mkuu sijui umeshawaza yapi katika biashara unayotaka kufungua. ila ningependa kukushauri jambo moja kabla hujakimbilia kununua lamination machine na laptop nk..
kwa mwelekeo ulio anza nao naona itakua a very begginer approach yani uwe na stationery afu na mashine mbili tatu, uuze 10,000 paka 20,000 kwa siku afu basi.
kama ndo lengo lako kutest na kujifunza hio biashara sawa ila..
kama una malengo makubwa na kama umejiandaa na unataka upambane kweli na kujikwamua ktk uchumi huu.. jaribu kutafuta kwanza “a stronghold approach” ambayo unahisi inaweza kuonesha u seriousness kdg..
kwa mfano uniambie nimefanya tafiti nimeona professionals aina flani labda wanasheria wanahitaji huduma abcd za stationeries au mashule wanachapisha mitihani mamia kila muhula, au maeneo ya vyuo wanafunzi wanahitaji vitu flani vya stationeries, au nimetembelea kumbi za starehe kila siku sherehe kadi wanatoa wapi.. au maofisi mengi kwanini nisiwapunguzie usimbufu wa ku print na copy nk.
ukiwaza hivyo itakusaidia kujua angle gani uingie kwenye hio biashara, utajua unahitaji vifaa gani, mtaji gani, uwaone watu gani.. na naamini utafanikiwa zaidi kwa namna hiyo!
tumia audience ambayo tayari wengine wamekutengenezea.. mfano we muuza jezi unajua wapenda mpira ndo wanunuzi wako, unajua mechi ya simba na yanga jmosi kwann usitumie audience ambayo tff imekutengenezea kupata hao wateja!
tafakari.. !