horse power 25 ni ghali sana. Not less that 2.5M+
Gharama zingine ni pamoja na Mashine ya kushonea viroba na weigh machine (preferably digital). Utapata morogoro road pia
 
Tunaomba feedback!

Tatizo la JF ni mtu kuanzisha mada ya kuomba msaada halafu baadaye hata hasemi kama alifanikiwa, alikutana na changamoto, au hakuanza kabisa.

Hii tunaiona sana na ikiendelea hivi basi kunakuwa hamna faida ya kupeana ushauri. Wengine tunahamasika pale tunapoona wenzetu wamefanikiwa. Lakini hata pale ambapo mafanikio hayajapatikana, bado kuna kitu cha kujifunza.
 
Tunaomba feedback!

Tatizo la JF ni mtu kuanzisha mada ya kuomba msaada halafu baadaye hata hasemi kama alifanikiwa, alikutana na changamoto, au hakuanza kabisa.

Hii tunaiona sana na ikiendelea hivi basi kunakuwa hamna faida ya kupeana ushauri. Wengine tunahamasika pale tunapoona wenzetu wamefanikiwa. Lakini hata pale ambapo mafanikio hayajapatikana, bado kuna kitu cha kujifunza.
Point point walete mrejesho
 
Wakuu naomba tushauriane na kupeana uzoefu juu ya hii biashara. Binafsi kwa mda mrefu sasa nimekua najipanga kufanya hii biashara..kuanzia kufunga mashine hadi kufanya packaging. Tayari nimeshanunua eneo pembeni kidogo ya mji kwa ajili ya hii kitu japo nimeweka na mifugo pia. Naomba mwenye ujuzi na aina za mashine za kukoboa mpunga na za kusaga mahindi atupe uzoefu.
 
Habari za jioni wakuu

Ninaombeni mawazo yenu. Niko kwenye mchakato wa kuanzisha kiwanda rasmi cha kusaga na kufungangasha unga wa nafaka mbalimbali. Nina mashine ya kusaga mahindi mkoani Dodoma na nilikua nafunga na kuuza unga kienyeji vijijini. Sasa nimeamua kuifanya iwe rasmi kabisa na Mungu akisaidia January 2016 bidhaa zangu zitakua sokoni. Niliyofanya mpaka sasa?
1. Mashine ya kukoboa na kusaga
Tayari ninayo na inatoa huduma

2. Mashine ya kupima, kufungasha na kufunga niliagiza kutoka China na iko kwenye hatua za mwisho za kuwa installed

3.Nimeshaanza mchakato wa kupata vifungashio kwenye kiwanda kimoja Bagamoyo. Mifuko ya kilo 5, 10 na 25 yenye nembo.

4.Stock ya mahindi ninayo karibia tani 10

5.Niko kwenye hatua za mwisho za kupata kibali cha tbs.

Kwa wazoefu wa biashara hii naomba kama kuna mwenye mchango wa ziada tushauriane mpaka hapo nilipofikia. Na kama kuna kitu kingine chochote kinahitajika.Tunaweza wasiliana hapa kwa michango au anymore business ideas/patnership na masoko zaidi.Au hata kwa PM

Shukran.
Mjasiriamali
Heshima yako boss...naomba kujua ulifikia wapi na hii biashara...
 
Mashine za kukobla nunua za roller tano..
Kusaga chongesha mwenyewe tumia plate za nchi 11 upana wa mashine ni wewe tu ila Mimi ni mapanga kumi na kupanda.
Motor ya kukoboa HP 30 itafaa
Motor kusaga HP 50 ila ukichonga mashine kubwa.
Kuhusu soko kipind cha mavuno utatafuta solo na sometimes mkopo utahusika.
Kipind kama hili soko uhakika ila mahind ya kusumbua.
Kuhusu mashine na installation na starter na vvibali na usajiri wa kampun jiandae na m10. Operating capital n wewe
 
Bei hizo ziko juu sana lakini haswa tumia za Sido kwa vinu mota ndo uingoe Dukani
Hivi kinu katika mashine ni kipi,na vipi hizi za kichina zina tatizo gani maana nasikia zinatoa unga vizuri sana.
 
Wadau, nataka kuwekeza katka biashara ya mashine ya kusaga na kukoboa. Naomba ushauri wenu kwa wenye uzoefu na biashara hii.
 
Hongera sana, Kuna mtu ameshauri hapo kuhusu kuwa na mtu wa Marketing. Napenda pia kushauri kuwa na watu wa marketing kwa kila mkoa kwa kuanzia angalau DSM, PWANI, sijajua kwa huko mikoani.. Ambao kila kwanza utawapa jukumu la kutengeneza Market Plan iliyoshiba kwa kuelezea na vitendo kuanza haraka juu ya vyanzo vya masoko. Kwa DSM waanze negotiations na shule ya Private, Cafterias za vyuoni mf. DUCE, UDSM, ARDHI, IFM, CBE, DIT, ST JOSEPH, TIA, ST MARK'S, MNMU nk.. Pia kufungua ofisi mbalimbali kwa kila maeneo yenye hizo nafaka. mf. Mbagala, Tabata, Buguruni, Gongolamboto, Temeke, Kigamboni, Mbezi, Kimara, Mwenge, Makumbusho, Magomeni, n.k. Promotion katika vyombo vya habari, kutafuta airtime za mahojiano na TV's au Redio.. Lakini mwisho wa siku kumbuka kutembelea VITUO VYA WATOTO YATIMA angalau kuwapa hizo nafaka. Kumbuka pia promotion nyakati za sikukuu. ALL THE BEST.

MUNGU akubariki kwa ushauri mzuri.
 
Habari za asubuhi wanajamvi,

Nina wazo la kuanzisha biashara ya kukoboa na kusaga nafaka lakini bado sina utaalamu nayo kwa maana ya kujua gharama za mashine ya kusaga na kukoboa zenye ubora utakaokidhi ushindani na gharama za installation na taratibu gani hufuatwa ili kuihalalisha hii biashara maana nataka pia kuwa nafunga unga katika mifuko na kuuza.

Mwenye ujuzi wa hii kitu please naomba unipe mwanga maana najua humu kuna wataalamu na wajuzi wakila namna.

Ahsanteni
 
Duuh uzi huu umekosa wachangiaji maana hata mimi nilikuwa nangoja mchango wa wajuzi kuhusu utaratibu wa kuhararisha ufungaji na usambazaji wa sembe jee TFDA wanahitajika au ni TRA na Halmashauri ya Manispaa/ Mji/Wilaya want to share?
 
Gharama za mashine zote pamoja na ufundi si chini ya 12m
 
Utaratibu wa usajili ni kama wa kawaida tu unapofungua kampuni ila TFDA, TRA na Manispaa lazma wahusike
 
Kwa yeyote mwenye uzoefu wa kutosha katika biashara hii tafadhali naomba ushauri. Nataka kuaingia katika biashara hii. Nipo hapa mjini dar es salaam.
Mchango wako ni wathamani Sana kwangu....
0716548250
 
Kwa mtazamo wangu naona ni biashara nzuri sana endapo utakuwa unachukua nafaka shamba unasaga Alafu unauza unga kwenye viroba!
 
Kwa mtazamo wangu naona ni biashara nzuri sana endapo utakuwa unachukua nafaka shamba unasaga Alafu unauza unga kwenye viroba!
Asante ndama kwa mchango wako na kunitia moyo
 
Habari ndugu zangu sina utaalamu sana Katika sekita hii kama umewahi kufanya au ni mtaaluma wa mashine hizi niambie kimsingi naitaji kuanzisha machine ya kusaga mahindi.. Na kukoboa.
Tafadhali kama ni mtaaluma wa haya niambie chochote.
Na kiwango kidogo cha mtaji na kikubwa.
 
Back
Top Bottom