Bible Vs Science: Je ulimwengu una umri gani?


Uligusia kuhusu suala la elimu na manufaa,sasa nimekuonyesha ya kuwa zipo elimi zisizo na manufaa.

Inaonekana ulikuwa hujui kama Uchawi nayo ni elimu.
 

Ubongo wangu uko salama salimini Master !

Unapokea ya haki na unayatupilia mbali ya batili.

Nipo ....!
 
Uligusia kuhusu suala la elimu na manufaa,sasa nimekuonyesha ya kuwa zipo elimi zisizo na manufaa.

Inaonekana ulikuwa hujui kama Uchawi nayo ni elimu.
ukisoma dictionary yeyote kigezo cha kwanza knowledge lazima iwe ni fact... kwa kigezo icho kwangu sioni kama uchawi ni knowlege
 
Hatukuangalii wewe sisi tuna angalia ukweli ulivyo.

Sasa kuanzia leo unatakiwa kusafisha ufahamu wako juu ya UCHAWI.

Nipo ....!
Watu hatuko sawa, ndio maana kuna wengine rangi nyekundu wanaona kijani na kijani ndio fact kwa upande wao....
 
Biblia haisemi chochote juu ya umri wa Dunia ila imetaja kuwepo kwa maji, uumbaji wa mimea na watu
Mimi ni mjiolojia na ningependa kuchangia kwa perspective ya kisayansi hasa tulivyofundishwa na kusoma paper na vitabu mbalimbali za kijiolojia

Kuna dhana mbili za evolution ambazo ndizo zinazoelea juu ya umri wa dunia
Dhana ya Organic evolution na Crustal Evolution
Hii ya Crustal evolution ndio hasa itaelezea vizuri umri wa dunia
Katika Crustal evolution inaanzia kwenye kuumbwa kwa dunia ambako kuna theories nyingi sana zinazoelezea juu ya kuumbwa kwa Ulimwengu (dunia ikiwemo) yaani The Creation of the Universe
Theory iliyoungwa mkono na wanasayansi wengi kwa sababu inaweza kufanyiwa majaribio ya kifizikia kwenye maabara ni ile ya Galaxy Theory ambayo inadai kulikuwepo na vumbi kubwa kwenye space na hilo vumbi ilikuwa na composition kubwa ya Hydrogen, Oxygen, Nitrogen, Iron, Nikel na aina zinginezo. Hili vumbi linaaminika kujikusanya taratibu takribani miaka bilioni 13/14 iliyopita na ilipotimu miaka bilioni 4.5 iliyopita hilo vumbi likaanza kujizungusha yenyewe kwa kasi kubwa na kutengeneza nguvu mbili za uvutano yaani Centrifugal force (nguvu inayosukuma mada kwenda mbali na katikati ya mzunguko) na centripetal force (Nguvu inayovuta mada kwenda katikati ya mzunguko). Vumbi hili ilipozunguka ikazidiwa na kuanza kukatika na kuzaa mikia ambayo ndiyo sayari zinazoizunguka Jua. Kiini cha katikati la hilo vumbi ndio Jua ambalo imezishikilia hizo sayari zote zilizomeguka wakati vumbi hilo linajizungusha kwa kasi. Umri wa kila sayari uanweza kutofautiana kwa sababu hazikumeguka kwa wakati mmoja
Mwezi ulitumika kupima umri wa Dunia kwa sababu ndio miamba inayopimika ambayo iko karibu na Dunia na kwa hiyo umri wa mwezi ni sawa na umri wa dunia kwa makadirio.
Vipimo vilivyopimwa kwenye miamba kutoka mwezini zinaonyesha kuwa ina miaka kati ya 4.4 mpaka 4.5 billion. Hii imefanyika kwa sababu kupata sample sahihi katika uso wa dunia ni ngumu kwa sababu miamba mingi yamefunikwa wakati miamba ya mwezini hayajafunikwa. Kipimio cha Radiometric Dating ndio inayoweza kuleta usahihi wa vipimo kwa sabau inatumia half-life concept ambayo inaleta majibu consistence kila inapotumika
 
Hiko kipimo ndo kilisema binadamu wa kwanza aliishi miaka milioni 3?
 

Kaka Hakuna mtu anayekataa kuwa Mungu hakuumba vitu vyote, unajua Kitabu cha Mwanzo ukikisoma vizuri kina kila kitu unachokiitaji kwenye hii Dunia, Kuna sayansi kubwa sana pale, kuna elimu nzito kabisa
sasa twende polepole
Mwanzo 1:1-2 Mungu alifanya nini?
1. Aliumba mbingu na nchi (Ardhi)
2.Nchi ilikuwa Giza, ukiwa na utupu
3. kulikuwa pia na vilindi vya maji
so hivyo vyote viliumbwa nje ya zile siku sita, je baada ya kuumbwa hivi vilikaa siku ngapi kabla ya zile siku sita ?

umetoa andiko la Kutoka 20:11, ni kweli ndani ya siku SITA mUNGU ALIUMBA BAHARI kwa kutenganisha maji na ardhi, Mwanzo 1:6 Mungu akasema na liwe anga katikati ya maji LIKAYATENGE MAJI NA MAJI, Mwanzo 1:9 naMaji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja ili pakavu paonekane.........

Kaka mitale na midimu ,
maandiko yote ya kuanzia Mwanzo 1.3-10 kitu kipya alichokiumba mungu kutoka vile vilivyokuwa awali Mwanzo 1:1-2 ni NURU pekee, lakini vingine kama Maji , Nchi, Giza alishaviumba kabla
Baada ya Mungu kukamilisha kuitransform Dunia iwe na mazingira ya kusupport uhai ndio kuanzia Mwanzo 1:11 na kuendelea anaanza kuweka Mimea na viumbe hai

MIMI NINACHOAMINI MUNGU ALIIUMBA DUNIA MIAMBA NA MAJI NA ILIKUWEPO KWA MUDA MREFU SANA, KISHA AKAPANGA MIPANGO YA KUWEKA VIUMBE HAI, LAKINI ILIBIDI LAZIMA AANDAE MAZINGIRA YA KUWAWEZESHA HAO VIUMBE HAI NA MIMEA IWEZE KUKUA NA KUSTAWI KWA UZURI, NDIO SASA MUNGU NDANI YA SIKU SITA ANAITRANSFORM DUNIA NA KUIPA MAZINGIRA YA KUWEZA KUTUNZA VITU HIVYO VYOTE

KITABU CHA MWANZO NI KITABU KIZURI SANA, NDIO MWANZO WA DUNIA NA NDIO MWANZO WA SAYANSI
 
Hiko kipimo ndo kilisema binadamu wa kwanza aliishi miaka milioni 3?
Mkuu unachotakiwa kujua methodology inafuata principles mfano inafahamika kuwa layer moja inabadilika kuingia layer ingine baada ya muda fulani unaoitwa half life lets say kutoka half life ya layer moja kwenda ingine inachukua miaka million 50 sasa si utahesabu tu layer zipo ngapi na utapata jibu na ndio maana hizo tafiti zao zinakubalika na wasomi ssa nyie mkiletewa mnapinga bila kuuliza methodology kisa tu imani zenu hazikubaliani na hilo. Ila cha kushangaza wanasayansi hao hao wakitoa tafiti mfano kuthibitisha Yesu/Issa au Mfalme Daudi waliwahi exist basi tafiti zao mnazikubali.

Tuache double standards tafiti hujibiwa kwa tafiti tafuta mfumo mwingine hesabu umr wa hiyo miamba ukipata no below 6000 ndio object ila kama hakuna mfumo mwingine credible zaidi kwanini mnapinga bila alternative?? Maana jibu lako lipo sarcastic sana
 

Dhana ya siku SITA tuliyo nayo sio ile iliyomaanishwa na Waebrania wakati ule. Jaribu kuangalia Istilahi "YOM" (neno la Kiebrania lenye maana ya Sita) linabeba maana gani. Ndio Waebrania waliposema Sita walikuwa na maana gani? Namba hiyo ina maana ya picha kumaanisha MUDA MREFU.Kwa mfano,mimi nikisema nina Watoto "KIBAO". Haimaanishi kwamba nina watoto wanaoitwa Kibao Bali wengi. Kwa hiyo,kwa Waebrani kila namba ilikuwa na maana yake.
 

Ukisoma biblia utagundua kulikuwa na maangamizi kabla ya maangamizi ya noah
Af biblia inaongelea historia ua binadam tuu na si vinginevyo
 
Kingine ni wanascience wanasema binadam alianza kutokea kama zinjathropus miaka laki2 iliopita
Homosapien(moden man) alitokea miaka elf50 iliyopita
 
Ila cha kushangaza wanasayansi hao hao wakitoa tafiti mfano kuthibitisha Yesu/Issa au Mfalme Daudi waliwahi exist basi tafiti zao mnazikubali.

Tatizo kuna wakristu wana mtizamo kama Wa Kiislamu kwamba Biblia ilipatikana kama Kurani inavyodaiwa kupatikana!

Biblia ni neno la Mungu kwa mtizamo kwamba tu Yale maudhui ni divinely authored. Lakini Lugha, Staili ya Uandishi, Utamaduni, ni vitu vya kiuandishi tu. Mungu hakuwa ana-detect uandishi wa neno kwa neno. Kwa Mfano, Magufuli akimuagiza Msigwa atoe press Release atamueleza mambo ya ku-communicate lakini Lugha na misamiati vitakuwa vya Msigwa mwenyewe na Release ile itaitwa ya Ikulu au Ujumbe Wa Raisi.
 
Mada yako ilipo anza ulikataa maswala ya udini lakini wewe umeleta udini hiyo sehemu apo ya 500 baada ya Yesu hapo a yupo mtume Muhammad lakini hujaandika umeacha wazi
 
"Uchawi" upi ni Elimu? Unaelewa maana ya Elimu? Kunyofoa viungo vya Albino ni Elimu? Kupasulia Nazi kwenye Kaburi nako ni Elimu?

Tuliza kichwa,nilicho kiona humu watu wanajadili mambo ya kielimu bila kujua elimu ni nini ?

Naendelea...

1. Kusonga ugali elimu au sio elimu ?

2. Kuendesha gari ni elimu au si elimu ?

3. Kusimama kwenye zebra kwa mwenye kupisha wavukaji wa miguu ni elimu sio elimu ?

4. Kula ni elimu au sio elimu ?

5. Kuruka kamba elimu au sio elimu ?

Nipo....
 
Mada yako ilipo anza ulikataa maswala ya udini lakini wewe umeleta udini hiyo sehemu apo ya 500 baada ya Yesu hapo a yupo mtume Muhammad lakini hujaandika umeacha wazi
Tofautisha udini na historia..... Udini naopinga ni ule kuja na kukashifu dini za watu mfano kusema Biblia ni feki au Mtume sijui alitokewa na mapepo sio malaika n.k hayo ndio udini ila sijakataza kuongelea viongozi wa hizo dini kwa minajili ya kujengea hoja tu na sio kuwakashifu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…