Umetafuta backing kwenye maandiko ya biblia ukagonga mwamba, endelea na upotevu wako bibie......ila kuwa makini kupotosha watu wengine maana utawabebea adhabu zao.
Wewe nawe mzito sana kuelewa...... sijui ilikuchukua muda gani kujua kusoma na kuandika🙄
Haya soma tena kwa ufahamu👇
Katika maandiko matakatifu kuna mafundisho, maagizo na unabii
Kwa mafundisho tunajifunza, kwa maagizo au amri tunatekeleza na unabii unatimizwa
Sababu ya Mungu kutuleta duniani ni kuja kutimiza kazi zake. Kila mtu ni mtume wa Mungu kwa nafasi yake, na tukifuata Mungu alichotutuma kwa kuisikiliza sauti ya tutatimiza hata unabii uliowahi tabiriwa. Hata wewe hapo ulipo unaweza kukuta unatimiza unabii either kwa kujua au kutokujua
Kwa kuuwasha mwenge Nyerere alikua anatimiza unabii ulioandikwa kwamba
Isaya 9: 2
Watu wale waliokwenda katika giza Wameona nuru kuu; Wale waliokaa katika nchi ya uvuli wa mauti, Nuru imewaangaza.
Tukumbuke wakoloni waliotutawala waliwekeza sana Kilimanjaro kwenye huduma za kijamii kama mashule, mahospitali, mahoteli, kilimo, makanisa...... Nyerere hakuishia kuwasha tuu mwenge kama tendo la imani. Bali aliweza kuisambaza ile nuru kutoka Kilimanjaro kwa kuhakikisha vijana wa ule mkoa wanasambazwa nchi nzima ili kueneza kile walichokua nacho kupitia mashule na ajira. Na hii ilisaidia sana kuvunja ukabila, matabaka na kuleta upendo na umoja.
Huo ndio unabii wa mwenge wa uhuru
Mwenge wa Tanzania haukuwashwa ili utumike kama silaha au uabudiwe, bali uliwashwa kama tendo la imani katika kuleta nuru na matumani kwa nchi yetu na majirani
2Petro 1: 19 - 20
Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing'aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.
Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.
Nyumisi Kiranja Mkuu NA WENZENU tafuteni maada zenye faida na maslahi ya nchi yetu tujadili
Punguzeni povu maana ni kama mwenge unawachoma hadi kumoyo
MWENGE ni object inayotumika kuamsha ari za watanzania kama KENGELE inavyotumia makanisani na ADHANA inavyotumika miskitini
Usiendeele kuumia maana tumekwisha uwasha mwenge😅😅😅