Biblia ni nini? Maelezo ya kina kuhusu kitabu hiki ambacho shetani anakichukia kuliko vitabu vyote!

Biblia ni nini? Maelezo ya kina kuhusu kitabu hiki ambacho shetani anakichukia kuliko vitabu vyote!

Biblia ni maelezo ya watu juu ya mambo mbalimbali,watu hao wakati mwingine humnukuu 'Mungu' au yesu,hakuna maneno ya Mungu kwenye biblia wala biblia si neno la Mungu
Mkuu samahani, Je, unamjua Mungu? Kama ni ndiyo, ulimjulia wapi? Kama siyo, umejuaje kuwa biblia siyo neno lake?
 
Sasa Wewe Unanipeleka Mbele Kwenye Mambo ya mbele wakati jambo la awali hujamaliza Huko Kote tutafika Wala usijali Twende Pole pole Kwanza Nijue Tatizo lake Pale Edeni ni Kosa gani..
Mbona nimekujibu. Adam na Hawa wapo leo? Shetani alisema hawatakufa. Nimekuambia pia walikuwa uchi. Mungu ni roho. Hao walibadilika wakawa roho?
Kama Nilivyokuambia Ukiona Huna Jibu sema Sina kwenye Mijadala ya Kielimu Ukisema Kitu Sijui wala Huwezi kuchekwa maana Si Kila Kitu tunaweza Kujua..

Kwa Kuwa bado nasubiri Uniambie Kosa La Shetani Ngoja Nijibu Hoja Uliyoleta..

Kwanza shetani alikuwa Sahihi kabisa Kusema Kuwa Yeye Ndiyo mmiliki wa Dunia Hii na Viti Vyote Kwa Kutumia Biblia hiyo hiyo Twende pamoja..

  • Biblia Inamtaja Shetani Kama Mungu wa Ulimwengu Huu, Mfalme wa dunia hii na Kiongozi wa Ulimwengu huu..
2 Wakorintho 4:3-4

"Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.



Yohana 12:31
" Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo; sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje."

1 Yohana 5:19
"Tunaijua kwamba sisi tuko kwa Mungu, lakini ulimwengu wote uko katika mikono ya yule m ovu."


Yohana 14:30
"Nisingependa kusema nanyi mengi, kwa maana mfalme wa dunia anakuja, wala hana lolote kwangu."



Yako mafungu mengi ila Hayo yanatosha kwa leo

Bado Hujaniambia Bado Kosa Lake Ni Nini
 
Mkuu samahani, Je, unamjua Mungu? Kama ni ndiyo, ulimjulia wapi? Kama siyo, umejuaje kuwa biblia siyo neno lake?
Hivi ule msitari paulo anasema alitunga uwongo Ili naye ajisifu walau kidogo,yale ni maneno ya Mungu?..au ule unaosema 'enyi wagalatia wajinga ni nani aliyewaloga..yale ni maneno ya Mungu au ya paulo kwa wagalatia!?
 
Kwanza shetani alikuwa Sahihi kabisa Kusema Kuwa Yeye Ndiyo mmiliki wa Dunia Hii na Viti Vyote Kwa Kutumia Biblia hiyo hiyo Twende pamoja..

  • Biblia Inamtaja Shetani Kama Mungu wa Ulimwengu Huu, Mfalme wa dunia hii na Kiongozi wa Ulimwengu huu..
Soma vizuri. Shetani anatajwa kama mungu wa dunia, sio Mungu. Angalia tofauti ya Capital na Small letter, mkuu
 
Biblia ni mkusanyiko wa vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi mbalimbali kwa muda wa takriban miaka 1,500, lakini vyote vina ujumbe mmoja unaotuelekeza kwa Mungu na jinsi ya kupata wokovu kwa njia ya Yesu Kristo.

Biblia imegawanyika katika sehemu kuu mbili:
  1. Agano la Kale – Linaeleza uumbaji wa dunia, historia ya Israeli, sheria za Mungu, unabii, na maandiko ya hekima. Linajumuisha vitabu vya Musa (Torati), vitabu vya kihistoria, vitabu vya mashairi na hekima (kama Zaburi, Mithali, na Mhubiri), na vitabu vya manabii.
  2. Agano Jipya – Linaeleza maisha, huduma, kifo, na ufufuo wa Yesu Kristo, pamoja na mafundisho ya mitume. Linajumuisha Injili, Matendo ya Mitume, nyaraka za mitume, na kitabu cha unabii – Ufunuo wa Yohana.
Je, Ni Sahihi Kuiita Biblia "Neno la Mungu"?
Ndiyo, ni sahihi kuiita Biblia Neno la Mungu kama unaelewa maana yake kwa usahihi. Biblia sio kitabu ambacho kila mstari wake ni maneno yaliyotamkwa moja kwa moja na Mungu, bali ni Maandiko yaliyoandikwa kwa uongozi wa Mungu (2 Timotheo 3:16). Ndani ya Biblia tunapata aina mbalimbali za Maandiko:
  1. Maneno ya Mungu Mwenyewe – Mfano, Amri Kumi (Kutoka 20:1-17) na maneno ya Yesu Kristo yaliyonukuliwa katika Injili.
  2. Maneno ya wanadamu waliovuviwa na Mungu – Manabii na mitume kama vile Isaya, Yeremia, na Paulo waliandika kwa kuongozwa na Mungu.
  3. Maneno ya wanadamu wa kawaida– Biblia inanukuu maneno ya watu mbalimbali, hata wale waliompinga Mungu. Mfano:
    • Maneno ya Shetani (Mwanzo 3:1-5, Mathayo 4:3-9) – yameandikwa ili kufunua uongo wake na jinsi Mungu anavyomshinda.
    • Maneno ya Goliathi (1 Samweli 17:8-10) – yanaonyesha kiburi chake kabla ya kushindwa na Daudi.
    • Maneno ya Farao (Kutoka 5:2) – yanadhihirisha ukaidi wake dhidi ya Mungu na jinsi jeshi lake lilivyoangamia.
    • Maneno ya makahaba – Mfano, Rahabu alivyoshuhudia juu ya ukuu wa Mungu wa Israeli (Yoshua 2:9-11).
Kwa nini sasa Biblia Inaitwa Neno la Mungu wakati ina maneno ya Shetani, Goliathi, na watu wengine waovu?
Biblia haielezi aliyoyatamka tu Mungu, bali inasimulia historia, mafundisho, unabii, na hata hila za Shetani kwa lengo la kutoa maarifa na mwongozo kwa wanadamu. Kila kilichoandikwa ndani yake kina sehemu katika mpango wa Mungu wa wokovu. Kwa hiyo, ingawa ndani yake kuna maneno ya waovu, ujumbe wa jumla wa Biblia ni Neno la Mungu kwa sababu unatoa ufunuo wa mpango wake kwa wanadamu.

Kama walioandika Biblia waliongozwa na Mungu, kwanini Biblia ina maneno yanayokinzana (Contradictions)?
Baadhi ya watu hudai kuwa Biblia ina "contradictions." Sababu zinazofanya watu wadai kwamba Biblia ina maneno yanayojipinga ni hizi:
  1. Kutokuelewa muktadha – Maandiko yanapotafsiriwa nje ya muktadha wake, yanaweza kuonekana kama yanakinzana.
  2. Tafsiri tofauti – Lugha za asili (Kiebrania, Kiaramu, na Kiyunani) zina maana za kina ambazo mara nyingine haziwezi kufasiriwa kikamilifu kwa lugha nyingine bila ufafanuzi wa kina. Kwahiyo kama mtu anasoma Biblia kwa lugha ya KIswahili, asipoelewa maana ya maneno fulani anatakiwa achunguze maana halisi ya maneno hayo kutoka kwenye lugha hizo "original" zilizotumika kuandika Biblia.
  3. Mitazamo tofauti ya waandishi – Injili nne(Mathayo, Marko, Luka, na Yohana) zinaelezea maisha ya Yesu kwa mitazamo(perspective) tofauti, lakini ujumbe wao ni mmoja. Yaani, kila mwandishi wa Injili hizo aliandika kwa mtazamo wake (perspective), akilenga wasikilizaji wake maalum na akisisitiza vipengele fulani vya huduma ya Yesu, lakini ujumbe wao wote unakubaliana juu ya ukweli wa Kristo.
  4. Kutompokea Roho Mtakatifu – Biblia inasema kuwa Roho Mtakatifu ndiye anayetufundisha na kututia kwenye kweli yote (Yohana 16:13). Watu wengi wanaodai kuwa Biblia ina makosa hawaongozwi na Roho Mtakatifu, hivyo hawawezi kuelewa maana ya kina ya Maandiko. (1 Wakorintho 2:14: “Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayakubali mambo ya Roho wa Mungu, maana kwake ni upuzi; wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yanatambulikana kwa jinsi ya rohoni.”)
  5. Kupuuza au kutotambua huduma ya ualimu katika Kanisa – Katika kanisa Mungu ameweka wengine kuwa walimu ili kusaidia kueleza na kufafanua Maandiko kwa usahihi. Waefeso 4:11-12 inasema: "Naye ameweka wengine kuwa mitume, wengine manabii, wengine wainjilisti, wengine wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe." Wanaodai kuwa Biblia ina makosa wanapaswa kuwauliza wale waliopewa huduma ya ualimu badala ya kutoa madai yasiyo na msingi. Mungu hajatuacha bila mwongozo, bali amewapa wengine karama ya kufundisha kwa ajili ya kujenga mwili wa Kristo.
  6. Uchambuzi wa juu juu – Wengi wanaosema Biblia ina makosa huwa hawajaisoma kwa kina wala kuitafakari kwa uangalifu. Kama nilivyoeleza katika ponit #5, katika Kanisa kuna Watumishi wenye huduma ya ualimu. Mtu anayeshindwa kuelewa Maandiko fulani anapaswa kuwauliza walimu.
Kwanini Biblia ni ya kuaminika?
  1. Utabiri wake umetimia – Unabii mwingi sana katika Biblia umetimia kwa usahihi, kwa mfano kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
  2. Jinsi ilivyohifadhiwa – Ingawa Biblia iliandikwa kwa maelfu ya miaka iliyopita, maandiko yake yamehifadhiwa kwa usahihi. Nakala kama "Dead Sea Scrolls" zinathibitisha uhalisi wa maandiko ya Agano la Kale.
  3. Athari zake kwa wanadamu – Hakuna kitabu kingine kilichobadilisha maisha ya watu kama Biblia. Mamilioni ya watu wameshuhudia jinsi Neno la Mungu lilivyobadilisha maisha yao. Majambazi wengi wameokoka, makahaba wengi wameacha umalaya, wachawi wameacha uchawi, wenye mapepo wengi wamefunguliwa nk nk baada ya kusikia Neno la Mungu.
  4. Majaribio ya kuiangamiza yameshindwa – Kwa karne nyingi, watawala wamejaribu kupiga marufuku na kuiangamiza Biblia, lakini bado imeendelea kuwepo na kuwa kitabu kinachosomwa zaidi duniani. Hivi sasa Biblia inauzwa kwa wingi huko Marekani
Kwa Nini Shetani Anachukia Biblia?
Shetani anachukia Biblia kwa sababu:
  • Inaonyesha ukweli wa Mungu na kufichua uongo wake – Biblia inafunua mipango yake mibaya.
  • Inawaelekeza watu kwa Yesu Kristo – Shetani hapendi watu wapate wokovu.
  • Ni silaha dhidi yake – Yesu alishinda majaribu ya shetani jangwani kwa kutumia Maandiko (Mathayo 4:1-11).
Biblia ni kitabu cha kipekee ambacho kina ujumbe wa wokovu kwa wanadamu wote. Ingawa ndani yake kuna maneno ya watu waovu, na hata Shetani mwenyewe, maandiko haya yote yamewekwa kwa kusudi la Mungu ili kutufundisha, kutuonya, na kutuelekeza wanadamu katika njia ya wokovu. Kwa hiyo, Biblia kwa ujumla wake ni Neno la Mungu, kwa kuwa ni andiko lililovuviwa na Mungu kwa kusudi lake kuu la kuokoa wanadamu. Badala ya kuitilia shaka, ni muhimu kuisoma, kuitafakari, na kuiishi, kwa kuwa ni nuru au taa katika giza la dunia hii.

Usikubali kupotoshwa na manabii wa uongo kuhusu ukweli wa kitabu hiki "BIBLIA"


You have known the truth, and let it set you free." (John 8:32)
Kuna sehemu au nchi mfano Afghanistan, kuna watu walikamatwa wakiwa na biblia za kiarabu wakahukumiwa kukatwa vichwa na binadamu. Shetani alikuwepo?
Msipende kumsingizia uongo shetani.
 
Bado Hujaniambia Bado Kosa Lake Ni Nini
Ufunuo 12:9
"Yule joka akatupwa, yule nyoka wa zamani aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye."

Yohana 8:44
"Ninyi ni wa baba yenu Ibilisi, na mnataka kuyatenda mapenzi ya baba yenu. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakusimama katika kweli, kwa sababu hamna kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa maana yeye ni mwongo na baba wa uongo."

Hujaona tu kuwa shetani ni mwongo?
 
Tunapambana na mawakala wa shetani humu wakipotosha maandiko matakatifu ya BIBLIA, hawatashinda
 
  1. Hivi ule msitari paulo anasema alitunga uwongo Ili naye ajisifu walau kidogo,yale ni maneno ya Mungu?..au ule unaosema 'enyi wagalatia wajinga ni nani aliyewaloga..yale ni maneno ya Mungu au ya paulo kwa wagalatia!?
Tafadhali jibu kwanza maswali ya awali, maana hiki ulichouliza mwandishi amekiweka kwenye uzi.
Amefafanua kuwa kwenye biblia kuna maneno ya Mungu mwenyewe, kuna maneno ya shetani, kuna maneno ya binadamu wa kawaida, kuna maneno ya wachawi, kuna maneno ya majini n.k. Yote yamewekwa kwa sababu maalum kabisa, na mwandishi amefafanua sababu hizo.

Sasa jibu maswali ya msingi;
  1. Je unamfaham/unamjua Mungu?
  2. Kama unamjua, ulimjulia wapi?
  3. Kama humjui, umejuaje biblia sio neno lake?
 
Back
Top Bottom