Biblia ni nini? Maelezo ya kina kuhusu kitabu hiki ambacho shetani anakichukia kuliko vitabu vyote!

Biblia ni nini? Maelezo ya kina kuhusu kitabu hiki ambacho shetani anakichukia kuliko vitabu vyote!

Vitabu vya Apokrifa ni "hekaya za Abunuwas." Visome tu kama unao muda wa kupoteza
Sorry, hizo unazoita hekaya zina tofauti gani na hizo zilizopo kwenye kitabu chako?

Unajua hata Bible ilipatikanaje? Unajua Laws of Canon zilipatikanaje? Unajua hata Aprokrifa ni nini au Pseudepigrapha?

Unajua kuna Pseudepigrapha ngapi kwenye Biblia ya sasa?

Je, Biblia ya sasa ina mwandishi yeyote ambaye ni claimed authentic, au wote ni attributed authors?

Kazi uliyouchagua kutetea ni ngumu sana...

Natamani nitenge muda ili tupate kuelimishana vizuri kuhusu haya mambo!
 
That's an unprofessional argument (argumentum ad hominem) and completely illogical 😀😀..
Your assertion regarding biblical contradictions demands a rigorous epistemological framework rather than unsubstantiated conjecture. The inquiry into your theological qualifications serves not as an ad hominem fallacy but as a legitimate means of assessing the depth of your exegetical acumen. Dismissing it outright suggests either an evasion of intellectual scrutiny or an inadvertent admission of inadequate expertise. If you truly possess the scholarly aptitude to critique the coherence of Scripture, an articulation of your academic credentials should be a trivial matter rather than a perceived logical misstep.
 
Maneno aliyosema Mungu:
"Na iwe nuru!" (Mwanzo 1:3)
"Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha." (Mwanzo 1:28)
"Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile; kwa maana siku utakapokula, hakika utakufa." (Mwanzo 2:16-17)

Maneno aliyosema Mungu mwenyewe kwa Musa (Amri Kumi)
"Mimi ndimi Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi." (Kutoka 20:2-3)
"Usiue. Usiibe. Usizini. Usitoe ushuhuda wa uongo." (Kutoka 20:13-16)

Maneno ya Mungu kwa Manabii
"Bwana asema hivi, Msihofu, maana mimi ni pamoja nanyi." (Isaya 41:10)
"Mimi ndimi Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi." (Ufunuo 1:8)

Maneno ya Yesu (Mungu Mwana)
"Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi." (Yohana 14:6)
"Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha." (Mathayo 11:28)
"Nanyi mtajua kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru." (Yohana 8:32)

LETA HOJA NYINGINE...
Naomba nitoke nje ya mada kidogo,mimi ni mkristo ila siyo mfia Dini,katika huo mstari wa yohana(14:6)yesu anakiri kweli yeye siyo mungu ila ni mtoto,kwa maana hiyo hiyo yesu ni mteule na mtendaji mkuu katika serikali ya mungu na ndio maana amekuwa na mamlaka ya kusema hakuna mtu atakae enda kwa Baba bila yeye,swali langu linakuja hapa hawa ndugu zetu wa imani ya pili kwa maana ya Waislam inamaana kuwa hawato enda mbinguni kwa kuwa wana mtume wao ambae wanamuamini ambae sisi hatumuni?
 
Sorry, hizo unazoita hekaya zina tofauti gani na hizo zilizopo kwenye kitabu chako?

Unajua hata Bible ilipatikanaje? Unajua Laws of Canon zilipatikanaje? Unajua hata Aprokrifa ni nini au Pseudepigrapha?

Unajua kuna Pseudepigrapha ngapi kwenye Biblia ya sasa?

Je, Biblia ya sasa ina mwandishi yeyote ambaye ni claimed authentic, au wote ni attributed authors?

Kazi uliyouchagua kutetea ni ngumu sana...

Natamani nitenge muda ili tupate kuelimishana vizuri kuhusu haya mambo!
Jibu ni moja tu: ni hekaya kwa sababu hazina pumzi ya Mungu ndio sababu makanisa yote ya kiprotestant yamezipiga chini. Kama wewe uko nje ya makanisa hayo sishangai ukizitumia. Period
 
Your assertion regarding biblical contradictions demands a rigorous epistemological framework rather than unsubstantiated conjecture. The inquiry into your theological qualifications serves not as an ad hominem fallacy but as a legitimate means of assessing the depth of your exegetical acumen. Dismissing it outright suggests either an evasion of intellectual scrutiny or an inadvertent admission of inadequate expertise. If you truly possess the scholarly aptitude to critique the coherence of Scripture, an articulation of your academic credentials should be a trivial matter rather than a perceived logical misstep.
I've already made it clear kwako Kuwa i Have have a theological education and That i am an ex Theologian and that what I write is grounded in both academic qualification and expertise. I am not merely credentialed but I possess the knowledge and analytical depth required for this discussion. So let’s dispense with irrelevant diversions and engage in a substantive debate (if You can) lakini maana Sikulazimishi.

Knowledge is the ability to critically analyze and articulate complex matters with precision, Wapo Niliosoma nao Theology mpaka Leo huwa nawaona bado tukikaa Meza moja wana Yada yada nyingi so Elimu ni kitu kimoja ila Maarida ni kitu kingine, If your objective is truth, then focus on the argument itself rather than attempting to challenge the credentials of the one presenting it.
 
Biblia ni mkusanyiko wa vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi mbalimbali kwa muda wa takriban miaka 1,500, lakini vyote vina ujumbe mmoja unaotuelekeza kwa Mungu na jinsi ya kupata wokovu kwa njia ya Yesu Kristo.

Biblia imegawanyika katika sehemu kuu mbili:
  1. Agano la Kale – Linaeleza uumbaji wa dunia, historia ya Israeli, sheria za Mungu, unabii, na maandiko ya hekima. Linajumuisha vitabu vya Musa (Torati), vitabu vya kihistoria, vitabu vya mashairi na hekima (kama Zaburi, Mithali, na Mhubiri), na vitabu vya manabii.
  2. Agano Jipya – Linaeleza maisha, huduma, kifo, na ufufuo wa Yesu Kristo, pamoja na mafundisho ya mitume. Linajumuisha Injili, Matendo ya Mitume, nyaraka za mitume, na kitabu cha unabii – Ufunuo wa Yohana.
Je, Ni Sahihi Kuiita Biblia "Neno la Mungu"?
Ndiyo, ni sahihi kuiita Biblia Neno la Mungu kama unaelewa maana yake kwa usahihi. Biblia sio kitabu ambacho kila mstari wake ni maneno yaliyotamkwa moja kwa moja na Mungu, bali ni Maandiko yaliyoandikwa kwa uongozi wa Mungu (2 Timotheo 3:16). Ndani ya Biblia tunapata aina mbalimbali za Maandiko:
  1. Maneno ya Mungu Mwenyewe – Mfano, Amri Kumi (Kutoka 20:1-17) na maneno ya Yesu Kristo yaliyonukuliwa katika Injili.
  2. Maneno ya wanadamu waliovuviwa na Mungu – Manabii na mitume kama vile Isaya, Yeremia, na Paulo waliandika kwa kuongozwa na Mungu.
  3. Maneno ya wanadamu wa kawaida– Biblia inanukuu maneno ya watu mbalimbali, hata wale waliompinga Mungu. Mfano:
    • Maneno ya Shetani (Mwanzo 3:1-5, Mathayo 4:3-9) – yameandikwa ili kufunua uongo wake na jinsi Mungu anavyomshinda.
    • Maneno ya Goliathi (1 Samweli 17:8-10) – yanaonyesha kiburi chake kabla ya kushindwa na Daudi.
    • Maneno ya Farao (Kutoka 5:2) – yanadhihirisha ukaidi wake dhidi ya Mungu na jinsi jeshi lake lilivyoangamia.
    • Maneno ya makahaba – Mfano, Rahabu alivyoshuhudia juu ya ukuu wa Mungu wa Israeli (Yoshua 2:9-11).
Kwa nini sasa Biblia Inaitwa Neno la Mungu wakati ina maneno ya Shetani, Goliathi, na watu wengine waovu?
Biblia haielezi aliyoyatamka tu Mungu, bali inasimulia historia, mafundisho, unabii, na hata hila za Shetani kwa lengo la kutoa maarifa na mwongozo kwa wanadamu. Kila kilichoandikwa ndani yake kina sehemu katika mpango wa Mungu wa wokovu. Kwa hiyo, ingawa ndani yake kuna maneno ya waovu, ujumbe wa jumla wa Biblia ni Neno la Mungu kwa sababu unatoa ufunuo wa mpango wake kwa wanadamu.

Kama walioandika Biblia waliongozwa na Mungu, kwanini Biblia ina maneno yanayokinzana (Contradictions)?
Baadhi ya watu hudai kuwa Biblia ina "contradictions." Sababu zinazofanya watu wadai kwamba Biblia ina maneno yanayojipinga ni hizi:
  1. Kutokuelewa muktadha – Maandiko yanapotafsiriwa nje ya muktadha wake, yanaweza kuonekana kama yanakinzana.
  2. Tafsiri tofauti – Lugha za asili (Kiebrania, Kiaramu, na Kiyunani) zina maana za kina ambazo mara nyingine haziwezi kufasiriwa kikamilifu kwa lugha nyingine bila ufafanuzi wa kina. Kwahiyo kama mtu anasoma Biblia kwa lugha ya KIswahili, asipoelewa maana ya maneno fulani anatakiwa achunguze maana halisi ya maneno hayo kutoka kwenye lugha hizo "original" zilizotumika kuandika Biblia.
  3. Mitazamo tofauti ya waandishi – Injili nne(Mathayo, Marko, Luka, na Yohana) zinaelezea maisha ya Yesu kwa mitazamo(perspective) tofauti, lakini ujumbe wao ni mmoja. Yaani, kila mwandishi wa Injili hizo aliandika kwa mtazamo wake (perspective), akilenga wasikilizaji wake maalum na akisisitiza vipengele fulani vya huduma ya Yesu, lakini ujumbe wao wote unakubaliana juu ya ukweli wa Kristo.
  4. Kutompokea Roho Mtakatifu – Biblia inasema kuwa Roho Mtakatifu ndiye anayetufundisha na kututia kwenye kweli yote (Yohana 16:13). Watu wengi wanaodai kuwa Biblia ina makosa hawaongozwi na Roho Mtakatifu, hivyo hawawezi kuelewa maana ya kina ya Maandiko. (1 Wakorintho 2:14: “Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayakubali mambo ya Roho wa Mungu, maana kwake ni upuzi; wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yanatambulikana kwa jinsi ya rohoni.”)
  5. Kupuuza au kutotambua huduma ya ualimu katika Kanisa – Katika kanisa Mungu ameweka wengine kuwa walimu ili kusaidia kueleza na kufafanua Maandiko kwa usahihi. Waefeso 4:11-12 inasema: "Naye ameweka wengine kuwa mitume, wengine manabii, wengine wainjilisti, wengine wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe." Wanaodai kuwa Biblia ina makosa wanapaswa kuwauliza wale waliopewa huduma ya ualimu badala ya kutoa madai yasiyo na msingi. Mungu hajatuacha bila mwongozo, bali amewapa wengine karama ya kufundisha kwa ajili ya kujenga mwili wa Kristo.
  6. Uchambuzi wa juu juu – Wengi wanaosema Biblia ina makosa huwa hawajaisoma kwa kina wala kuitafakari kwa uangalifu. Kama nilivyoeleza katika ponit #5, katika Kanisa kuna Watumishi wenye huduma ya ualimu. Mtu anayeshindwa kuelewa Maandiko fulani anapaswa kuwauliza walimu.
Kwanini Biblia ni ya kuaminika?
  1. Utabiri wake umetimia – Unabii mwingi sana katika Biblia umetimia kwa usahihi, kwa mfano kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
  2. Jinsi ilivyohifadhiwa – Ingawa Biblia iliandikwa kwa maelfu ya miaka iliyopita, maandiko yake yamehifadhiwa kwa usahihi. Nakala kama "Dead Sea Scrolls" zinathibitisha uhalisi wa maandiko ya Agano la Kale.
  3. Athari zake kwa wanadamu – Hakuna kitabu kingine kilichobadilisha maisha ya watu kama Biblia. Mamilioni ya watu wameshuhudia jinsi Neno la Mungu lilivyobadilisha maisha yao. Majambazi wengi wameokoka, makahaba wengi wameacha umalaya, wachawi wameacha uchawi, wenye mapepo wengi wamefunguliwa nk nk baada ya kusikia Neno la Mungu.
  4. Majaribio ya kuiangamiza yameshindwa – Kwa karne nyingi, watawala wamejaribu kupiga marufuku na kuiangamiza Biblia, lakini bado imeendelea kuwepo na kuwa kitabu kinachosomwa zaidi duniani. Hivi sasa Biblia inauzwa kwa wingi huko Marekani
Kwa Nini Shetani Anachukia Biblia?
Shetani anachukia Biblia kwa sababu:
  • Inaonyesha ukweli wa Mungu na kufichua uongo wake – Biblia inafunua mipango yake mibaya.
  • Inawaelekeza watu kwa Yesu Kristo – Shetani hapendi watu wapate wokovu.
  • Ni silaha dhidi yake – Yesu alishinda majaribu ya shetani jangwani kwa kutumia Maandiko (Mathayo 4:1-11).
Biblia ni kitabu cha kipekee ambacho kina ujumbe wa wokovu kwa wanadamu wote. Ingawa ndani yake kuna maneno ya watu waovu, na hata Shetani mwenyewe, maandiko haya yote yamewekwa kwa kusudi la Mungu ili kutufundisha, kutuonya, na kutuelekeza wanadamu katika njia ya wokovu. Kwa hiyo, Biblia kwa ujumla wake ni Neno la Mungu, kwa kuwa ni andiko lililovuviwa na Mungu kwa kusudi lake kuu la kuokoa wanadamu. Badala ya kuitilia shaka, ni muhimu kuisoma, kuitafakari, na kuiishi, kwa kuwa ni nuru au taa katika giza la dunia hii.

Usikubali kupotoshwa na manabii wa uongo kuhusu ukweli wa kitabu hiki "BIBLIA"


You have known the truth, and let it set you free." (John 8:32)
Wewe una huduma ya ualimu kutoka kwa Bwana!
 
Jibu ni moja tu: ni hekaya kwa sababu hazina pumzi ya Mungu ndio sababu makanisa yote ya kiprotestant yamezipiga chini. Kama wewe uko nje ya makanisa hayo sishangai ukizitumia. Period
Huu Ndo utetezi wako?
Duh Bhasi nahisi Bado unasafari Ndefu sana ya Kujifunza Unajua Makanisa ya Kiprotestant yameanza Mwaka gani?

Ndo maana Niliuliza Unafahamu Kuhusu Aprokrifa na Pseudepigrapha...?

Sasa Nimepata Jibu Huna Unalojua Kuhusu Hivyo vitu!

Nilitaka Nikuvishe Mzigo mzito wa Kujibu hoja Ambazo Huna elimu nazo..Nisamehe

Kama Hujui hata what so Called Pumzi ya Mungu (Canon) zilipangwaje kwa sheria zipi basi una safari ndefu sana..

Uwezo wako Ni mdogo sana 😀😀😀

Kwaheri..🤣🤣

Maana Kama hoja Zote nilizokuuliza kwenye Post Jibu lake ni Vitabu vinafuatwa na Protestant 🤣🤣 unasafari ndefu sana
 
Naomba nitoke nje ya mada kidogo,mimi ni mkristo ila siyo mfia Dini,katika huo mstari wa yohana(14:6)yesu anakiri kweli yeye siyo mungu ila ni mtoto,kwa maana hiyo hiyo yesu ni mteule na mtendaji mkuu katika serikali ya mungu na ndio maana amekuwa na mamlaka ya kusema hakuna mtu atakae enda kwa Baba bila yeye,swali langu linakuja hapa hawa ndugu zetu wa imani ya pili kwa maana ya Waislam inamaana kuwa hawato enda mbinguni kwa kuwa wana mtume wao ambae wanamuamini ambae sisi hatumuni?
Amini alichosema Yesu. Isitoshe alisema njia ni nyembamba iendayo uzimani nao waionao ni wachache.
 
Huu Ndo utetezi wako?
Duh Bhasi nahisi Bado unasafari Ndefu sana ya Kujifunza Unajua Makanisa ya Kiprotestant yameanza Mwaka gani?

Ndo maana Niliuliza Unafahamu Kuhusu Aprokrifa na Pseudepigrapha...?

Sasa Nimepata Jibu Huna Unalojua Kuhusu Hivyo vitu!

Nilitaka Nikuvishe Mzigo mzito wa Kujibu hoja Ambazo Huna elimu nazo..

Kama Hujui hata what so Called Pumzi ya Mungu (Canon) zilipangwaje kwa sheria zipi basi una safari ndefu sana..

Uwezo wako Ni mdogo sana 😀😀😀

Kwaheri..🤣🤣

Maana Kama hoja Zote nilizokuuliza kwenye Post Jibu lake ni Vitabu vinafuatwa na Protestant 🤣🤣 unasafari ndefu sana
Safiri salama
 
Natamani Mtu aniambie Shetani alisema uongo Sehemu gani maana Umeandika Uongo wa shetani Miss Hebu niambie na Mimi lro niujue uongo wa shetani
Ile kusema wakila tunda hawatakufa, pale tu ndipo uongo wa shetani ulipo. Na ni kawaida ya shetani kuweka ukweli mwingi na kuchanganya na uongo kidogo.

Kifo kipo cha kiroho na kimwili, saa ile ile walipokula, utukufu wa Mungu uliwaondoka wakabaki uchi na ndipo kifo cha kiroho kilipotokea.
 
Huu Ndo utetezi wako?
Duh Bhasi nahisi Bado unasafari Ndefu sana ya Kujifunza Unajua Makanisa ya Kiprotestant yameanza Mwaka gani?

Ndo maana Niliuliza Unafahamu Kuhusu Aprokrifa na Pseudepigrapha...?

Sasa Nimepata Jibu Huna Unalojua Kuhusu Hivyo vitu!

Nilitaka Nikuvishe Mzigo mzito wa Kujibu hoja Ambazo Huna elimu nazo..Nisamehe

Kama Hujui hata what so Called Pumzi ya Mungu (Canon) zilipangwaje kwa sheria zipi basi una safari ndefu sana..

Uwezo wako Ni mdogo sana 😀😀😀

Kwaheri..🤣🤣

Maana Kama hoja Zote nilizokuuliza kwenye Post Jibu lake ni Vitabu vinafuatwa na Protestant 🤣🤣 unasafari ndefu sana
Wewe ni Atheist uliyejifunika mwavuli wa Theology. Wewe na wenzako mlifikiri mtaweza kuipotosha jamii yote kwa hoja za kishetani eti Biblia sio Neno la Mungu ina contradictions. Misheni yenu imefeli mapema sana na ukweli umejulikana: Biblia ni Neno la Mungu.
 
"Neno la Mungu" siyo Biblia.

  • Neno la Mungu linatajwa kuwepo kutoka mwanzo hata kabla ya uumbaji wakati Biblia niya juzi.

  • "Neno la Mungu" halifungwi kwenye kitabu/kitu fulani, Neno la Mungu lipo kila sehemu.

  • Kwenye Biblia watu wengi wameongea, mapepo na Shetani pia wameongea kwenye Biblia, hii inaonesha Biblia siyo Neno la Mungu.

Biblia ni kitabu kama vilivyo vitabu vingine.
 
Usichanganye Neno la Mungu na ule mstari "Neno alikuwepo kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu"
Umemaaniasha Neno la Mungu kabla ya Biblia halikuwepo

Hili ni Neno la Mungu?
Mwa 3:4 SUV
[4] Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
 
Hoja dhaifu. Jina sio kipimo cha uhalali wa kitu.
  • Neno Utatu halipo pia katika Biblia, lakini dhana ya Mungu mmoja katika nafsi tatu iko wazi (Mathayo 28:19).
Mungu hana nafsi tatu wala hana mtoto wala hakuna mungu Baba, mwana na roho huo ni ushirikina mtupu, na hiyo Biblia ni kitabu cha ujanja ujanja ambacho hata kwenye maandiko hakipo
 
Hoja dhaifu. Jina sio kipimo cha uhalali wa kitu.
  • Neno Utatu halipo pia katika Biblia, lakini dhana ya Mungu mmoja katika nafsi tatu iko wazi (Mathayo 28:19).
Mwambie tu kuwa ni mkusanyiko wa vitabu vilivyowekwa pamoja. Huo mkusanyiko unaitwa Biblia. Hata mkusanyiko wa viungo huitwa mwili, lakini ndani yake hakuna kiungo kinachoitwa mwili!
 
Back
Top Bottom