Biblia ni nini? Maelezo ya kina kuhusu kitabu hiki ambacho shetani anakichukia kuliko vitabu vyote!

Biblia ni nini? Maelezo ya kina kuhusu kitabu hiki ambacho shetani anakichukia kuliko vitabu vyote!

Huyo member ni msanii, mimi kuna maswali nimemuuliza hata kujibu ameshindwa. Ameyaacha plain

Mimi biblia naijua . O level nimesoma Maua seminary na nilipata A ya bible knowledge, na A level nilipata B ya divinity pale loyola.
Kama O-level tu unapiga kelele hivi, siku ukipata PhD hata moja tu si dunia yote itajua?
Alijaribu kunidanganya kwa kusema kwenye biblia utumwa uliruhusiwa agano la kale tu kabla yesu hajaja , mimi nikamuuliza swali kwa mstari wa agano jipya amegoma kujibu
Hapa JF nina nyuzi nyingi, mkuu. Ni vigumu kujibu kila swali analouliza mtu. Na maswali mengine hayahusiani directly na mada kama hilo swali lako. Hivyo kuacha kujibu swali lako sio kwamba nimeshindwa.
 
Ukiulizwa swali unapaswa kulijibu kwanza kabla hujauliza swali jipya
Uelewa wako ni mdogo. Mateso aliyoyapata Ayubu yalimletea faida kubwa kuliko kama asingeteswa. Kwa haraka haraka unaweza kufikiri Mungu alimuonea, kumbe sio.
 
Mungu hatambui kitabu kinachoitwa Biblia, kama unabisha leta andiko lililotaja neno biblia
Hoja dhaifu. Jina sio kipimo cha uhalali wa kitu.
  • Neno Utatu halipo pia katika Biblia, lakini dhana ya Mungu mmoja katika nafsi tatu iko wazi (Mathayo 28:19).
 
Hoja dhaifu. Jina sio kipimo cha uhalali wa kitu.
  • Neno Utatu halipo pia katika Biblia, lakini dhana ya Mungu mmoja katika nafsi tatu iko wazi (Mathayo 28:19).
Chochote ambacho hakikuandikwa katika maandiko ni batili, maana kimekuwapo kwa busara/maarifa ya kibinadamu. Hivyo na fundisho la utatu sio la kimaandiko na ni la uongo na Mathew 28:19 haiuzungumzii utatu kama mlivyoaminishwa na wanadamu. BTW Yesu Kristo mwenyewe alisema tusimwamini tu blindly ila tumuamini kama yasemavyo maandiko; why tuamini hayo mafundisho ambayo ndani ya maandiko hayapo?
 
Biblia ni mkusanyiko wa vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi mbalimbali kwa muda wa takriban miaka 1,500, lakini vyote vina ujumbe mmoja unaotuelekeza kwa Mungu na jinsi ya kupata wokovu kwa njia ya Yesu Kristo.

Biblia imegawanyika katika sehemu kuu mbili:
  1. Agano la Kale – Linaeleza uumbaji wa dunia, historia ya Israeli, sheria za Mungu, unabii, na maandiko ya hekima. Linajumuisha vitabu vya Musa (Torati), vitabu vya kihistoria, vitabu vya mashairi na hekima (kama Zaburi, Mithali, na Mhubiri), na vitabu vya manabii.
  2. Agano Jipya – Linaeleza maisha, huduma, kifo, na ufufuo wa Yesu Kristo, pamoja na mafundisho ya mitume. Linajumuisha Injili, Matendo ya Mitume, nyaraka za mitume, na kitabu cha unabii – Ufunuo wa Yohana.
Je, Ni Sahihi Kuiita Biblia "Neno la Mungu"?
Ndiyo, ni sahihi kuiita Biblia Neno la Mungu kama unaelewa maana yake kwa usahihi. Biblia sio kitabu ambacho kila mstari wake ni maneno yaliyotamkwa moja kwa moja na Mungu, bali ni Maandiko yaliyoandikwa kwa uongozi wa Mungu (2 Timotheo 3:16). Ndani ya Biblia tunapata aina mbalimbali za Maandiko:
  1. Maneno ya Mungu Mwenyewe – Mfano, Amri Kumi (Kutoka 20:1-17) na maneno ya Yesu Kristo yaliyonukuliwa katika Injili.
  2. Maneno ya wanadamu waliovuviwa na Mungu – Manabii na mitume kama vile Isaya, Yeremia, na Paulo waliandika kwa kuongozwa na Mungu.
  3. Maneno ya wanadamu wa kawaida– Biblia inanukuu maneno ya watu mbalimbali, hata wale waliompinga Mungu. Mfano:
    • Maneno ya Shetani (Mwanzo 3:1-5, Mathayo 4:3-9) – yameandikwa ili kufunua uongo wake na jinsi Mungu anavyomshinda.
    • Maneno ya Goliathi (1 Samweli 17:8-10) – yanaonyesha kiburi chake kabla ya kushindwa na Daudi.
    • Maneno ya Farao (Kutoka 5:2) – yanadhihirisha ukaidi wake dhidi ya Mungu na jinsi jeshi lake lilivyoangamia.
    • Maneno ya makahaba – Mfano, Rahabu alivyoshuhudia juu ya ukuu wa Mungu wa Israeli (Yoshua 2:9-11).
Kwa nini sasa Biblia Inaitwa Neno la Mungu wakati ina maneno ya Shetani, Goliathi, na watu wengine waovu?
Biblia haielezi aliyoyatamka tu Mungu, bali inasimulia historia, mafundisho, unabii, na hata hila za Shetani kwa lengo la kutoa maarifa na mwongozo kwa wanadamu. Kila kilichoandikwa ndani yake kina sehemu katika mpango wa Mungu wa wokovu. Kwa hiyo, ingawa ndani yake kuna maneno ya waovu, ujumbe wa jumla wa Biblia ni Neno la Mungu kwa sababu unatoa ufunuo wa mpango wake kwa wanadamu.

Kama walioandika Biblia waliongozwa na Mungu, kwanini Biblia ina maneno yanayokinzana (Contradictions)?
Baadhi ya watu hudai kuwa Biblia ina "contradictions." Sababu zinazofanya watu wadai kwamba Biblia ina maneno yanayojipinga ni hizi:
  1. Kutokuelewa muktadha – Maandiko yanapotafsiriwa nje ya muktadha wake, yanaweza kuonekana kama yanakinzana.
  2. Tafsiri tofauti – Lugha za asili (Kiebrania, Kiaramu, na Kiyunani) zina maana za kina ambazo mara nyingine haziwezi kufasiriwa kikamilifu kwa lugha nyingine bila ufafanuzi wa kina. Kwahiyo kama mtu anasoma Biblia kwa lugha ya KIswahili, asipoelewa maana ya maneno fulani anatakiwa achunguze maana halisi ya maneno hayo kutoka kwenye lugha hizo "original" zilizotumika kuandika Biblia.
  3. Mitazamo tofauti ya waandishi – Injili nne(Mathayo, Marko, Luka, na Yohana) zinaelezea maisha ya Yesu kwa mitazamo(perspective) tofauti, lakini ujumbe wao ni mmoja. Yaani, kila mwandishi wa Injili hizo aliandika kwa mtazamo wake (perspective), akilenga wasikilizaji wake maalum na akisisitiza vipengele fulani vya huduma ya Yesu, lakini ujumbe wao wote unakubaliana juu ya ukweli wa Kristo.
  4. Kutompokea Roho Mtakatifu – Biblia inasema kuwa Roho Mtakatifu ndiye anayetufundisha na kututia kwenye kweli yote (Yohana 16:13). Watu wengi wanaodai kuwa Biblia ina makosa hawaongozwi na Roho Mtakatifu, hivyo hawawezi kuelewa maana ya kina ya Maandiko. (1 Wakorintho 2:14: “Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayakubali mambo ya Roho wa Mungu, maana kwake ni upuzi; wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yanatambulikana kwa jinsi ya rohoni.”)
  5. Kupuuza au kutotambua huduma ya ualimu katika Kanisa – Katika kanisa Mungu ameweka wengine kuwa walimu ili kusaidia kueleza na kufafanua Maandiko kwa usahihi. Waefeso 4:11-12 inasema: "Naye ameweka wengine kuwa mitume, wengine manabii, wengine wainjilisti, wengine wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe." Wanaodai kuwa Biblia ina makosa wanapaswa kuwauliza wale waliopewa huduma ya ualimu badala ya kutoa madai yasiyo na msingi. Mungu hajatuacha bila mwongozo, bali amewapa wengine karama ya kufundisha kwa ajili ya kujenga mwili wa Kristo.
  6. Uchambuzi wa juu juu – Wengi wanaosema Biblia ina makosa huwa hawajaisoma kwa kina wala kuitafakari kwa uangalifu. Kama nilivyoeleza katika ponit #5, katika Kanisa kuna Watumishi wenye huduma ya ualimu. Mtu anayeshindwa kuelewa Maandiko fulani anapaswa kuwauliza walimu.
Kwanini Biblia ni ya kuaminika?
  1. Utabiri wake umetimia – Unabii mwingi sana katika Biblia umetimia kwa usahihi, kwa mfano kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
  2. Jinsi ilivyohifadhiwa – Ingawa Biblia iliandikwa kwa maelfu ya miaka iliyopita, maandiko yake yamehifadhiwa kwa usahihi. Nakala kama "Dead Sea Scrolls" zinathibitisha uhalisi wa maandiko ya Agano la Kale.
  3. Athari zake kwa wanadamu – Hakuna kitabu kingine kilichobadilisha maisha ya watu kama Biblia. Mamilioni ya watu wameshuhudia jinsi Neno la Mungu lilivyobadilisha maisha yao. Majambazi wengi wameokoka, makahaba wengi wameacha umalaya, wachawi wameacha uchawi, wenye mapepo wengi wamefunguliwa nk nk baada ya kusikia Neno la Mungu.
  4. Majaribio ya kuiangamiza yameshindwa – Kwa karne nyingi, watawala wamejaribu kupiga marufuku na kuiangamiza Biblia, lakini bado imeendelea kuwepo na kuwa kitabu kinachosomwa zaidi duniani. Hivi sasa Biblia inauzwa kwa wingi huko Marekani
Kwa Nini Shetani Anachukia Biblia?
Shetani anachukia Biblia kwa sababu:
  • Inaonyesha ukweli wa Mungu na kufichua uongo wake – Biblia inafunua mipango yake mibaya.
  • Inawaelekeza watu kwa Yesu Kristo – Shetani hapendi watu wapate wokovu.
  • Ni silaha dhidi yake – Yesu alishinda majaribu ya shetani jangwani kwa kutumia Maandiko (Mathayo 4:1-11).
Biblia ni kitabu cha kipekee ambacho kina ujumbe wa wokovu kwa wanadamu wote. Ingawa ndani yake kuna maneno ya watu waovu, na hata Shetani mwenyewe, maandiko haya yote yamewekwa kwa kusudi la Mungu ili kutufundisha, kutuonya, na kutuelekeza wanadamu katika njia ya wokovu. Kwa hiyo, Biblia kwa ujumla wake ni Neno la Mungu, kwa kuwa ni andiko lililovuviwa na Mungu kwa kusudi lake kuu la kuokoa wanadamu. Badala ya kuitilia shaka, ni muhimu kuisoma, kuitafakari, na kuiishi, kwa kuwa ni nuru au taa katika giza la dunia hii.

Usikubali kupotoshwa na manabii wa uongo kuhusu ukweli wa kitabu hiki "BIBLIA"


You have known the truth, and let it set you free." (John 8:32)
Nitarudi
 
Chochote ambacho hakikuandikwa katika maandiko ni batili, maana kimekuwapo kwa busara/maarifa ya kibinadamu. Hivyo na fundisho la utatu sio la kimaandiko na ni la uongo na Mathew 28:19 haiuzungumzii utatu kama mlivyoaminishwa na wanadamu. BTW Yesu Kristo mwenyewe alisema tusimwamini tu blindly ila tumuamini kama yasemavyo maandiko; why tuamini hayo mafundisho ambayo ndani ya maandiko hayapo?
Unaamini kuna Roho Mtakatifu? Tuanzie hapo kwanza.
 
Wewe una PhDs ngapi kati ya hizi:
  1. PhD in Biblical Studies
  2. PhD in Old Testament Studies
  3. PhD in New Testament Studies
  4. PhD in Biblical Theology
  5. PhD in Biblical Hermeneutics
  6. PhD in Septuagint Studies
  7. PhD in Textual Criticism
  8. PhD in Biblical Exegesis
  9. PhD in Biblical Archaeology
  10. PhD in Biblical Languages and Literature
  11. PhD in Torah Studies
  12. PhD in Prophetic Literature
  13. PhD in Wisdom Literature
  14. PhD in Psalms and Poetic Books
  15. PhD in Gospel Studies
  16. PhD in Pauline Studies
  17. PhD in Johannine Literature
  18. PhD in Apocalyptic Literature
  19. PhD in Biblical Ethics
  20. PhD in Intertestamental Studies
  21. PhD in Pentateuch Studies
  22. PhD in Historical Books
  23. PhD in Deuteronomistic History
  24. PhD in Psalms Studies
  25. PhD in Hebrew Prophecy
  26. PhD in Dead Sea Scrolls Studies
  27. PhD in Ancient Near Eastern and Biblical Studies
  28. PhD in Old Testament Eschatology
  29. PhD in Old Testament Law and Ethics
  30. PhD in Old Testament Theology
  31. PhD in Synoptic Gospels Studies
  32. PhD in Parables of Jesus
  33. PhD in Christology of the New Testament
  34. PhD in Acts and Early Church History
  35. PhD in Petrine Literature
  36. PhD in New Testament Textual Criticism
  37. PhD in Pauline Theology
  38. PhD in New Testament Eschatology
  39. PhD in Hebrews and General Epistles
  40. PhD in Revelation Studies
  41. PhD in Biblical Hebrew Studies
  42. PhD in Biblical Greek Studies
  43. PhD in Aramaic and Semitic Languages
  44. PhD in Biblical Exegetical Methods
  45. PhD in Biblical Literary Criticism
  46. PhD in Biblical Translation Studies
  47. PhD in Septuagint and Greek Old Testament
  48. PhD in Intertextuality of the Bible
  49. PhD in Biblical Rhetoric and Persuasion
  50. PhD in Biblical Canon Studies
Inahusiana Nini na Maswali au Na Post Nilizoandika?
 
Hoja dhaifu. Jina sio kipimo cha uhalali wa kitu.
  • Neno Utatu halipo pia katika Biblia, lakini dhana ya Mungu mmoja katika nafsi tatu iko wazi (Mathayo 28:19).
Huko usiguse maana Hukujui..
UNahamisha Mada badala Kujibu swali uliloulizwa...Duh many Logical fallacy
 
Chochote ambacho hakikuandikwa katika maandiko ni batili, maana kimekuwapo kwa busara/maarifa ya kibinadamu. Hivyo na fundisho la utatu sio la kimaandiko na ni la uongo na Mathew 28:19 haiuzungumzii utatu kama mlivyoaminishwa na wanadamu. BTW Yesu Kristo mwenyewe alisema tusimwamini tu blindly ila tumuamini kama yasemavyo maandiko; why tuamini hayo mafundisho ambayo ndani ya maandiko hayapo?
👏👏👏
 
Inahusiana Nini na Maswali au Na Post Nilizoandika?
Kuna post umeonyesha kuwa umesoma Theology. Taja ni PhDs ngapi za Theology ulizo nazo katika hizo 50. Itasaidia kuelewa kwanini unadai Biblia ina contradictions
 
Kuna post umeonyesha kuwa umesoma Theology. Taja ni PhDs ngapi za Theology ulizo nazo katika hizo 50. Itasaidia kuelewa kwanini unadai Biblia ina contradictions
Swala ni kwamba Inakusaidia Nini Kwenye Kujibu maswali Ninayo Kuuliza?

Ok tuseme nimekuambia Kuhusu Area of Professional expertise, Je itakusaidia Nini katika Kujibu swali Ninalokuuliza?

"That's an unprofessional argument (argumentum ad hominem) and completely illogical 😀😀..

Baki na Hiyo niliyokuambia Kuwa Nimesoma Theology Inatosha sana..

Biblia Ina contradiction ila Ukitaka Tuzidiscuss Niambie tutafanya Hivyo Ila kwenye Discussion hiyo nataka Tufanya kama wasomi na Sio stramen zako na Logical fallacy zisizo na maana
 
Back
Top Bottom