Umesoma ndugu.
Kuna Mambo mengi ya kujifunza kwenye historia ya Mahusiano ya Mungu na Mwanadamu.
Utawala ni Siasa inayohusisha Nguvu za kiroho.
Ndio maana wengi wanasema kushinda uongozi kwa maneno tu sio rahis, lazima kuwe na nguvu fulani nyuma yako.
Huwezi elewa dunia inakwendaje bila kutafuta uelewa wa mambo ya rohoni na nguvu za kiroho.
Wasiojua wanaachwa wasijue maana wataleta vurugu kwa wanaojua, na wasiojua siku zote wapo wengi[emoji3][emoji3]
Na wanaojua siku zote huwa wachache na wanaendelea kujua zaidi na kutumia elimu hii kunufaika na kufika mbali zaidi na zaidi...
That's the law. Of nature.
Unadhani watu ni wajinga wanapopiga kampeni ya uchaguzi na kuzunguka maeneo yote ya nchi nzima? Kila jimbo, kila utawala?
Sipendelei siasa, ila Ndio maana nawaambiaga wanasiasa kuwa Upinzani hapa nchini haitokaa itawale nchi hata kidogo kwa sababu they're too weak on almost everything.
Wanataka kujua lakini at the same time hawataki kujua.
Chama tawala kinawatazama tuu, na kuwanyamazia kimya...kimetega mitego mingi sana na masimiko mengi mno ya kuitawala nchi milele, na hakuna hata chama, au serikali au nchi ingine inayoweza kutikisa chama tawala nchini...hata marekani wenyewe. (Rejelea kipindi cha Magu, mambo aliyoyafanya kibabe na nchi zingine, na kila mtu alimtii, kuitisha mkutano wa nchi masikini kusema ni matajiri, kumuita yule kigogo wa madini ikulu, kuichomolea nje korona, na kadhalika.)
Serikali ya Tanzania nadhani ipo vizuri na fit mno katika kuilinda na kuitunza jamii yake kuliko serikali ingine yoyote ile duniani kwa sasa...na pia inafulea watanzania kama watoto wadogo yaani..tunadekadeka tuu ujinga
Hata marekani wenyewe wapo so vulnerable kuliko Tanzania. Na hii yote tunamshukuru sana Nyerere aliyoyafanya..baba wa taifa was a little genius, mjanja, na sawa na malaika wa kisiasa kwa ajili ya eneo lake la kazi ambalo ni Tanzania.
Kama hauwezi kuelewa, usijali. Kajifunze, ukiwa sawa ndio uje usome tena hii post.[emoji2][emoji2]