Heri ya krimasi wana JF. Mimi ni mgeni humu ndani ila nimependezwa sana na JF kwa kuelimisha, kukosoa, kuburudisha na kila kitu kinachoendelea humu.
Nilikua nna wazo la kufungua duka la spea za pikipiki aina ya boxer katika eneo langu nnaloishi kwani kwa kipindi cha miaka miwili ilopita nimeona zikiongezeka kwa kasi sana. huku kwetu maduka ya spea za boxer ni kama hakuna kwani maduka mengi ni ya spea za pikipiki aina nyingine.
nilipenda kujua kama kuna mtu anajua, ni kiasi gani nahitaji kuanza nacho, upatikanaji wa spea zenyewe, na jinsi gani naweza kuvutia wateja kila siku.