Biashara ya Mbao na Miti: Fahamu Uendeshaji, Faida na Changamoto zake

Ndugu, nitakusaidia kukutafutia miti. Ukishapewa ABC na wataalamu ni PM nikufanikishie.
 
JamiiForums katika ubora wake! Katika biashara au uwekezaji wa muda mrefu huu unalipa! nimeona hadi hapa mafinga Wakenya wananunua ardh na kupanda miti Wabongo 2melala 2.
 
Naombeni ufafanuzi kuhusu kodi inayotakiwa kulipwa TRA. Nijuavyo kama ni misitu ya asili kila cubic meter unalipia kama 205,000. Je bado kuna kodi nyingine y a kulipa TRA?
 
KVM vp mrejesho wa hii kitu. Tushirikishe maendeleo yake kaka, wengine ndo tunataka kuanze

Samahani bwana nilikuwa nimesafiri kidogo.

Lakini maendeleo ni mazuri kutosha. Kumbuka tu kwamba mimi nilianza kitambo kidogo na miti yangu mingine naweza
kuipasua muda wowote ule. Nataka kuanza upasuaji rasmi ndani ya miaka miwili ijayo.

Hata hivyo miti ipo kwenye stage mbalimbali kama picha hapo chini zinavyoonyesha.

Kitu cha kufarijika ni kuwa kumekuwepo na muamko mkubwa sana wa upandaji miti. Sasa hivi ukitoka Njombe mjini kuelekea Songea ni takribani kilomita zaidi ya mia moja unachoona ni mashamba ya miti tu kulia na kushoto.










 
Nani anaweza kuandika business plan nzuri kwa ajili ya biashara hii ya miti ili tuweze kumiliki shamba kubwa na kuweza kuvutia wawekezaji?

Kuliko small scale farming ambao wengi wetu tunaifanya

Nawasilisha
 
nani anaweza kuandika business plan nzuri kwa ajili ya biashara hii ya miti ili tuweze kumiliki shamba kubwa na kuweza kuvutia wawekezaji?

Kuliko small scale farming ambao wengi wetu tunaifanya

nawasilisha

Nadhani business plans nzuri za miradi ya kilimo zinaweza kutengenezwa na watu waliomaliza SUA (Agricultural Economics).

Hata hivyo mimi napenda kuwahamasisha zaidi wapandaji wadogo wadogo hasa wa kule vijijini. Wengi wao wana uwezo wa kupanda ekari chache (ekari mbi, tano hadi kumi) lakini impact yake kwenye kijiji walimo inakuwa kubwa sana sana hasa kama kila mwanakijiji atapanda hiyo miti. Hicho ndicho unachokiona kwenye barabara za kutoka Njombe kwenda Songea, Njombe kwenda Makete, na Njombe kwenda Lupembe.
 

Hongera sana mkuu!!,muda si mrefu utakuwa bonge la millionea.
 
Jamii forums katika ubora wake! Katika biashara au uwekezaji wa muda mrefu huu unalipa! nimeona hadi hapa mafinga wakenye wananunua ardh na kupanda miti wabongo 2melala 2,

Mkuu sisi wabongo tumelala kisawasawa!!,ngoja Wakenya watuzidi.
 

Kweli mkuu!,upo Njombe mkuu?
 

Naungana na KVM, wawekezaji wakubwa kwenye misitu wanatosha walioko Mufindi/Kilolo na kwingineko. Ningekuwa na uwezo ningeandika bango pale mwanzoni mwa mkoa wa Njombe ukitoka Iringa, lingesomeka hivi " WAWEKEZAJI KWENYE MISITU TOKA NJE YA TANZANIA WASIJE MKOA WA NJOMBE,MBEYA,RUVUMA NA RUKWA" yaani waishie huko huko kwa wenzetu, hivi hata kazi ya kuotesha miti tunahitaji wawekezaji? watalaam tunao,mbegu tunazo,mvua tunayo,ardhi tunayo, manpower tunayo, soko la ndani tunalo.

Ukitaka kuona impact ya small scale ya misitu ktk jamii nenda Makete, wilaya nzima wananchi waliotesha miti zamani, unakuta kibabu kina vimilioni kadhaa ndani, nyumba nzuri na sasa umeme unasogezwa, mambo yatakuwa vizuri.

Nadhani sisi kama Watz kwa sasa, tuanze kujadiliana namna bora ya kusindika mazao ya misitu hii ili tuongeze thamani. Juzi nimekutana na Wachina kule Mapanda Mufindi wanatafuta miti ya kununua kwa ajili ya fenicha Dodoma, nikahuzunika sana, ila tutafika siku moja.
 
Reactions: KVM
Wewe upo kijiji gani mkuu?

 
Nipo Wino - Mpakani mwa Ruvuma na Njombe upande wa Ruvuma
 

KVM,

Hapo pekundu imebidi na mimi nifanye kwangu.
 
Habarini watu wa Mungu, mimi ninavutiwa kufanya biashara ya kuuza mbao Nairobi, mtaji kwangu suo tatizo sana, msaada ninaohitaji kwenu ni process za kupata kibali, kama kuna mtu anafaham utaratibu mzima wa kibali au taratibu nyingine zinazohusiana anisaidie tafadhali.

Asanteni sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…