Biashara ya nguo, viatu, mikoba na cosmetics kutoka Uganda

Ni kweli tatizo mtaji. Mtaji ndio tatizo na mambo za kukopa si nzuri.

Ila unaweza kwenda kusafisha macho wikend moja.

Hilo la kusafisha macho jamaa nalo neno..nafikiri nikishajionea mwenyewe nitapata ufaham zaidi kuhusu cha kufanya..... binafsi nko boda hapa nahangaika na vishughuli vya hapa na pale.....nataaman hawa wafanyabiashara wa mikoani wangekuwa wanaishia kwangu nafata mizgo mwenyewe wakja hawana haja ya kuvuka mpaka Kampala nawauzia kwa bei pouwa
 
Habari wana jamvi,naomba ushauri nataka kwenda uganda kuleta nguo za mitumba,pochi na viatu pamoja na vipodozi napenda kujua cha kufanya maana ndo nataka kuanza ikiwemo accomodation nikiwa uganda,je huku Tanzania nitaziuzaje,mtaji kwa mzigo wa kwanza uwe shingapi vip usafiri,Ushuru na TRA? Msaada plz.

thamns sana ngoja nikupm
 
sikuwa na access ya net naomba nikupm kwa maelezo zaid
.....JE NILIENDELEA AMA?...
Kwa kweli sijarud tena kuchukua huko mzigo nikaamua kubadili upepo, nikaenda maduka ya hapa dsm kwa wahindi wapumbavu watupu, wezi wale, matusi yao mizigo mibaya kama roho zao, just hasara juu ya hasara...
Kwa sasa nachukua nguo ilala na zinanilipa, kuna jamaa pale wana vijana wao wanapoint nguo kali kali wenyewe wanaita sumu, then inapofika mchana wanazitundika kwa pamoja, wamenizoe nikifika mfano mtu ana nguo kama elf 5000 katundika anakuruhusu uchague zile utakazo na wanafanyaje
1.tops nachukuaga kwa 3000 unauza elf 8000
2. Gauni ndef nachukuwa kwa 8000 nauza mwisho 15,000
3.gauni fupi 5000 nauza elf 10 mwisho
4.skin jeans nachukulia elf 5, nauza 10,000 mwisho,
5.sketi fupi 5000 na kuuza 10elf,
hvyo naona bora hii ya bongo kuliko uganda, sikutaka kuwa mchoyo kwan jf imenisaidia mengi ktk maisha yangu, pia kama kuna m2 ana ushauri kuhusu the way ninavyofanya hii biashara namkaribisha, kama kuna sehemu nyngne pana soko zuri la mtumba namkaribisha pia, nimeandika mara nyngi nyingi coz natumia 4n kuandika, karibuni wadau tusaidiane hasa vijana maisha yasonge mbele.
 
Uganda nguo ni bei nafuu sana kwa sababu nchi za America,Asia na Europe zimefanya uganda kama sehemu ya kupeleke nguo ,begi,viatu etc kutokana na kuwa hawana urasimu wa biashara na kodi ni kidogo sana.Tanzania kuna urasimu na kukandamiza sana wafanyabashara kwa njia za kodi.kule wanasapoti wafanyabiashara kwa vitendo.

Pia soko ni kubwa kuna watu toka tanzania,Kenya ,rwanda,Congo,Burundi,Eritrea,Ethiopia,China,India etc na hakuna sheria kali za uhamiaji kama tanzania kwa ufupi kule hakuna kufatiliana utaifa ni free kabisa.Twende kwenye maswali yako sasa,

Sehemu ambazo unaweza nunua mzigo ni city centre lakin mitaa ya Ben Kiwanuka,Tax park,Copper complex,Arua park na Owino market na sehemu jiran na Owino market.
Kwa vile unataka mitumba ingia Owino Market uko vitu ni bei rahis sana ila inahitaji ubageini na ni lazima ubageini,viatu ( TimberLand )ambavyo nanunua Tanzania 90,000 tzsh kule nanunua kwa 15,000-18,000 tzsh ila wanakuanzia mbali unaomba upunguziwe.
Uko Owino wafanyabiashara wanajua kiswahili vizuri ila ukiambiwa bei,wewe sema ambayo ni kidogo sana kutegemea na mzigo pia wakat unanunua ndio wakat mzuri wa kujua pia utauza kiasi gani.
Tshirt ya 15,000 tzsh pale unapata kwa 1,500 tzsh tena hiyo bei rejareja kwa wewe ukinunua kwa uwingi bei ni rahis sana.Uganda imefanywa kama dampo la bidhaa hizo na watu wa ulaya,asia na america.

Sehemu ya kulala maeneo ya copper complex kuna guest nzuri moja inaitwa Galaxy Guest house ni nzuri sana,bei zake ni ndogo sana kutegemea na unachukua room gani bei uanzia 15,000 ugsh hadi 30,000 Ugsh ndio bei ya juu kabisa.
room zipo ghorofan chini ni mgahawa,pia ukikuta imejaa jiran na hapo kuna nyingine Boston guest house ni nzuri pia na ata wafanyakaz wa hapo uongea kiswahili .bei zake ni ndogo.na hizo sehemu ni jiran na shoprite pia kutoka hapo hadi owino ni dakika 2 tu kutembea na hizo sehemu ndio kwenye maduka mbalimbali.

Kuhusu kodi,kuna mbinu inafanyika nitaku pm si vizuri nikieleza hapa.Kuna njia mbili za kwenda uko kuna njia ya kupitia Nairobi hadi Kampala na kuna jia ya kati hadi Bukoba kisha unapanda bus za Friends huondoka saa moja asubuh kutoka bukoba kwenda kampala,na saa sita na nusu uko kampala,ukifika hapo chukua bodaboda hadi Galaxy Guest house au Boston zipo maeneo ya copper complex jiran na shoprite ambapo kwa bodaboda haizid 2000 ugsh.

Pia ata maeneo ya Arua park kuna guest za kulala pia. ( hayo maeneo ni kama unavyoona kariakoo majina ninayotaja ni kama mitaa tu mfano msimbazi etc hizo sehemu ziko jiran jirani )

Rate za ubadilisha pesa ni 1.5 hadi 1.6
yani 1,000 Tzsh ni 1550-1600 Ugsh.
wakat ambapo shule zinafunguliwa rate inashuka sababu wanafunz wengi wa kitanzania wanakuja na pesa na wanachange inaweza pungua hadi 1.5 au 1.55.

kuna bus kama Falcon utoka dar kupitia njia ya kati hadi bukoba kisha kampala.
njia ya nai mfano kuna spider utokea dar-nairob-kampala.

ni wewe sasa kuamua,nawajua watu wengi wanawake/wanaume wamefanikiwa sana kimaisha kupitia biashara hii.cha muhimu ukinunua kitu uombe sana kupunguziwa pia usiingiwe tamaa za kununua vitu ambavyo hukupanga kuna vitu vizuri sana kule na cha muhimu kuwa makini ili usiibiwe pesa,uporaji kule hakuna labda mtu achane pochi yake bila wewe kujua.

mkiwa na swali ulizeni

Webale nyo,webale indala sebbo.Maelezo yako yanaonesha unaijua vilivyo kampala.
 
Hilo la kusafisha macho jamaa nalo neno..nafikiri nikishajionea mwenyewe nitapata ufaham zaidi kuhusu cha kufanya..... binafsi nko boda hapa nahangaika na vishughuli vya hapa na pale.....nataaman hawa wafanyabiashara wa mikoani wangekuwa wanaishia kwangu nafata mizgo mwenyewe wakja hawana haja ya kuvuka mpaka Kampala nawauzia kwa bei pouwa

Ilo linawezekana unaweza kununua kwa jumla na kuwasambazia au ukifungua duka kubwa boda hapo Mtukula.

Ila mtaji unahusika hapo
 
uko boda ya wapi,uganda?. Huwa najiuliza kwanini wafanyabiashara wa bukoba wanafanya mahemezi kahama na sio kampala.
 
Nikwel jamaa mtaj wa maana unahitajika Jah live ngoja nijichange kujipanga sina budi ndugu...
 
uko boda ya wapi,uganda?. Huwa najiuliza kwanini wafanyabiashara wa bukoba wanafanya mahemezi kahama na sio kampala.
Nipo Mutukula ndugu... hilo la wafanyabiashara wa Bukoba kufata mizigo Kahama sijalisikia sana labda Buseresere nasikia huko bidhaa ni bei pouwa. Tatzo la ndugu zetu wa Bukoba (wahaya) wanataka faida kubwa sana kwa mara moja, so hata kama kuna dealer analeta mizigo mizur kutoka nje bei yake lazima itakuwa ni kubwa....
 
Uganda nguo ni bei nafuu sana kwa sababu nchi za America,Asia na Europe zimefanya uganda kama sehemu ya kupeleke nguo ,begi,viatu etc kutokana na kuwa hawana urasimu wa biashara na kodi ni kidogo sana.Tanzania kuna urasimu na kukandamiza sana wafanyabashara kwa njia za kodi.kule wanasapoti wafanyabiashara kwa vitendo.

Pia soko ni kubwa kuna watu toka tanzania,Kenya ,rwanda,Congo,Burundi,Eritrea,Ethiopia,China,India etc na hakuna sheria kali za uhamiaji kama tanzania kwa ufupi kule hakuna kufatiliana utaifa ni free kabisa.Twende kwenye maswali yako sasa,

Sehemu ambazo unaweza nunua mzigo ni city centre lakin mitaa ya Ben Kiwanuka,Tax park,Copper complex,Arua park na Owino market na sehemu jiran na Owino market.
Kwa vile unataka mitumba ingia Owino Market uko vitu ni bei rahis sana ila inahitaji ubageini na ni lazima ubageini,viatu ( TimberLand )ambavyo nanunua Tanzania 90,000 tzsh kule nanunua kwa 15,000-18,000 tzsh ila wanakuanzia mbali unaomba upunguziwe.
Uko Owino wafanyabiashara wanajua kiswahili vizuri ila ukiambiwa bei,wewe sema ambayo ni kidogo sana kutegemea na mzigo pia wakat unanunua ndio wakat mzuri wa kujua pia utauza kiasi gani.
Tshirt ya 15,000 tzsh pale unapata kwa 1,500 tzsh tena hiyo bei rejareja kwa wewe ukinunua kwa uwingi bei ni rahis sana.Uganda imefanywa kama dampo la bidhaa hizo na watu wa ulaya,asia na america.

Sehemu ya kulala maeneo ya copper complex kuna guest nzuri moja inaitwa Galaxy Guest house ni nzuri sana,bei zake ni ndogo sana kutegemea na unachukua room gani bei uanzia 15,000 ugsh hadi 30,000 Ugsh ndio bei ya juu kabisa.
room zipo ghorofan chini ni mgahawa,pia ukikuta imejaa jiran na hapo kuna nyingine Boston guest house ni nzuri pia na ata wafanyakaz wa hapo uongea kiswahili .bei zake ni ndogo.na hizo sehemu ni jiran na shoprite pia kutoka hapo hadi owino ni dakika 2 tu kutembea na hizo sehemu ndio kwenye maduka mbalimbali.

Kuhusu kodi,kuna mbinu inafanyika nitaku pm si vizuri nikieleza hapa.Kuna njia mbili za kwenda uko kuna njia ya kupitia Nairobi hadi Kampala na kuna jia ya kati hadi Bukoba kisha unapanda bus za Friends huondoka saa moja asubuh kutoka bukoba kwenda kampala,na saa sita na nusu uko kampala,ukifika hapo chukua bodaboda hadi Galaxy Guest house au Boston zipo maeneo ya copper complex jiran na shoprite ambapo kwa bodaboda haizid 2000 ugsh.

Pia ata maeneo ya Arua park kuna guest za kulala pia. ( hayo maeneo ni kama unavyoona kariakoo majina ninayotaja ni kama mitaa tu mfano msimbazi etc hizo sehemu ziko jiran jirani )

Rate za ubadilisha pesa ni 1.5 hadi 1.6
yani 1,000 Tzsh ni 1550-1600 Ugsh.
wakat ambapo shule zinafunguliwa rate inashuka sababu wanafunz wengi wa kitanzania wanakuja na pesa na wanachange inaweza pungua hadi 1.5 au 1.55.

kuna bus kama Falcon utoka dar kupitia njia ya kati hadi bukoba kisha kampala.
njia ya nai mfano kuna spider utokea dar-nairob-kampala.

ni wewe sasa kuamua,nawajua watu wengi wanawake/wanaume wamefanikiwa sana kimaisha kupitia biashara hii.cha muhimu ukinunua kitu uombe sana kupunguziwa pia usiingiwe tamaa za kununua vitu ambavyo hukupanga kuna vitu vizuri sana kule na cha muhimu kuwa makini ili usiibiwe pesa,uporaji kule hakuna labda mtu achane pochi yake bila wewe kujua.

mkiwa na swali ulizeni

Mkuu hongera kwa kuwa msaada mzuri
 
Sihishi Uganda ila uwa naenda. Ata mwezi huu naweza nikaenda. Bado sijakata ticket hivo nikikata ndio itakuwa uhakika

mkuu mie nlikua nataka nijue pia kuhusu nguo za special,je nazo znapatikana kwenye hzo market ulizotaja?money stunna!
 
Zinapatikana mkuu. Kuna mtu niliwai kumnunulia nguo uko anaishi Mwanza kwa nguo moja nilinunua 2,400 ugsh na nyingine ya bei sana 3,000 cha ajabu akaniambia aliziuza kwa 25,000 tzsh adi 30,000tzsh ( zilikuwa nguo special za watoto wa miaka 3-6) ilikuwa 2010
 
thenkyuu mkuu! Tutaftana zaidi ili uweze nisaidia kuhusu hli! Kama hutojal,
 
Back
Top Bottom