Biashara ya Mbao na Miti: Fahamu Uendeshaji, Faida na Changamoto zake

Biashara ya Mbao na Miti: Fahamu Uendeshaji, Faida na Changamoto zake

Hivi mti mmoja wa mbao ukikomaa na umetunzwa vizuri inaweza kutoa mbao ngapi ya 6x2 nikipata hesabu hiyo basi naweza kuingia kwenye shughuli ya upandaji miti.
 
Tunauza mashine za kukatia nyasi/miti /kupalilia nakuchimbia mashimo . Wasiliana nasi na tutakualetea moja kwa moja kutoka chini. Ni Pm au tembelea kurasa zetu Facebook & Instagram thebridgetz na @thebridgegulio
 
Wazo zuri. Nilipita maeneo ya Sumbawanga hasa Wilaya ya Kalambo,nako kuna mashamba haya japo kwa uchache! Issue kubwa hapa uwe na eneo. Huwezi kukodi kwa vile ni zao la kudumu na la muda mrefu.
Sumbawanga mashamba unapata kwa bei gani kwa heka, na je aina gani ya miti inalimwa maeneo hayo.
 
Sumbawanga mashamba unapata kwa bei gani kwa heka , na je aina gani ya miti inalimwa maeneo hayo
Niliona mikaratusi mingi,imestawi sana. Kuhusu bei, sikufanya utafiti wa kutosha llabda niwasiliane na wadau wa huko nikujuze.
 
Mimi nigependa kuwahamasisha wanJF kupanda miti ya mbao hasa mbao nyeupe (pines and cypress). Miti hii inasitawi sana sehemu za nyanda za juu kusini.

Mimi nilianza kupanda miti hii kama miaka kumi iliyopita. Nimepanda miti mingi kila mwaka bila kukosa. Kwa sasa ninazo ekari nyingi za miti hii. Vile vile miaka ya karibuni nimepanda eucalyptus.

Wakati naanza kupanda miti mche mmoja nilikuwa nanunua kwa Shs 50 na kuupanda kwa Shs 20. Kwa vile napanda miti mingi (zaidi ya laki moja kwa mwaka) baadaye niliamua kuotesha miche mimi mwenyewe ili kupunguza gharama.

Gharama zaidi ya miche na upandaji ni barabara za moto kuzunguka msitu. Hata hivyo nilinunua ngómbe na kuwaweka kwenye shamba ili wale majani yanayozunguka msitu. Wamenisaidia sana.

Unaweza kupanda miti kidogo kidogo kila mwaka kutumia mshahara wako kama nilivyofanya mimi. Baada ya miaka kadhaa utakuwa na miti mingi na utaweza kuwa unauza miti au kupasua mbao kila mwaka.
Mkuu tupo pamoja mimi pia nimekuwa nikipanda kila mwaka na January hii naenda kupanda tena huko Mufindi,wanaJF wahamasike ni uwekezaji muhimu wenye manufaa makubwa sana unawekeza mtaji mdogo kwa gharama ndogo unavuna kwa faida kubwa
 
KVM naona hii kazi uliinza muda mrefu kidogo, mimi binafsi naipenda sana hii biashara maana nilishawahi onja utamu wa pesa yake baada ya kuuza miti kidogo niliyopanda nikiwa sekondari. Nimefanikiwa kunua ekari 200 huko njombe najipanga kuanza kupanda January 2013 na 2014 ili mwaka 2022 niwe milionea sio kuanza kulalamikia mafao!
Am speechless. Haya ndo mambo ya kufanya. Tukikalia kulalamika tutakufa tukilalamika.
 
Am speechless. Haya ndo mambo ya kufanya. Tukikalia kulalamika tutakufa tukilalamika.
Hivi wakuu vipi miti kama mninga, ule mti wa kutengenezea vinyago, sijui ndo mpingo sina uhakika. Hii miti ni ghali sana. Je inaweza kupandwa katika shamba binafsi?

Inakomaa baada ya muda gani?
 
Nawashukuru wakuu wote humu ndani kwa michango yenu! Mm nilianza kupanda mwaka Jana kwa kupanda heka 2 tu. Mwaka huu mpaka this December nimefanikiwa kupanda heka sita za pines maeneo ya mbozi. Nimepanga kudunduliza kwenye mshahara wangu kdogo kidogo ila kila mwaka nataka nipande at least 10 hectares.
 
Asante sana kwa taarifa njema. Nami baada ya kusoma kwa muda mrefu na kujitafakarisha nimeamua kuingia. ..mwezi February mwanzoni nategemea kwennda Njombe, nitapitia Mapanda (jirani na Mafinga) kwa ajili kununua shamba angalau eka 5.
 
Mie nataka kulima miti ya Mininga kwa ajiri ya mbao. Plz naombeni mwongozo. Je, miti hii itakua tayari kuvunwa baada ya muda gani? Na je, ni mikoa gani inafaa kwa kilimo hiki?
 
Mie nataka kulima miti ya Mininga kwa ajiri ya mbao. Plz naombeni mwongozo. Je, miti hii itakua tayari kuvunwa baada ya muda gani?na jee ni mikoa gani inafaa kwa kilimo hiki?

Sina uhakika sana lakini nimesikia kuwa mninga huchukua kama miaka 80 hivi.
 
U
Ninashukuru sana kwa hii topic, hata mimi nipo interested sana na kupanda miti na ni idea ya muda sasa, issue kwangu ni namna ya kuanza especially kupata shamba kwa ajili ya kupanda. Ningeomba kupata japo idea kama ninaweza kupata eneo huko njombe na kwingineko ukizingatia mimi ninaishi dar. Na price inakuwaje, pia gharama za miche kwa sasa ni kiasi gani na kuotesha plus kutunza. Please please mwenye data ninaomba
Naweza kunichek nikuunganishie mashamba.
 
Mimi nigependa kuwahamasisha wanJF kupanda miti ya mbao hasa mbao nyeupe (pines and cypress). Miti hii inasitawi sana sehemu za nyanda za juu kusini.

Mimi nilianza kupanda miti hii kama miaka kumi iliyopita. Nimepanda miti mingi kila mwaka bila kukosa. Kwa sasa ninazo ekari nyingi za miti hii. Vile vile miaka ya karibuni nimepanda eucalyptus.

Wakati naanza kupanda miti mche mmoja nilikuwa nanunua kwa Shs 50 na kuupanda kwa Shs 20. Kwa vile napanda miti mingi (zaidi ya laki moja kwa mwaka) baadaye niliamua kuotesha miche mimi mwenyewe ili kupunguza gharama.

Gharama zaidi ya miche na upandaji ni barabara za moto kuzunguka msitu. Hata hivyo nilinunua ngómbe na kuwaweka kwenye shamba ili wale majani yanayozunguka msitu. Wamenisaidia sana.

Unaweza kupanda miti kidogo kidogo kila mwaka kutumia mshahara wako kama nilivyofanya mimi. Baada ya miaka kadhaa utakuwa na miti mingi na utaweza kuwa unauza miti au kupasua mbao kila mwaka.
Mkuu asante kwa taarifa. Tukihitaji mashamba huko Njombe waweza kutusaidia kuyapata? Ekari moja ni shilingi ngapi? Liwe pori la kuanza kufyeka mwenyewe.
 
Mkuu asante kwa taarifa. Tukihitaji mashamba huko Njombe waweza kutusaidia kuyapata? Ekari moja ni shilingi ngapi? Liwe pori la kuanza kufyeka mwenyewe.

Mimi kwa sasa siwezi kukusaidia ila wasiliana na Malila
 
Naombeni msaada juu ya hili,kwa wale wanaofanya biashara ya mbao au waliowahi kufanya biashara hii,naomba kujua changamoto zake na faida zake. Mtaji wake chini ni pesa ngapi, gharama ya kibali, na nikiwa mgeni katika soko nini kitatokea.

Asanteni.

Nawasilisha wakuu.

Sent from my Y3 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom