Bibi zake mke wangu wakikosa pesa ya kulipa ada wanaanza kutumia mabavu nilipe mahari

Bibi zake mke wangu wakikosa pesa ya kulipa ada wanaanza kutumia mabavu nilipe mahari

Nimesha mwambia wakaanza kumwambia maneno ya kiseng** tu et umeona mme ndio bora kuliko sisi ndugu zako.
Kiukweli mume anatakiwa kuwa bora kuliko ndugu zako.

Ndugu zako hukuwachagua, umejikuta tu ni ndugu zako.

Mume unatakiwa kuwa umemchagua mwenyewe.

Uliyepata mahusiano kwa kumchagua mwenyewe ni muhimu kuliko hao uliojikuta tu una mahusiano nao kwa ajali ya kibaiolojia.
 
Namimi naona hivyo maana ni kama kesi hivi alafu hata uwaambie sina hela wanalazimisha ulipe, kuna kipindi babu yake alikuja kudai kwa nguvu nikamjibu mi sina hela, siku iyo wife alimpikia akala na nauli ya kumrudisha tukampa hakuja na nauli, nilivyo impa hiyo nauli akaigomea ni ndogo 😂😂😂 . Alivyo fika nyumbani akawaambia hata kula hajala.
Umevamia mtumbwi wa vibwengo
Usipokaza hiyo ndoa itakufa
 
Kiukweli mume anatakiwa kuwa bora kuliko ndugu zako.

Ndugu zako hukuwachagua, umejikuta tu ni ndugu zako.

Mume unatakiwa kuwa umemchagua mwenyewe.

Uliyepata mahusiano kwa kumchagua mwenyewe ni muhimu kuliko hao uliojikuta tu una mahusiano nao kwa ajali ya kibaiolojia.
Ndugu zake wana mambo ya ovyo wameona tumejitafuta wife nikamfungulia duka wakaona kuna hela hapa, maana tunajitafuta tujenge.
 
Hayo mambo ya kusikiliza ndugu ndugu kwenye mahusiano mwambie marufuku, utakuta ndugu wenyewe wote ndoa zilishawashinda.
Kabisa na huwa nakaa naongea nae na analijua hilo.
 
Ndugu zake wana mambo ya ovyo wameona tumejitafuta wife nikamfungulia duka wakaona kuna hela hapa, maana tunajitafuta tujenge.
Ndugu kama hao unatakiwa kuwajulisha mapema kabisa kuwa wewe ni mnyambilis wasikuzoee zoee vibaya.
 
Na wewe jamaa ulikubalije kutoa mahali nyingi kiasi hicho wakati wewe mwenyewe maisha yako ya kuunga UNGA tu ya min -me

Siku hizi mahali ikizidi sana laki 4-7 sasa wewe unatoaje mahali ya 2.7 million?

Mimi naona ubaya uliuanza wewe
 
We hujui tu kulikuwa na baba yangu mdogo ndio alienda kubagain mahali sijui nayeye alikuwa ananikomesha akawakubalia milion 3 kwanza hiyo m 2.7 niliona niongee nao mwenyewe kuwa hela waliyo niwekea nikubwa ndio nikashusha.

Ila kuhusu maisha uwezo wa kula na kuishi ninao kaka, ila inshort mahali ni kubwa.
 
Ndoa kama ilikua ni ya kimila sawa ila kama ni ya kidini anatakiwa amalize mahari vinginevyo ni utapeli kama utapeli mwingine
Kwa mujibu wa kiimani.....niko tayari kusahihishwa.......
Mahari inahesabika ni deni ikiwa muoaji hana uwezo wa kulipa kwa wakati huo anatoa kidogo kati ya kile walichoelewana na kubakia deni ili ndoa ipite.....lakini ikiwa muoaji amekusudia kabisa kutokumaliza hali ya kuwa uwezo wa kufanya hivyo anao basi hapo atahesabika amefanya utapeli na hiyo ndoa itakuwa batili........

Lakini pia nadhani anayetakiwa kudai mahari ni mke kwa kuwa mke ndio mwenye kupokea mahari sasa inakuwaje wazazi wanakuwa mbele kwenye hili.....
 
Back
Top Bottom