Habari za usiku huu mabibi na mabwana..
Mimi ni miongoni ya waliokosa ajira mpaka sasa, kutokana na hali hiyo nimejidunduliza na kupata M1. Kipindi nasoma chuo nilikua nafanya biashara ndogondogo nikiwa naishi hapo hapo hostel. Pia nilikua nazunguka hostel nyingine kike mbalimbali jijini Dsm nyakati za jioni, kuwauzia nguo za mitumba,nguo za ndani na chochote kile atakachoniagiza mteja naenda kujumua namletea kama pafyumu, belt au saa.
Naomba nisiwachoshe sana nina mtaji wa Milion 1 tu nataka niende Uganda kununua vitu kule nije kuuza huku kwetu. Nimejaribu kupitia uzi mbalimbali za miaka ya nyuma za biashara hiyo, nimepata mawili matatu.
Sasa kutokana na miaka kwenda naombeni maoni au ushauri kwa watu wanaofanya biashara hii hivi sasa.
Asanteni