Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

Ndo nataka niifanye na mie. Tatizo wahindi wanachakachua first class...la ndo ufate kampala au nairobi au ujilipue kuagiza nje, lakini kuna chimbo nimeligundua acha nitake risk nione zitakuwaje
Kaka tusaidiane na mimi nimekuja Dar nataka nikirudi mkoani nirudi na mtumba ili niuze.
 
Wakuu naomba ushauri wenu mimi nipo nchini MLW nimepata fremu nataka nifungue duka la nguo za kiume jeans tshirts caps shirts belts Saa na vitu vingine vya kiume lkn changamoto yangu nimepata fremu ya ndani ya jengo je nifanyeje ili wateja wajue kuna duka lenye nguo kali kwa ndani.
 
Ngoja waje watu wa Malawi wakushauri mi napita
[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
kwa dar nenda mnazi mmoja kwenye maduka ya wahindi,utaona maduka mengi sana ya mitumba.

(1) Belo grade A Kg 45-55 kwa nguo za kiume ni laki5-4,kila belo lina nguo 200-250..Grade B laki3-2.8
(2) nguo za watoto. -Nguo nyepesi kuanzia umri 0-6yrs mpaka 2-12yrs grade A laki5-4.5
-Nguo za kawaida umri 0-6yrs na 2-12yrs grade A laki4-3.
Grad B nguo za watoto ni laki2.5
(3) Nguo za kike grade A laki3,grade B laki2-1.8
NB:Ila bhana sasa hivi nguo wanachakachua sana kama sio mzoefu unaweza kununua grade A ukaja kukutana na mafampa.

Ukitaka belo lenye nguo nzuri mpe cha juu mfanyakazi utakayekutana nae apo,lakini ukijifanya bandidu inakula kwako

great thinker
 
mkuu,

Mimi pia nitaanza biashara hii wiki ijayo hapa dar es salaam,japokuwa sina uzoefu wowote kuhusu biashara hii isipokuwa imekuwa kichwani muda mrefu na ninaipenda toka moyoni na pia kabla ya kuamua nilipata ABC kuihusu.

Nilipitia maandiko ya wajasiliamali mitandaoni na pia wadau wengine wenye uzoefu wa biashara hii na hata kuomba ushauri kwa wafanyabiashara wenyewe wanaofanya biashara hii pale Kariakoo na kwingineko.

Wengi wanasema biashara ya mitumba kwa ujumla inalipa sana isipokuwa inahitaji umakini katika manunuzi ya mzigo ili utengeneze faida.

Kwa maoni yao wanasema;
~Ukiwa ndo unaanza kufanya biashara hii ni mara mia ukanunue mzigo pale Ilala sokoni has a kwenye ule mnada unaoanza saa 4 aksubuhi kuliko kununua balo kwani wafanyabiashara wa Kariakoo wengi si waaminifu wanaweza kukuuzia balo lenye malonya mengi na hivyo kwa vyovyote mzigo utakukata na kukusababishia hasara.

Wanashauri kwa mfanyabiashara anayeanza ni vema apate uzoefu wa kutosha na connection ya uhakika kabla ya kuamua kwenda kununua balo la nguo pale.

Nyongeza ya hilo,kwa kuwa huna uzoefu wa kutosha,wafanyabiashara wa kariakoo ni rahisi kukuibia kwa kutojua tu grades za mabalo amboyo kimsingi yanatofautiana quality na bei,

Mfano;kuna mabalo yanauzwa kuanzia 150,000-600,000 kwahiyo unaweza hitaji balo let's say la (laki 4) na wao wakakupatia la (laki 1.5),kwa vyovyote hapo itakuwa ngumu kwa wewe kugundua kama umetapeliwa hadi utakapoiona hasara.

Binafsi nakushauri kanunue mzigo wako pale Ilala sokoni,achana na habari za balo katika hatua hizi za awali otherwise uwe na mtu wa kuaminika kwelikweli pale Kariakoo ambaye atakusaidia upate mzigo unaoutarajia japo ni ngumu kidogo ila inawezekana.

Aksante.
Umenifungua sana . Niko Moro nataka kuianza hii biashara hivi karibuni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wanajukwaa,

Mimi ni mwajiliwa na nina mpango wa kutafuta njia ya kujiongeza kipato. Katika kuchanganya mawazo nimeona biashara ya haraka haraka ambayo sitahitaji Fremu wala leseni ni kununua balo za mitumba na kupeleka mnadani siku za jumamosi na jumapili ambazo nakuwa off.

Nuomba kupata uzoefu kwa yoyote aliyewahi kufanya biashara hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si nimesikia mitumba imepigwa marufuku au niaje?
 
Habari, naomba ushauri nahitaji kufanya Biashara ya nguo za mtumba nahitaji kujua kati ya Uganda na Bujumbura Burundi ni wapi naweza pata Mzigo mzuri?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio unataka kuanza au?


RubiiKimimi[emoji85]
 
Ndugu zangu, Kwa yoyote aliyewahi kununua mitumba kwa jumla na kupeleka kwenye mnada, naomba kujua hali ya faida na changamoto zake. Maana nimeshawishika kufanya hiyo biashara siku za weekend ambazo ninakuwa Off.
 
Back
Top Bottom