Biblia ndio kitabu pekee kinachojibu maswali Mengi kumuhusu binadamu na maisha yake

umempa majibu Mazuri Sana.
Usimuamshe aliye lala.

Agenda ya LGBT hajiulizi nyuma yake aliweka pesa zake ni Nani.

Mashoga na wasagaji nani anawapa pesa za kufanya mambo yao.

Then kuna kiwanda cha kufyatua watoto,
mwanamke haitaji tena kubeba mimba, napeleka mbegu na yai, then mnafata mtoto.

Ukijumlisha na Aliens viumbe wa sayari nyingine nao watakuja kwenye hii planet yetu.

Nimepata Ushaidi ya kibiblia kuonesha kabla ya Adamu kuumbwa, kuna viumbe wengine waliishi hapa dunia kabla.

na ndio hao wanasaidia kukuza Technologia ya duniani.

Sasa piga picha,
hao watoto wa mitambo na hizo Alien zikiungana kuna mtu atakua salama hapa dunian, zikisema sisi nichakula chao tutabisha ??? 🤣🤣🤣
 
True..na biblia inakuelezea kila kitu, lakini kama hauelewi, ni hauelewi.

Mungu anasikitika kuona mwanadamu anaangamia kwa kukosa maarifa, kwa sababu inasikitisha na kuumiza sana.

People dont know anything...and they love knowing shit that leads to nothing.

Sent from my SM-A310F using JamiiForums mobile app
 
Nafsi ndio inabeba Akili
Mwili hauwezi kubeba akili.

Bali unabeba Memory (kumbukumbu) tu.
na kumbukumbu hizo hukaa kwenye ubongo na kwenye Moyo.

Sababu:
Katika Kula chakula bora..
Utakua na kumbukumbu nzuri na utaweza kukumbuka mengi.

Lakini kula vizuri hakukupi Akili ndugu.
Akili ni Kama Wisdom tunapata kwa kupewa na aliyetuumba kwa kusikia neno lake na kujua hekima yake.
 
Mungu mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele Alishindwaje kuumba binadamu ambao hawato angamia?

Badala yake aliumba binadamu wanaoweza kuangamia na kuanza kusikitika?

Ina onekana kwamba Mungu Hajui yote, kama anajua yote kwa nini aliumba binadamu ambaye ana msikitisha?

Alishindwaje kuumba binadamu ambaye atamfurahisha milele?
 
Wakati unaendelea kubishana hapa wapo wengine wana access maisha ya ulimwengu wa roho wakiwa hapahapa duniani,

Watu gani hao?
Lete ushahidi usio na shaka?
Ngoja na mimi nichangie kidogo.

Wanadamu ni sawa na pande mbili za shilingi.

Tunaonekana tuko sawa kwa kila kitu(utu),Lakini kila mtu ana upande wake ,mwonekano wake, tabia yake, ufahamu wake, maono yake n.k.

Si kila mwanadamu aliye mbele yako ni sawa na wewe.

Unataka ushahidi usio na shaka. Mungu ni roho huwezi kuiprint ikaonekana.

Wewe una roho.Je unaweza kutuonyesha jinsi inavyofanana?

Unahitaji kujua watu wenye access na ulimwengu wa roho.

1.Wachawi na wote wanaotumia nguvu za giza.

2.Watumishi wa Mungu wa kweli na watu wote walio katika ulimwengu wa nuru.

Ukitaka kuujua huu ulimwengu wa nuru na giza unafanyaje kazi tafuta watu wa haya makundi watakusaidia kuujua zaidi.

Ninaposema pande mbili za shilingi, namaanisha kuwa kuna watu hawajui chochote kinachohusu ulimwengu wa roho na kuna wengine wanaujua na kuutumia ulimwengu wa roho kiufasaha.

Vyote hivi utavijua ikiwa una IMANI haijalishi ni ya namna gani, utachagua ni imani ipi,ya gizani au nuruni. Na huwezi kumjua Mungu kama huna imani.
 
Unataka ushahidi usio na shaka. Mungu ni roho huwezi kuiprint ikaonekana.

Wewe una roho.Je unaweza kutuonyesha jinsi inavyofanana

Nimekunukuu hapo juu
Na tuumbe mtu kwa mfano wetu.
Binadamu aliye umbwa aliumbwa nafsi au mwili tu?

Kama iliumbwa nafsi tu nitakubaliana nawe Mungu ni nafsi, ila binadamu alianza kuumbwa mwili kitu kinachoonyesha hata huyo mumdhaniaye ni mwili.

Aliyesema ni nafsi mmeitoa kwenye chanzo kipi?

Mimi Sina roho na ni myth isiyo na mashiko toka ngano za kale za Wahenga.

Roho ni nini?
Usije sema ni pumzi maana tunajua ilipotokea na jinsi inavyokuwa created na mwili hasa Respiratory system.
 
Kwahiyo hapa ninazungumza na kiumbe kingine ambacho si mwanadamu?
 
Okay. Chanzo cha nafsi.

Mwanzo:2:7

BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai;mtu akawa nafsi hai.
 
Kwanza unakosea sana kuwa mjinga. Na kama unajua alafu unatoa hoja dhaifu hizi, basi huu ni upumbavu. Na hata Mungu mwenyewe hawezi ku tolerate watu wapumbavu.

Pili, hauwezi kuujua ukuu wa Mungu (umilele) kwa akili za kimwili zinazoharibika. Fikra zako ni za kimwili, za akili inayoharibika, na si za milele...so chochote kile utakachofikiri hakiwezi kufikia umilele wa Mungu...sanasana unaonekana Boya....ndio maana wenye imani wanakuambia kwa lugha nyepesi kuwa unakufuru.

Tatu, mwanadamu haharibiki, kinachoharibika kwa mwanadamu ni vazi lake la nje, ambalo ndio udongo.

Ujinga ni pale unaona hilo vazi lako (mwili) kuwa ndio kila kitu, wakati hilo vazi ni la hapa tuu duniani, au mars, au kwenye ulimwengu huu tuu unaoonekana, ila vazi la mbinguni haulijui, maana lipo, vazi la motoni lipo, na haulijui, na hata kama kuna vazi la ulimwengu mwingine tofauti na hiyo niliotaja kama lipo, maana yake litakuwepo ukibahatika kufika huko.

Alafu, Mungu aliumba viumbe wengine, wasio na vazi la mwili, akaghairi, na mpaka umeumbwa mwanadamu uishi hapa duniani maana yake wewe sio wa kwanza.

Huenda ni wa pili, huenda ni wa saba, huenda ni wa mia tano, hauwezi kujua. Kwa sababu mwanadamu sio wa milele

Ukweli usioujua ni kuwa mwanadamu atapata maisha ya milele endapo akiacha vazi la mwili na kwenda kupata vazi la kiroho.

Sasa hapa ni suala la wewe kujua.

Lakini ukibishia sana hili na kudhania kuwa hakuna ulimwengu wa roho, basi ukifa (ukiliacha vazi la dunia hii utapotelea kusikojulikana, au kwa lugha ya biblia, utakufa.

Ila ukijua maisha ya ulimwengu wa roho, utaendelea kuishi milele

NB: Midhambi ndio inayomsikitisha Mungu, na midhambi ni matendo yako wewe mwanadamu. Unaambiwa ufanye mema, alafu unatenda dhambi, unadhani unataka Mungu akuendeshe kama rimoti.

Kama ushawahi kufundisha timu ya mpira utakua unaelewa...umefundisha timu imeiva, wanaingia uwanjani kucheza wanapigwa nne bila, watu wanajichezea wanavyotaka na unawafundisha kabisaa wacheze mfumo huu wao wanaenda kujichezea hovhovo..utajihisije?

Hivyo ndio Mungu anahisi kwako unapomkosea.

Na mwanadamu anaangamia kwa kukosa maarifa..na Biblia ilishasemaga..so..[emoji88][emoji88]
 
Pili, hauwezi kuujua ukuu wa Mungu (umilele) kwa akili za kimwili zinazoharibika. Fikra zako ni za kimwili, za akili inayoharibika, na si za milele...so chochote kile utakachofikiri hakiwezi kufikia umilele wa Mungu...sanasana unaonekana Boya....ndio maana wenye imani wanakuambia kwa lugha nyepesi kuwa unakufuru.

Kama yeye hawezi kwa kutumia fikra za kimwili na akili wewe umetumia nini kugundua?

Umilele wa Mungu umejuaje?
Maana pia unatumia fikra na akili za Mwanadamu awe ndugu yetu ni malaika
 
Wewe ni mwanadamu au kiumbe kingine?
Mimi natoka kwenye:
Kingdom: Animalia

Multicellular organisms; cells with a nucleus, with cell membranes but lacking cell walls

Phylum: Chordata

Animals with a spinal cord

Class: Mammalia

Warm-blooded chordates that bear live young; females have mammary glands that secrete milk to nourish young

Order: Primates

Mammals with collar bone; eyes face forward; grasping hands with fingers; two types of teeth (incisors and molars)

Family: Hominidae
Primates with upright posture, large brain, stereoscopic vision, flat face, different use of hands and feet

Genus: Homo
Hominids with S-curved spine, recognisable as human

Species: Homo sapiens
Humans with high forehead, well-developed chin, thin skull bones
 
Sijakuelewa. Mimi sikubahatika kwenda shule,mjadala ulikuwa kwa Kiswahili ingekuwa vizuri ungetumia lugha ninayoilewa.

Sifa mojawapo ya Lugha kama haieleweki kwa msikilizaji huwa haina maana.

Ulichokiandika hakijaleta maana yoyote kwangu.
Ahsante.
 
Unataka mchakato wote wa uumbaji?
Mwanzo:2:7

BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai;mtu akawa nafsi hai.

Nimeqoute mstari wako
Ndio nimeuliza kipi kilianza kwa kutumia huu mstari
 
Kwani shetani wafuasi wake hawamwabudu?

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…