Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sumbawanga mashamba unapata kwa bei gani kwa heka, na je aina gani ya miti inalimwa maeneo hayo.Wazo zuri. Nilipita maeneo ya Sumbawanga hasa Wilaya ya Kalambo,nako kuna mashamba haya japo kwa uchache! Issue kubwa hapa uwe na eneo. Huwezi kukodi kwa vile ni zao la kudumu na la muda mrefu.
Niliona mikaratusi mingi,imestawi sana. Kuhusu bei, sikufanya utafiti wa kutosha llabda niwasiliane na wadau wa huko nikujuze.Sumbawanga mashamba unapata kwa bei gani kwa heka , na je aina gani ya miti inalimwa maeneo hayo
Mkuu tupo pamoja mimi pia nimekuwa nikipanda kila mwaka na January hii naenda kupanda tena huko Mufindi,wanaJF wahamasike ni uwekezaji muhimu wenye manufaa makubwa sana unawekeza mtaji mdogo kwa gharama ndogo unavuna kwa faida kubwaMimi nigependa kuwahamasisha wanJF kupanda miti ya mbao hasa mbao nyeupe (pines and cypress). Miti hii inasitawi sana sehemu za nyanda za juu kusini.
Mimi nilianza kupanda miti hii kama miaka kumi iliyopita. Nimepanda miti mingi kila mwaka bila kukosa. Kwa sasa ninazo ekari nyingi za miti hii. Vile vile miaka ya karibuni nimepanda eucalyptus.
Wakati naanza kupanda miti mche mmoja nilikuwa nanunua kwa Shs 50 na kuupanda kwa Shs 20. Kwa vile napanda miti mingi (zaidi ya laki moja kwa mwaka) baadaye niliamua kuotesha miche mimi mwenyewe ili kupunguza gharama.
Gharama zaidi ya miche na upandaji ni barabara za moto kuzunguka msitu. Hata hivyo nilinunua ngómbe na kuwaweka kwenye shamba ili wale majani yanayozunguka msitu. Wamenisaidia sana.
Unaweza kupanda miti kidogo kidogo kila mwaka kutumia mshahara wako kama nilivyofanya mimi. Baada ya miaka kadhaa utakuwa na miti mingi na utaweza kuwa unauza miti au kupasua mbao kila mwaka.
Am speechless. Haya ndo mambo ya kufanya. Tukikalia kulalamika tutakufa tukilalamika.KVM naona hii kazi uliinza muda mrefu kidogo, mimi binafsi naipenda sana hii biashara maana nilishawahi onja utamu wa pesa yake baada ya kuuza miti kidogo niliyopanda nikiwa sekondari. Nimefanikiwa kunua ekari 200 huko njombe najipanga kuanza kupanda January 2013 na 2014 ili mwaka 2022 niwe milionea sio kuanza kulalamikia mafao!
Hivi wakuu vipi miti kama mninga, ule mti wa kutengenezea vinyago, sijui ndo mpingo sina uhakika. Hii miti ni ghali sana. Je inaweza kupandwa katika shamba binafsi?Am speechless. Haya ndo mambo ya kufanya. Tukikalia kulalamika tutakufa tukilalamika.
Mie nataka kulima miti ya Mininga kwa ajiri ya mbao. Plz naombeni mwongozo. Je, miti hii itakua tayari kuvunwa baada ya muda gani?na jee ni mikoa gani inafaa kwa kilimo hiki?
Naweza kunichek nikuunganishie mashamba.Ninashukuru sana kwa hii topic, hata mimi nipo interested sana na kupanda miti na ni idea ya muda sasa, issue kwangu ni namna ya kuanza especially kupata shamba kwa ajili ya kupanda. Ningeomba kupata japo idea kama ninaweza kupata eneo huko njombe na kwingineko ukizingatia mimi ninaishi dar. Na price inakuwaje, pia gharama za miche kwa sasa ni kiasi gani na kuotesha plus kutunza. Please please mwenye data ninaomba
Mkuu asante kwa taarifa. Tukihitaji mashamba huko Njombe waweza kutusaidia kuyapata? Ekari moja ni shilingi ngapi? Liwe pori la kuanza kufyeka mwenyewe.Mimi nigependa kuwahamasisha wanJF kupanda miti ya mbao hasa mbao nyeupe (pines and cypress). Miti hii inasitawi sana sehemu za nyanda za juu kusini.
Mimi nilianza kupanda miti hii kama miaka kumi iliyopita. Nimepanda miti mingi kila mwaka bila kukosa. Kwa sasa ninazo ekari nyingi za miti hii. Vile vile miaka ya karibuni nimepanda eucalyptus.
Wakati naanza kupanda miti mche mmoja nilikuwa nanunua kwa Shs 50 na kuupanda kwa Shs 20. Kwa vile napanda miti mingi (zaidi ya laki moja kwa mwaka) baadaye niliamua kuotesha miche mimi mwenyewe ili kupunguza gharama.
Gharama zaidi ya miche na upandaji ni barabara za moto kuzunguka msitu. Hata hivyo nilinunua ngómbe na kuwaweka kwenye shamba ili wale majani yanayozunguka msitu. Wamenisaidia sana.
Unaweza kupanda miti kidogo kidogo kila mwaka kutumia mshahara wako kama nilivyofanya mimi. Baada ya miaka kadhaa utakuwa na miti mingi na utaweza kuwa unauza miti au kupasua mbao kila mwaka.
Mkuu asante kwa taarifa. Tukihitaji mashamba huko Njombe waweza kutusaidia kuyapata? Ekari moja ni shilingi ngapi? Liwe pori la kuanza kufyeka mwenyewe.