Bibi zake mke wangu wakikosa pesa ya kulipa ada wanaanza kutumia mabavu nilipe mahari

Unajitengenezea bomu tu kama una mpango nae malizia mahari yao km.huna mpango nae ungemuacha tu kuliko kumpotezea muda
 
Ushauri kwa Waislamu, nimetaja waislamu makusudi ili wapuuzi wengine wasiliingilie

Muislamu tambua mahari ndio inakupa uhalali wa kumuingilia huyo mke wako,kwahiyo ule ujinga wa kusema mahari haimaliziwi sio katika Uislamu
Kwanza tumia lugha ya kistaarabu ya karne ya 21, kumuingilia ndio kitu gani? Sema kufanya mapenzi au ngono.
Ni imani za ajabu ajabu tu ndio zina hayo maelekezo ya kwamba uhalali wa ngono kati ya watu wawili ni hadi mahari ilipwe(biashara ifanyike), ni ujima mtupu.
 
Hahahah watu wanataka chao umegeuzwa mtaji hapo mkeo yeye anasemaje kwani?
 
Lugha ya kuingilia ndio ya kistaarabu zaidi lau ungejua

Katika uislamu hakuna biashara ndio maana mahari ni zawadi tena kwa mwanamke,na Kizur zaidi mwanamke mwenyewe anasema anataka nini,wengine huolewa kwa kununuliwa msahafu tu,wengine huolewa kwa kutaja mahari ndogo kabisa,hii kuonyesha katika uislamu hakuna biashara

Na mahari hizi hizi ndogo ambazo dada zetu huzitaja,ndio wasio kuwa waislamu huzi dhihaki kwa kusema waislamu wanaolewa kwa mahari ndogo sana,ni ishara kwamba hata wao wameona katika Uislamu hakuna biashara kama kwao

Mahari ni zawadi na halali ya kuhalalisha tendo la ndoa kufanyika baina ya mke na mume katika imani ya kiislamu

Kwahiyo kama huko kwengine mnaona hakuna ulazima, ni shida zenu na sio zetu.

asante.
 
Na wewe jamaa ulikubalije kutoa mahali nyingi kiasi hicho wakati wewe mwenyewe maisha yako ya kuunga UNGA tu ya min -me

Siku hizi mahali ikizidi sana laki 4-7 sasa wewe unatoaje mahali ya 2.7 million?

Mimi naona ubaya uliuanza wewe
Mimi nimefikaje hapo?
 
waislamu wanaolewa kwa mahari ndogo sana,
Juzuu 2 tu na Msaahafu mmoja unachukua mwali wako unaenda kujichapia, jana nimekuta wanawake wamevaaa ushungi wanajadiriana jambo moja wanasema mwanaume kua na mwanamke mmoja sio kweli mwanaume bismillah awe na wanawake kuanzia wawili ila kinyume na hapo mwanaume mke mmoja sio kweli
 

Waambie waje kumchukua. Kisha warudishe na ile ya mwanzo waliyopokea.
 
Mtoto wao yuko kwako?,wacha ujinga lipa mahari..
Unaona wana shida,anasahau bint yao mpaka inamuona wao ndio walimaliza,
Nyang'au wahesiπŸ˜†
 
Wakija tena kudai waambie hela ya kumalizia hiyo huna wala kwakweli hutegemei kuja kupata. Hali ngumu, vitukuu vyao vinasoma. Sometimes unawapigia unawaomba wakusaidie na ada.
 
Kama usumbufu wote huo unatokana na mahari iliyobaki, jikusanye malizia mahari yao halafu usiwe na muda nao.

Kata mazoea na wao.
Na ndio nataka nikifanye.
 
Lengo la kufanya mahari iwe nyepesi ni watu kuoa na kuolewa kuepuka Zinaa

Kwanza mke ukimtolea mahari chache huwezi kumfanya kama mali yako na kumfanya utakavyo,ndio kuna watu wanatengua miguu wake zao na hata kuwaua

Ngono hata wanyama wanafanya,lakini mwanaadamu amepewa hadhi ya juu kwa ubora na heshima,ndio maana ikawekwa ndoa kama takaso na heshima

Kwani ni uongo wanaume haturidhiki na mwanamke mmoja,hata hao wanao Pinga wake wengi utawakuta na mke mmoja na mahawara 4 mpaka 5,kipi bora hapo,anayeoa kihalali na kula halali au yule anayekula haramu?

Ndio maana katika qur'an tumeambiwa tuoe kuanzia wawili,watatu hadi wanne
 
Wapigie hesabu za pesa ulizowatumia kisha deduct kwenye deni la mahari kisha achana nao kwa amani

Wakimchukua mjukuu wao usibishane nao maana lao ni moja.... KUKUTESA
 
Sio kwamba nimedhamilia kuto kuwapa mahali, mamb yang yaliyumba kiasi, we watu gani wanadai mahali nimetoka nimetoka msibani kumzika baba yangu mzazi ile narud tu hata kunipa pole anakuja kudai mahali ihali nimesha lipa M 1 na point.
 
Hahahah watu wanataka chao umegeuzwa mtaji hapo mkeo yeye anasemaje kwani?
Mke akimwambia bibi yake ukweli, bibi anapandwa na presha πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kwa hio tuoe wanne?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…