Biblia ni nini? Maelezo ya kina kuhusu kitabu hiki ambacho shetani anakichukia kuliko vitabu vyote!

Huko kwa Yesu tumeshatoka na Sirudii tens Huko
 
Mjadala umekuwa mzuri:
Tulioufuatilia tumejifunza mambo mengi:
Ahsanteni wote mlioshiriki kikamilifu:
 
Davidmmarista
Huu uzi nafikiri ulikupita
HUU UNAJIBU DUKUDUKU ZAKO ZOTE ULIZOANDIKA KWENYE UZI WAKO
 
Ni hadithi zilizotungwa na watu na wakaziita "kitabu cha Mungu"
 
Natamani Mtu aniambie Shetani alisema uongo Sehemu gani maana Umeandika Uongo wa shetani Miss Hebu niambie na Mimi lro niujue uongo wa shetani
Maandiko yanayoonyesha uongo wa shetani ni mengi sana. Ukisoma kuanzia kitabu cha Mwanzo utayaona.
Isitoshe, shetani anawatumia pia watu kusema uongo. Kumbuka yale maneno aliyosema Petro, kisha Yesu akamwambia "rudi nyuma yangu shetani"
Hapo shetani alitumia kinywa cha Petro, kama ambavyo hata leo watu wanatumiwa na shetani kuipinga Biblia
 
Kama unaijua Biblia ya vitabu 66 tuu Basi unasafari ndefu Sana Mkuu
Kwa level ya Elimu naweza kusema upo shule ya msingi.
Ndugu yangu, nafikiri somo la historia ya Kanisa lilikupita. Tafuta muda ubukue somo hilo ujifunze Canonization Process. Biblia yenye vitabu 66 inatambuliwa duniani kote na makanisa ya Kiprotestanti na Kiinjili. Inajumuisha vitabu 39 vya Agano la Kale na vitabu 27 vya Agano jipya. Hii ndiyo Biblia ninayoiamini mimi. Najua Kanisa Katoliki lina vitabu 73 (vikijumuisha vitabu 7 vya Deuterokanoniko/Apokrifa) na Waorthodoksi wa Ethiopia wana vitabu 81. Tofauti hii si ya 'kiwango cha shule,' bali ni ya misingi ya kihistoria na kidoktrini ya kila dhehebu.
 
Mdogo wangu unajua vitu vingi, lakini Biblia kama Kitabu cha Mungu haikupaswa kutetewa kiasi hiki ilitakiwa isiwe na contradiction kabisa yani iwe imenyooka na wala isihitaji tafsiri
 
Biblia ni maelezo ya watu juu ya mambo mbalimbali,watu hao wakati mwingine humnukuu 'Mungu' au yesu,hakuna maneno ya Mungu kwenye biblia wala biblia si neno la Mungu
Ndugu, ulichosema kinakosa muktadha mzima wa Maandiko Matakatifu. Wasomi wa theolojia wanajua kuwa Biblia asili yake ni Mungu aliyewaongoza watu kusema ukweli wake. Ukiondoa sauti ya Mungu iliyowaongoza waandishi hao, huwezi kuelezea jinsi vitabu 66 vilivyoandikwa na watu tofauti takriban 40, kwa kipindi cha miaka 1,500, halafu vikabaki na ujumbe mmoja wa kiimani unaoshikamana bila kupingana.

Inaonekana pia hujasoma kwa makini mada yote.
Hiyo hoja yako kwamba hakuna maneno ya Mungu kwenye Biblia sio sahihi kihistoria na kitheolojia. Biblia ina maeneo mengi yenye nukuu za moja kwa moja (direct dictation) ambapo Mungu anazungumza katika nafsi ya kwanza (kwa mfano Amri 10 au Sauti kutoka mbinguni). Agano Jipya pia limejaa maneno ya moja kwa moja ya Yesu (ambayo kwenye Biblia kadhaa huchapishwa kwa wino mwekundu). Kumbuka Mungu hakushusha Biblia kwa kamba kutoka mbinguni; alizungumza na wanadamu, na wanadamu hao wakarekodi maneno hayo yaliyotoka kinywani mwake.
 
Mdogo wangu unajua vitu vingi, lakini Biblia kama Kitabu cha Mungu haikupaswa kutetewa kiasi hiki ilitakiwa isiwe na contradiction kabisa yani iwe imenyooka na wala isihitaji tafsiri
Mbona mada imeeleza vizuri kuhusu hizo unazoziita "contradiction." Soma tena mada kwa utulivu.
Halafu kama Biblia isingekuwa kitabu cha Mungu isingepingwa kiasi kikubwa hivi kama unavyoona mada za kuipinga Biblia zilivyo nyingi. Na nimeeleza kwnye mada kwanini shetani anawatumia watu kuipinga.

Sasa mojawapo ya kazi zangu mimi ni kumpinga shetani kila anapojitokeza kujaribu kupotosha ukweli.
Yak 4:7-10
"Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi."
 
Hebu anza wewe kuthibitisha kama Yesu alifufuka!
Mapepo na wachawi wanakimbia kwa Jina la Yesu. Kila wanaponiijia huwa nawafukuza kwa Jina la Yesu na wanatii amri.
Huo ni uthibitisho kuwa Yesu yuko hai. Mtu aliyekufa uliona wapi jina lake likawa tishio?
Soma hapa kwa maelezo zaidi
 
Yote ni mahangaiko ya binadamu katika kutafuta riziki!elimu zote ni mahangaiko ya kutafuta riziki!
 
Yote ni mahangaiko ya binadamu katika kutafuta riziki!elimu zote ni mahangaiko ya kutafuta riziki!
Kuna watu wakiamka hawawazi watakula nini wala watakunywa nini kwa sababu wana pesa za kumwaga!
Unafikiri hao wakisoma Biblia lengo lao ni kutafuta riziki?
Mimi naisoma Biblia ili nijue jinsi ya kuishi matakatifu ili siku Yesu akija niwe miongoni mwao watakaonyakuliwa.
 
Pole kwa kujaza confusions kichwani,biblia ni maneno ya watu na si ya Mungu,watu wenyewe wala hawakumsikia Mungu akisema hayo maneno maana hawakuwa manabii
Hata hiyo injili imeandikwa miaka 70-100 baada ya yesu kuondoka,waandishi wala hawakuwahi kumuona yesu,ni fasihi simulizi tu
 
Muongo unayejiamini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…