Biashara ya Nafaka mtaji mkubwa faida kiduchu

Hajui tu,Mimi nililima viazi eka 3 Kwa laki gharama ya 500,000. Nikapata elfu 15,000.huwezi kuamini! Mvua ziliharibu viazi shambani,watu wanafikiria kulima ni rahisi hivyo.
Kilimo chetu ni mchezo wa kubet
 
Tani 30 ilikuwa inakuchukua muda gani kukusanya na kuuza?
 
Endelea na biashara...usikate tamaa. Hata wenye sheli wauza mafuta wanachokusanya ni sh 20 au 30 kwa lita. Kwa kuwa mzunguko mkubwa na wanauza kwa wingi..hyohyo sh 20 hadi 30 wanazokusanya ndio tunawaita matajiri.

Ukitaka kutoboa aisha ufanye biashara haramu katika biashara halal. Au ufanye biashara halali katika biashara haramu.
 
Niliifanya pia ikanishinda back in 2015-2016. Niliona nahangaika sana na faida haba. Then unawapelekea wafanyabiashara wanakaa na mali wanakuja kulipa baadaye. Nikaachana nayo.
 
Usemacho ni kweli, nina experience hiyo mzigo mkubwa faida ndogo, Hustle za kutosha.
 
Malizia ukiwa na eneo la kuuzia unapataje? Napo
 
Boss hiyo hela ni nyingi sana na hatari kuiweka kwenye kikapu kimoja,vipi likitokea la kutokea,ajali moto n.k au ndo mzigo hua unakua na bima?

Anyways kama bado una tafuta biashara karibu kuna biashara nilifanya japo kwa uchache ila ilikua na faida,kikubwa inataka usimamizi na uwe na uwezo wa kufikia watu wengi maana yake uwe na mtaji.

1. Aina ya bidhaa ni chakula(cookies)
2. Muda wa ku-expire bidhaa ni 12 months
3. Mfumo wa biashara ni mzalishaji na ni distributer kwenye madukani,then unagawana faida na mwenye duka.

4. Namna ya kuzalisha,unachanganya viungo na kuoka,then unafanya packaging.

Ukiwa na mashine ya kufanya packaging itakua nzuri sana maana vitu vyenyewe ni vidogo vidogo,so vinahitaji speed kuvipack

5. Thamani ya bidhaa kwa end user ni Tsh.. 100

Kwa kiasi cha 2.5m faida ni wastani wa Tsh 350,000/- kwa mwezi sawa na wastani wa Tsh 11,666.....kwa siku.

Kama mtaji utakuwa mara 2 yake faida itakuwa mara mbili na kuendelea

5. Biashara ina unique code ya kibiashara imejificha katika ladha.... Hivyo ni ngumu kuiga ladha labda uvujishe siri ya mchanganyiko wako.

6.Wateja ni maeneo yenye watu wengi..mfano stendi,maduka ya shule,vyuoni,na maduka ya mtaani(Vioski)

Kama utaifanya iwe serious yani ukafanya packeging vizuri,kuzalisha kwa wingi,kutafuta mawakala wa kusambaza,na ukasambaza hadi maduka ya mikoani faida utapata...

Mimi nilijaribu kusambaza maduka jirani na maeneo ya shule na mitaani...

Kwenye Tsh 100 faida baada ya kugawana na mwenye duk unaweza pata tsh 25 hadi 35,

Ila kwa jumla ya bidhaa kwa mtaji wa 2.5m hukosi 350,000/- kwa mwezi


Utaratibu.

1. Ununue kanuni(formulas) za kutengeneza bidhaa na radha zake,ambapo hii itakufanya uzalishe bidhaa,ufanye packaging,u-supply,na ukusanye mapato mwenyewe au na timu yako

2. Uingie ubia kisheria na mwenye formula ya bidhaa,ambapo yeye atatengeneza bidhaa,na wewe ufanye packaging,kusupply na kukusanya mapato.

3. Uingie ubia kisheria na mwenye formula ya bidhaa,ambapo yeye atatengeneza bidhaa, afanye packaging,na kussuply.Wewe ubakie kukusanya mapato.


4. Uingie ubia kisheria uweke mtaji wa uzalishaji bidhaa,ambapo mzalishaji atatengeneza bidhaa, afanye packaging,ku-supply akusanye mapato.




Who ever interested DM
 
Kaka mtaji more than 30 million faida Tzs 2.5 million per month.. kaka faida n ndogo compared to capital invested n hustling aiseee..
It is almost 10%
Fikiria mtu aliyewekeza 300milion kwenye nyumba za kupangisha atapata only 1.0m per month.
Aliyewekeza 30m kwenye nyumba ya kupangisha ataingiza only 150k per month.
 
Uko sahihi mimi nilifanya nikawa napata faida 500 mpaka 600 nimefanya kwa mwaka mmoja pekee na nilikua na mtu nasupply kwake sema mwisho kashtuka bei ila nimekacha nishapiga faida kama 40m. Inatosha sasa ila unatakiwa uwe mjanja aisee lasivyo unaweza kula hasara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…