Biashara ya nguo, viatu, mikoba na cosmetics kutoka Uganda

Biashara ya nguo, viatu, mikoba na cosmetics kutoka Uganda

Zinapatikana mkuu. Kuna mtu niliwai kumnunulia nguo uko anaishi Mwanza kwa nguo moja nilinunua 2,400 ugsh na nyingine ya bei sana 3,000 cha ajabu akaniambia aliziuza kwa 25,000 tzsh adi 30,000tzsh ( zilikuwa nguo special za watoto wa miaka 3-6) ilikuwa 2010

mkuu tunakushukuru kwa elimu unayotupa.mimi nina duka la nguo za special za kiume,maana dar tunanunua kwa bei kubwa sana,mfano shirt 15,000.huko uganda inakuaje?au naomba kuwasiliana kwa ushauri zaidi maana inaonyesha unaijua uganda kibiashara zaid.0719640960
 
Zinapatikana mkuu. Kuna mtu niliwai kumnunulia nguo uko anaishi Mwanza kwa nguo moja nilinunua 2,400 ugsh na nyingine ya bei sana 3,000 cha ajabu akaniambia aliziuza kwa 25,000 tzsh adi 30,000tzsh ( zilikuwa nguo special za watoto wa miaka 3-6) ilikuwa 2010

wafanyabiashara wa bongo wana tamaa sana. nguo ananunua elfu tatu anaiuza elf 30!!! mmmh.
money stunna tumefaidika na darasa lako hapa. santee!
 
Kuna mpaka wafanyaiashara wanatoka maeneo ya Mbeya,Tabora n.k nao nawaona wanakwenda kwa basi Ug wanachukua mzigo na kurudi nao hapa Tz na hata hapa K.k wengine wanachukua huko Ug
 
Habari wana jamvi,naomba ushauri nataka kwenda uganda kuleta nguo za mitumba,pochi na viatu pamoja na vipodozi napenda kujua cha kufanya maana ndo nataka kuanza ikiwemo accomodation nikiwa uganda,je huku Tanzania nitaziuzaje,mtaji kwa mzigo wa kwanza uwe shingapi vip usafiri,Ushuru na TRA? Msaada plz.

Asante sana kwa kaelezo mazuri kiongozi,nimeamini kweli”information is power”je ni siku gani !nzuri yq kufanya shopping?vp weekends wanafungua maduka??
 
Aksante kwadarasa money stunna nawachangiaji wote.. mimi nipo musoma nataka kuanza biashara ya vitu vyawatoto kama toys,baby walker,bouncer, vitanda tafadhali mwenye kufahamu maduka yanamna iyo ug.. price zao zipo poa kama Kwenye nguo?
 
Sipo ug ila uwa naenda. Na pia nishafanya biashara uko za kuwapelekea mizigo fulani pia nimenunua nyumba uko maeneo ya Munyonyo karibu na gaba

poa sana kaka..naomba tuwasiliane kupitia simu,mana mi mgeni humu..hata kum MP mtu siwezi ndo naendelea kujifunza.tafadhali kaka.
 
Uganda nguo ni bei nafuu sana kwa sababu nchi za America,Asia na Europe zimefanya uganda kama sehemu ya kupeleke nguo ,begi,viatu etc kutokana na kuwa hawana urasimu wa biashara na kodi ni kidogo sana.Tanzania kuna urasimu na kukandamiza sana wafanyabashara kwa njia za kodi.kule wanasapoti wafanyabiashara kwa vitendo.

Pia soko ni kubwa kuna watu toka tanzania,Kenya ,rwanda,Congo,Burundi,Eritrea,Ethiopia,China,India etc na hakuna sheria kali za uhamiaji kama tanzania kwa ufupi kule hakuna kufatiliana utaifa ni free kabisa.Twende kwenye maswali yako sasa,

Sehemu ambazo unaweza nunua mzigo ni city centre lakin mitaa ya Ben Kiwanuka,Tax park,Copper complex,Arua park na Owino market na sehemu jiran na Owino market.
Kwa vile unataka mitumba ingia Owino Market uko vitu ni bei rahis sana ila inahitaji ubageini na ni lazima ubageini,viatu ( TimberLand )ambavyo nanunua Tanzania 90,000 tzsh kule nanunua kwa 15,000-18,000 tzsh ila wanakuanzia mbali unaomba upunguziwe.
Uko Owino wafanyabiashara wanajua kiswahili vizuri ila ukiambiwa bei,wewe sema ambayo ni kidogo sana kutegemea na mzigo pia wakat unanunua ndio wakat mzuri wa kujua pia utauza kiasi gani.
Tshirt ya 15,000 tzsh pale unapata kwa 1,500 tzsh tena hiyo bei rejareja kwa wewe ukinunua kwa uwingi bei ni rahis sana.Uganda imefanywa kama dampo la bidhaa hizo na watu wa ulaya,asia na america.

Sehemu ya kulala maeneo ya copper complex kuna guest nzuri moja inaitwa Galaxy Guest house ni nzuri sana,bei zake ni ndogo sana kutegemea na unachukua room gani bei uanzia 15,000 ugsh hadi 30,000 Ugsh ndio bei ya juu kabisa.
room zipo ghorofan chini ni mgahawa,pia ukikuta imejaa jiran na hapo kuna nyingine Boston guest house ni nzuri pia na ata wafanyakaz wa hapo uongea kiswahili .bei zake ni ndogo.na hizo sehemu ni jiran na shoprite pia kutoka hapo hadi owino ni dakika 2 tu kutembea na hizo sehemu ndio kwenye maduka mbalimbali.

Kuhusu kodi,kuna mbinu inafanyika nitaku pm si vizuri nikieleza hapa.Kuna njia mbili za kwenda uko kuna njia ya kupitia Nairobi hadi Kampala na kuna jia ya kati hadi Bukoba kisha unapanda bus za Friends huondoka saa moja asubuh kutoka bukoba kwenda kampala,na saa sita na nusu uko kampala,ukifika hapo chukua bodaboda hadi Galaxy Guest house au Boston zipo maeneo ya copper complex jiran na shoprite ambapo kwa bodaboda haizid 2000 ugsh.

Pia ata maeneo ya Arua park kuna guest za kulala pia. ( hayo maeneo ni kama unavyoona kariakoo majina ninayotaja ni kama mitaa tu mfano msimbazi etc hizo sehemu ziko jiran jirani )

Rate za ubadilisha pesa ni 1.5 hadi 1.6
yani 1,000 Tzsh ni 1550-1600 Ugsh.
wakat ambapo shule zinafunguliwa rate inashuka sababu wanafunz wengi wa kitanzania wanakuja na pesa na wanachange inaweza pungua hadi 1.5 au 1.55.

kuna bus kama Falcon utoka dar kupitia njia ya kati hadi bukoba kisha kampala.
njia ya nai mfano kuna spider utokea dar-nairob-kampala.

ni wewe sasa kuamua,nawajua watu wengi wanawake/wanaume wamefanikiwa sana kimaisha kupitia biashara hii.cha muhimu ukinunua kitu uombe sana kupunguziwa pia usiingiwe tamaa za kununua vitu ambavyo hukupanga kuna vitu vizuri sana kule na cha muhimu kuwa makini ili usiibiwe pesa,uporaji kule hakuna labda mtu achane pochi yake bila wewe kujua.

mkiwa na swali ulizeni
JF ni zaidi ya shule! Asante sana kiongozi. Vp ukiwa na mtaji wa kama milion 1.5 na uko dar hii biashara mtu unaweza ukaimudu?
 
Sipo ug ila uwa naenda. Na pia nishafanya biashara uko za kuwapelekea mizigo fulani pia nimenunua nyumba uko maeneo ya Munyonyo karibu na gaba

aaah Gaba!!! nilienda pale beach wakati wa honeymoon yangu! Halafu nilifanya shopping ya nguvu pale Mukwano. Nafikiri kuna mambo nahitaji kuyafanya hivi karibuni nitakuja kukutafuta humu kamanda!
 
Mtaji wa kama mil 4.5 upo,ishu ni soko la kuja kuuzia,kwa sehemu kama dar jamani kupata sehemu ambayo biashara ya nguo inalipa kodi yake si ndo itakufilisi
 
Back
Top Bottom