much know
JF-Expert Member
- Oct 22, 2017
- 14,061
- 21,592
Mke wake hata hahusikiwewe si umwambie mke wako akiondoka ndoa imeisha, sasa hivi anza kutafuta replacement kimya kimya.
Mke wake hata hahusikiwewe si umwambie mke wako akiondoka ndoa imeisha, sasa hivi anza kutafuta replacement kimya kimya.
Mahari ni deni kama ulikubali kuoa kidini.......imetolewa ruksa ya kutoa kidogo ili kuepusha zinaa na hali ya kuwa muoaji hana uwezo kwa muda huo lakini kama uwezo wa kulipa unao na umefanya kusudi ili upate deni basi utahesabiwa kuwa ndoa yako ni batiliNa hayo pia ni mawazo yako mahari sio deni na ndio maana haifungi kaa kwa kutulia
Mke anahusika kwa namna au nyingine....kwa hiyo harassment ni dhahiri kuwa mke yuko upande wa familia yake japo kwa mlango wa nyuma sana.......Mke wake hata hahusiki
Mahari ni nature ?Nature iheshimiwe
Hiyo mahari imetolewa na kupokelea kimila sasa kwa mujibu wa mila mwanamke hahusiki kwenye kupanga mahari.Mke anahusika kwa namna au nyingine....kwa hiyo harassment ni dhahiri kuwa mke yuko upande wa familia yake japo kwa mlango wa nyuma sana.......
Hakuna mwanamke aliyekupenda na kuamua kuolewa na wewe akataja mahari kubwa kiasi hicho hata kama anajua kuwa uwezo wa kulipa unao!!!!
Mahari sidhani kama ni jambo la lazima au la gharama kwa mujibu dini ni kama tu zawadi anayopewa mwanamke na mumewe kwa heshima ya kuolewa na yeye....na ndio maana wengine Wanataka msahafu tu...... wengine mkufu wa dhahabu...... wengine hata gauni zuri.......na sio fedha au mavitu ya gharama.......Baba yangu hakuchukua mahari kwa dada yangu na Mimi nimepanga kutochukua mahari wakiolewa be watoto wangu wa kike.
Sipendi hii biashara ya kuuza mtoto wangu.
Kama ni kimila sawa......Hiyo mahari imetolewa na kupokelea kimila sasa kwa mujibu wa mila mwanamke hahusiki kwenye kupanga mahari.
Na kwa maelezo ya mleta mada inaonyesha binti ni yatima ndo maana naona hahusiki
Ni imani za kimila, na hizi dini watu wanatumia kama geresha tu ila wengi huoana kimila.Nani kawaambia mahari haitakiwi kuisha ? Ni imani za mtaa au imani za kidini? Kama kwa upande wa Dini kwa waislam mahari ni deni inatakiwa ilipwe haraka sana kabla hujafa na ukifa ukiwa na deni hilo ndugu zako wanatakiwa wakulipie
Kwa nini mahari huwa haiishi??Habari?
Nimeoa tangu 2021 wakaniambia nilipe m 2.7 nikawa nimelipia kama milion moja na sehemu hv, sasa imebaki m 1 lakini hawa bibi zake na wife kila wakikosa ada ya kumlipia mtoto wao au ada ya kulimia wananiijia juu nilipe mahari ambapo na mimi muda huo nakuwa sina hela.
Mi ninavyojua mahari huwa haiishi ambapo unaweza lipa taratibu, haya sasa hivi wamesema wanamuijia mke wangu na watoto dah! Halafu hela sina, je hii ni sahihi? Maana huyo mke wangu kwao ni mjukuu tu ila watoto wao wameolewa bure hata mahari haijatolewa ila mimi huwa najitahidi kutoa kidogo kidogo.
Kwa nini mahari haitakiwi kuisha kulipwa?Mkuu mahari haitakiwi kuisha na wablock wote wasikuzoee
Kwa kuanzia hakuna undugu katika yako na familia ya mke wako, kuna urafiki, mahusianona na kujuana tuMila na desturi za makabila mengi ya kitanzania. Ukimaliza mahari unakuwa kama umeua undugu kati ya hizo familia mbili
Tamaduni za makabila mengi ya kitanzania huacha kiasi fulani kidogo cha mahari ili kutunza ujamaa kati ya familia mbili, maana wakiumwa, wakipata msiba na mambo mengine bado watamshirikisha aliyelipa mahari. Kumaliza mahari hutafsiriwa kama kutotaka ujamaa tena kati ya hizo familia mbali kwani walishapewa kila kitu walichotaka.Kwa nini mahari haitakiwi kuisha kulipwa?
Kama hakuna undugu mdogo wako anaweza kuoa familia moja na wewe ulipooa?Kwa kuanzia jakuna undugu katika yako na familia ya mke wako, kuna urafiki, mahusianona na kujuana tu
Mke anapokea mahari kuipeleka wapi??Kwa mujibu wa kiimani.....niko tayari kusahihishwa.......
Mahari inahesabika ni deni ikiwa muoaji hana uwezo wa kulipa kwa wakati huo anatoa kidogo kati ya kile walichoelewana na kubakia deni ili ndoa ipite.....lakini ikiwa muoaji amekusudia kabisa kutokumaliza hali ya kuwa uwezo wa kufanya hivyo anao basi hapo atahesabika amefanya utapeli na hiyo ndoa itakuwa batili........
Lakini pia nadhani anayetakiwa kudai mahari ni mke kwa kuwa mke ndio mwenye kupokea mahari sasa inakuwaje wazazi wanakuwa mbele kwenye hili.....
Vipi hao mke na mume wakiachana? Undugu wa wa hizo familia bado utaendelea?Tamaduni za makabila mengi ya kitanzania huacha kiasi fulani kidogo cha mahari ili kutunza ujamaa kati ya familia mbili, maana wakiumwa, wakipata msiba na mambo mengine bado watamshirikisha aliyelipa mahari. Kumaliza mahari hutafsiriwa kama kutotaka ujamaa tena kati ya hizo familia mbali kwani walishapewa kila kitu walichotaka.
Ikumbukwe kua hii si kwa makabila yote ya kitanzania wala haihusiani na taratibu za dini
Ndio, anaweza.Kama hakuna undugu mdogo wako anaweza kuoa familia moja na wewe ulipooa?
Kwanini wewe ukipewa zawadi unaipeleka wapi....??Mke anapokea mahari kuipelekea wapi??