Hii biashara ni nzuri na inatoka lakini bila kua mjanja mjanja basi kutoboa ni ngumu sana, zaidi ya kupata hela ya kula tu kwasababu faida yake kwa kila kilo ni tsh 50-100...haiwezi kuzidi hapo.
Nilikua na million 6 nikasema nikaangalie swala la mahindi, unaweza kujaza gari la tani 10, gunia 100, baada ya kufikisha sokoni ukapata faida ya laki 3, imagine fuso zima unapata faida ya laki 2-3 ni ndogo ukilinganisha na hustling huko vijijini porini mashambani inaweza kuchukua hata week 2, na ukifika sokoni kama huna sehemu ya kuuzia umpe mfanyabiashara kwa mkopo akiuza ndio akupe hela.
Kwenye maharage ni hivyo hivyo, unanunua gunia kwa 2500/= shambani/mnadani unakuja kuuza kwa 2600/=....imagine unanunua kilo 2000, ambayo ni kama 5,000,000/= alafu unaenda kuuza kwa 2600/= ambayo ni sawa na 5,200,000/=....
Investment ya million 5 upate laki mbili, million 10 upate laki 4, sasa hii biashara si pasua kichwa? Ingekua kwa mwezi unaenda safari 3/4 ingekuwa poa sana, lakini unajikuta kwa mwezi mpaka mzigo uishe unaenda mara moja tu,..
Lakini ukiwa na mzunguko mzuri na ukawa na eneo lako la kuuzia basi hii biashara utaipenda.
Boss hiyo hela ni nyingi sana na hatari kuiweka kwenye kikapu kimoja,vipi likitokea la kutokea,ajali moto n.k au ndo mzigo hua unakua na bima?
Anyways kama bado una tafuta biashara karibu kuna biashara nilifanya japo kwa uchache ila ilikua na faida,kikubwa inataka usimamizi na uwe na uwezo wa kufikia watu wengi maana yake uwe na mtaji.
1. Aina ya bidhaa ni chakula(cookies)
2. Muda wa ku-expire bidhaa ni 12 months
3. Mfumo wa biashara ni mzalishaji na ni distributer kwenye madukani,then unagawana faida na mwenye duka.
4. Namna ya kuzalisha,unachanganya viungo na kuoka,then unafanya packaging.
Ukiwa na mashine ya kufanya packaging itakua nzuri sana maana vitu vyenyewe ni vidogo vidogo,so vinahitaji speed kuvipack
5. Thamani ya bidhaa kwa end user ni Tsh.. 100
Kwa kiasi cha 2.5m faida ni wastani wa Tsh 350,000/- kwa mwezi sawa na wastani wa Tsh 11,666.....kwa siku.
Kama mtaji utakuwa mara 2 yake faida itakuwa mara mbili na kuendelea
5. Biashara ina unique code ya kibiashara imejificha katika ladha.... Hivyo ni ngumu kuiga ladha labda uvujishe siri ya mchanganyiko wako.
6.Wateja ni maeneo yenye watu wengi..mfano stendi,maduka ya shule,vyuoni,na maduka ya mtaani(Vioski)
Kama utaifanya iwe serious yani ukafanya packeging vizuri,kuzalisha kwa wingi,kutafuta mawakala wa kusambaza,na ukasambaza hadi maduka ya mikoani faida utapata...
Mimi nilijaribu kusambaza maduka jirani na maeneo ya shule na mitaani...
Kwenye Tsh 100 faida baada ya kugawana na mwenye duk unaweza pata tsh 25 hadi 35,
Ila kwa jumla ya bidhaa kwa mtaji wa 2.5m hukosi 350,000/- kwa mwezi
Utaratibu.
1. Ununue kanuni(formulas) za kutengeneza bidhaa na radha zake,ambapo hii itakufanya uzalishe bidhaa,ufanye packaging,u-supply,na ukusanye mapato mwenyewe au na timu yako
2. Uingie ubia kisheria na mwenye formula ya bidhaa,ambapo yeye atatengeneza bidhaa,na wewe ufanye packaging,kusupply na kukusanya mapato.
3. Uingie ubia kisheria na mwenye formula ya bidhaa,ambapo yeye atatengeneza bidhaa, afanye packaging,na kussuply.Wewe ubakie kukusanya mapato.
4. Uingie ubia kisheria uweke mtaji wa uzalishaji bidhaa,ambapo mzalishaji atatengeneza bidhaa, afanye packaging,ku-supply akusanye mapato.
Who ever interested DM