Biblia wanayotumia Wakotoliki na wanayotumia Walutheri pamoja na madhehebu mengine ni tofauti?

Author wa Bible ni Holy Spirit na Catholic Church. Whoever against the Mother Holy Church is against Jesus himself. Sasa hutaki sawa ....
 
Misale ya waumini sio biblia
 
Huu uzi ni kipimo cha kuonyesha waislam ni wastaarabu sana kuanzia comment ya kwanza mpaka ya 42 hakuna matusi wala dhihaka yoyote juu ya dini yenu hali hii iwe kwenye nyuzi zote kila mtu aheshimu imani ya mwenzake
 
Zina tofautiana na hata idadi ya vitabu ni tofauti.Katoliki vipo 72 na Lutheran vipo 66
 
Wakatoliki ndio walitafsiri biblia hizi tunazotumia kutoka katika lugha za Kiebrania na Kigiriki, ambazo ndizo lugha mbili original zilizotumika kuandika biblia za awali. Biblia wanazotumia Wakatoliki zina vitabu 72 na wanazotumia Waprotestanti na Wapentekoste zina vitabu 66.
 
Misale ya Waumini sio Biblia ndugu, usipotoshe wadau!
 
Inaonyesha haujui chichite kuhusu tafsiri za bibiblia.Lugha Mama iliyotunza neno la Mungu ni KihirikI,kiebrania na Kiyunani.Hiyo ni kutokana na utajiri mkubwa wa mameno wa lugha hizo.Lugha zetu sisi bado ni changa mno,na zinakua kila siku.Maneno yake yanabadilika maana kila baada ya musa fulani.Hivyo,kila baada ya musa fulani hufanyila tafsiri tena kutoka lugha asili kuja lugha zetu.
Lakini tafsiri za biblia zipo za aina mbili,ya neno kwa neno na ya maana kwa maana.Ukisoma biblia iliyotafsiriwa neno kwa neno inatofautinana na iliyotafsiriwa maana kwa maana.
Mfano tafsiri ya neno kwa neno.
Yesu anaambiwa salam mfalme wa wayahudi.
Mfano ya tafsiri ya maana kwa maana
Shikamoo mfalme wa wayahudi.Wao wametafsiri maana tu,ili tuelewe ililuwa salama.
Hivyo ili uelewa maandiko vizuri,ni vema ukawa unasoma tafsiri ya neno kwa neno na ya maana kwa maana kwa wakati mmoja.
 

Wapo wanaoamini vitabu vimeongezwa na wapo wanaoamini vitabu vimepunguzwa sasa basi mkweli ni yupi?

Ukweli ni kwamba dini zimeanzishwa na watu hivyo ni ujinga sana kuamini kuwa dini ziko sahihi kwa asilimia mia. Haipo dini iliyokamilika, zote zinalenga maslahi binafsi.

JESUS CHRIST aliishi kama mfano tumfuate, hiyo ndio njia ya kweli na uzima. ndo maana hata dini zilizokuepo kipindi kile zilimpinga.

Binadamu ni kiumbe mharibifu sana, wachache wanamaarifa wanapotosha wengi, epuka kuwa kundi la wengi.

”watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa”.
 
Misale ya Waumini sio Biblia ndugu, usipotoshe wadau!
kama sio biblia ni kitabu gani hicho, ni liturjia au katekisimu? Lini wakatoliki wamebeba biblia kama waprotestanti tuwaone na tujue biblia zao?
 
Jambo usilolijua si vizuri kulizungumzia. Zingatia neno moja lako linaweza potosha walio wengi ama kufunza walio wengi.
Weka hili
 
MTu kama hana hata biblia nyumban ukimwandikia haya itakuwa kaz bure.
 
Biblia sahihi kwa kufanyia utapeli ni hiyo inayoruhusu unywaji wa pombe tofauti na apo hizo nyingne walitunga watu wenye Figo mbovu.
 
kama sio biblia ni kitabu gani hicho, ni liturjia au katekisimu? Lini wakatoliki wamebeba biblia kama waprotestanti tuwaone na tujue biblia zao?
Misale sio Biblia, misale ni kitabu cha Wakatoliki chenye mpangilio wa masomo ya biblia kwa kadri ya kipindi cha mwaka wa kanisa, kama vile Mwaka A, B, C au kipindi maalum cha mwaka kama vile majilio au Kwaresma, pasaka nk. Misale imebeba pia sala mbalimbali na miongozo kama ya ubatizo, maziko nk. Misale huandaliwa na Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC). Swali jingine?
 
Jambo usilolijua si vizuri kulizungumzia. Zingatia neno moja lako linaweza potosha walio wengi ama kufunza walio wengi.
Weka hili
kama we unalijua unapaswa ulieleze kwa ufasaha ili kuondoa upotoshaji. Humu kila mtu yuko huru kuzungumzia jambo lolote regardless analijua au halijui, anayelijua vema huja na ukweli wote, ndivyo mijadala ilivyo, hujadiliwa hata na wasiojua mambo hayo na wajuaji huweka sawa. Kama unaona misale ya waumini si biblia pinga na sema kwa nini si biblia na sio kukimbilia kuona maoni ya mwenzako ni upotoshaji wakati ukweli unaujua wewe na unatakiwa uutoe
 
hayo ndiyo majibu yanayotakiwa kutolewa, swali endelevu, je hiyo misale ndiyo liturjia au katekisimu, fafanua na hapa kwa weledi tujue
 
Lini wakatoliki walibeba biblia kama waprotestanti tuijue hiyo biblia yao na inauzwa wapi tuipate?
 
Unaweza ukawa upo sahihi, ila watu Makini hawawezi kukuchukulia seriously maana uliwai tunga Uwongo humu dhidi ya Arius na Baraza la Nicea ili andiko lako liwe relivant. Likes na Follows za Jf zinaweza fanya Mtu aongope bila kuwa na mategemoe yoyote ya msingi dhidi ya uowngo huo.
AMANDRA!.

Gal 5:9 SUV​

Chachu kidogo huchachua donge zima.
 
Mkuu let the caged bird sings
unaweza kuweka uongo niliosema Kuhusu Arius na baraza la Nicea ningefurahi pia na mimi Kuuona..

Daima Nachukia Uongo na ndo maana Mara nyingi narekebisha Uongo kwa kutumia Facts sana sana Uongo ulionezwa na Dini Ili kuziba Maovu yake..

NAsubiri nione uongo wangu na ikiwezekana Niombe msamahe hadharani kwa Thread kabisa kila mtu ajue nilidanganya na nitaomba radhi..

Shukrani Sana mkuu nasubiri!
 
Lini wakatoliki walibeba biblia kama waprotestanti tuijue hiyo biblia yao na inauzwa wapi tuipate?
Biblia zinauzwa maduka ya vitabu, mara nyingi maduka haya yapo katika Parokia zote za Kanisa Katoliki, including biblia, misale na vitabu mbalimbali vinavyoandikwa na waumini wao. Kwa Dar ukienda pale St. Joseph mjini utavipata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…