Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

mitaa ya Arua Park, Ben kiwanuka street, jiran na Owino market, Tax park. etc hizo sehemu zimekaribiana pia ukiambiwa 10000 ujue ni 5000 utaangalia na nguo yenyewe

Asante Mkuu. Nitajaribu kwenda huko. Je, passport ni lazima siku hizi?
 
nashangaa kwa nini kampala nguo ni rahisi kuliko Dsm wakati uganda ni land locked country! mm sijui aisee nisaidieni
 
Visa yake ni ya hapohapo board yaani entry tu, au unaomba embassy infact Kenya ni entry tu sifahamu Uganda japo ni part of EAC
 
Visa yake ni ya hapohapo board yaani entry tu,au unaomba embassy infact kenya ni entry tu sifahamu uganda japo ni part of e.a.c

Nchi zote za africa mashariki visa unapata pale pale boda,unagongewa kwenye passport yako na ni bure kabisa kwa nchi wanachama wa afrika mashariki.
 
nashangaa kwa nini kampala nguo ni rahisi kuliko Dsm wakati uganda ni land locked country! mm sijui aisee nisaidieni

Sababu ni hii, Uganda uwa wanaagiza nguo na vitu vingine kwa wingi,pia mizigo yao mingi upitia bandari ya mombasa na uko hakuna mlolongo na usumbufu mwingi kama bandari ya Tanzania.

Pia Uganda hakuna kodi za kukomoana kama za Tanzania na ndio maana ata ukiwa na million 5 ya Tanzania uganda unapata gari nzuri sana.

Tatizo la tanzania imeshindwa kuchukua kodi kwa matajiri hivo inawakamua wafanyabiashara wanyonge.

Pia Uganda ni free kila mtu ni ruksa kufanya biashara hakuna kufatiliana sana kama uku kwetu mara Kimbunga etc
Uganda kuna watu toka Congo, Rwanda, Eritrea, Ethiopia, Somalia, Tanzania, Kenya, China, India etc wanafanya biashara na wamefungua maduka bila kuulizwa mambo za passport wakati uku Tanzania utafatiliwa na utafukuzwa sababu kupata hivo vibali ni pesa nyingi sana.

Uwepo wa jamii tofauti tofaut na kutokuwepo usumbufu au kimbungai umesababisha Kampala kuwa mji mkuu wa biashara kwa raia toka South Sudan, Rwanda, Burundi, Congo, Tanzania, Kenya
 
Habari,

Naombeni ushauri wenu. Nahitaji na natamani kuanza biashara ya mitumba ya nguo na viatu na nipo mkoani singinda. Je, nahitaji mtaji wa sh ngapi ili nianze? Pili, je baro kwanzia daraja la 1-3 ni bei gani kwa kila daraja,na yanapatikana wapi? Na pia naomba wenye uzoefu na hii biashara waniwekee waz changamoto zake na je wamewezaje kufanikiwa?

Kama kuna ambao hawakufanikiwa pia wanisaidie kunijuza kwanini hawakufanikiwa. Msisahau kunijuza na kwa upande wa viatu. Nitashukuru kwa msaaada wanajamii na mungu awabariki
 
Nadhani Kama una milioni moja unaweza anza viatu na Hizo Nguo kwa Nairobi kuna viatu vya mtumba bei ya chini pale Gikombaa unaeza elekezwa namna ya kupata mzigo kwa singida kuna gari la moja kwa moja Hadi Nairobi kupitia Arusha.
 
Kama una mtaji mdogo kamwe usinunue mfuko au baro kama unavyoita. Pamoja na kwamba watakwambia ni grade 1 au ngapu bado haina garantii kuwa utapata nguo au viatu safi. Unaweza ukafungua mfuko ukapata pea moja tu nzuri nyingine zote famba. The same kwa nguo. So ili ufanikiwe kwa kuchukua ma baro lazima uanze na atleast 10 na kuendelea maana mengine utapata na mengine hutapata kitu.

So kwa mtaji wa 1m jaribu kuchagua pea moja moja au nguo moja moja kutoka kwa wale wanao nunua mabaro mengi na kuuza pea moja moja au nguo moja moja kwa bei ya jumla.
 
Asante kwa ushauri iMind, naufanyia kazi
 
Mambo ya kodi yakoje boda?
 
habari,naombeni ushauri wenu. Nahitaji na natamani kuanza biashara ya mitumba ya nguo na viatu na nipo mkoani singinda. Je nahitaji mtaji wa sh ngapi ili nianze? Pili je baro kwanzia daraja la 1-3 ni bei gani kwa kila daraja,na yanapatikana wapi? Na pia naomba wenye uzoefu na hii biashara waniwekee waz changamoto zake na je wamewezaje kufanikiwa? Kama kuna ambao hawakufanikiwa pia wanisaidie kunijuza kwanini hawakufanikiwa. Msisahau kunijuza na kwa upande wa viatu.Nitashukuru kwa msaaada wanajamii na mungu awabariki

Mkuu je biashara ya viatu na nguo inalipa uko singida
 
Sawa ni biashara na ndiyo tunazo vaa Ila kama inataka iwe endelevu uza nguo mpya kwani kuna wakati utafika mitumba ita pigwa zengwe kwa kuongezewa kodi kubwa na lengo isiingie nchini.
 
Unapotaja sehemu za bidhaa rahisi duniani naamini China itakuwa ya kwanza... Karibu sana Guanzhou na hata Hongkong utapata nguo hadi za 0.5USD ukiipeleka Bongo unauza 10USD

nahitaji kufanya biashara ya nguo za kike hasa mitumba nahitaji ushauri wa kina kabla sijaanza kwakuwa wewe ni mzoefu naomba tuwasiliane namba yangu hii hapa +255 0714 4873 11
 
Za leo ndgu zanguni,

Kwa muda mrefu nimekuwa naumiza kichwa, nifanye biashara gani ili niweze kujiongezea kipato, wazo lililonijia ni biashara ya uuzaji wa nguo za mitumba kwa kununua marobota,na kuuza rejareja,je ni changamoto gani zilizopo kwenye biashara hiyo kwani nataka niuze nguo za mchanganyiko za wanaume kwa wanawake watoto na n,k,ni wap naweza kupata bidhaa ya namna hiyo, mi nipo Dar, natanguliza shukrani.
 
Hata mimi hiyo biashara naifuatilia kwa ukaribu sana;mi niko mkoani ila kama uko dsm nenda pale maeneo ya Tazara kariakoo ulizia jamaa mmoja anaitwa LALAN ni supplier mkubwa sana anasupply nchi nzima;
 
Wasiliana na kijana mtafutaji wiseboy atakupa mwanga namna ya kufanikisha hii biashara!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom