Biblia wanayotumia Wakotoliki na wanayotumia Walutheri pamoja na madhehebu mengine ni tofauti?

Kanisa katoliki linalobatiza mashoga. Soon papa anataka biblia ibadilishwe tena.
Mkuu hiii viva katoliki heri ungeandika VIVA MASHUJAAA FC
 
Hujui ukichoandika. Wakatoliki HAWAMUABUDU Bikira Maria bali wanamuheshimu. Katika maombi wanamuomba AWAOMBEE kwa Mungu. Acheni upotoshaji
Kusujudia sio kuabudu siyo...
Nipe mstari katika Biblia unaogiza wakristo WAOMBE Maria AWAOMBEE Kwa Mungu?
Ukikosa ujue huo sio ukristo?
 
Mbona unaandika unazunguka hapo hapo? Kanisa limeanzishwa Yesu Kristu mwenyewe na kukabidhiwa kwa Mtume Petro. Na Mtume Petro anapowatuma Mitume kwenda kuhubiri neno sehemu mbalimbali kama Marco kwenda Misri, Mtume Thomas kwenda India na Mtume Yohana kwenda Antiokia.

Hayo yote yalianza karne ya kwanza. Dola ya Kirumi ilipingana na Ukristu sana na ikawatesa na kuwaadhibu watu wote waliomhubiri Kristu hadi karne ya 3. Karne ya 3 dola ya kirumi ikiwa chini ya Mfalme Constantine ndipo ikakubali kuwa Ukristo uwe ndiyo dini rasmi ya dola.

Ndipo ukaanza kuendelea dunia nzima ikiwa na makao yake makuu Rome Italy na Constatinople yakiwa makao madogo. Mwaka 325 Kanisa likafanya mkutano mkuu wa kwanza pale Nicea ambapo maaskofu walianza kutofautiana kiitikadi za imani.

Mwaka 590 chini ya Mfalme Gregory ndopo jina la Roman Catholic likaanza kutumika rasmi kwa ajili ya kujikita kimamlaka za nchi.

Mwaka 1054 ndipo kanisa la Orthodox likajitenga na kanisa KATOLIKI. Mwaka 1521 Martin Luther naye akajitenga.

Wewe historia yako unaitoa wapi? Haya nipe na wewe historia ya KIDHEHEBU chako
 
Kusujudia sio kuabudu siyo...
Nipe mstari katika Biblia unaogiza wakristo WAOMBE Maria AWAOMBEE Kwa Mungu?
Ukikosa ujue huo sio ukristo?
Ukisoma Biblia bila nguvu ya Roho Mtakatifu UTAWEHUKA tu.
 
Weka mstari Unaogiza watu WAOMBE Maria AWAOMBEE Kwa Mungu?
Acha Kona Kona..
Biblia siyo utaratibu wa kusali. Kuna Biblia halafu kuna sala. Hakuna dhehebu lolote ambalo linaingia kanisani na kusoma Biblia bila kutengeneza utaratibu wa sala.

Roman Catholic wanaomba Mama Maria AWAOMBEE kwa Mungu. Ni heshima tu kwa Mama wa Yesu Kristu. Au unataka kusema Bikira Maria siyo Mama wa Yesu
 
Mtume Petro anapowatuma Mitume kwenda kuhubiri neno sehemu mbalimbali kama Marco kwenda Misri, Mtume Thomas kwenda India na Mtume Yohana kwenda
Hakuna mtume hata mmoja alitumwa na Petro kuwa akahubiri

Yesu mwenyewe ndio aliwatuma

Soma Marko 16:15-16

"Akawaambia, “Nendeni ulimwenguni kote, mkawahubirie watu wote Habari Njema. Ye yote atakayeamini na kubatizwa ataoko lewa. Lakini ye yote ambaye atakataa kuamini, atahukumiwa.'


Yesu ndie aliwatuma mitume wote kwenda hakuntuma Petro tu kuwa nenda wewe halafu wewe kawatume wengine.Wote walipewa amri na Yesu mwenyewe wasambae huko na huko mwenye kwenda Roma aende mwenye kwenda ugiriki aende,nk na aliwambia yeye mwenyewe binafsi mbele ya wote akiwemo Petro pale wakiwa Israel sio Roma.Na Yesu hakunwambia Petro pale kuwa Petro watume hawa waende ulimwenguni kote kuhubiri Injili

Kusema Petro ndie aliwatuma ni uongo uliokubuhu
 
Roman Catholic wanaomba Mama Maria AWAOMBEE kwa Mungu. Ni heshima tu kwa Mama wa Yesu Kristu. Au unataka kusema Bikira Maria siyo Mama wa Yesu
Hayo mliyatoa wap? Kwenye Biblia hayapo

Mtume Petro alikuwa akipiga magoti mbele ya Maria na kumuomba awaombee kwa Mungu?
 
Weka mstari Unaogiza watu WAOMBE Maria AWAOMBEE Kwa Mungu?
Najua huwezi pata maana ukatolik haufuati Biblia

Kwa ufupi mnafuata kitu ambacho haipo kwenye Biblia sasa kazia na mstari hapo chini

1 Timotheo 4:1 Hata hivyo, neno lililoongozwa na roho linasema wazi kwamba wakati ujao watu fulani wataiacha imani, wakisikiliza maneno ya uwongo yaliyoongozwa na roho waovu na mafundisho ya roho waovu,
 
Kanisa la kweli ni lipi?, linalofuata kila kilicho andikwa kwenye Biblia ?
Naombeni msaada tafadhali nihamie huko
 
Kwahiyo kwa wasio wakatoliki hivyo vitabu wanavichukulia kama hekaya?
 
Nimekwambia nitajie KIDHEHEBU chako na uniambie kilianza lini?. Siyo mnakomaa tu na kubishana na Kanisa lenye waumini 1.4 Billion duniani kote
 
Nimekwambia nitajie KIDHEHEBU chako na uniambie kilianza lini?. Siyo mnakomaa tu na kubishana na Kanisa lenye waumini 1.4 Billion duniani kote
Jibu unachoulizwa

Muulizaji kakuuliza hili

"Weka mstari Unaogiza watu WAOMBE Maria AWAOMBEE Kwa Mungu?"

Si umjibu mbona swali liko wazi tu
 
Jibu unachoulizwa

Muulizaji kakuuliza hili

"Weka mstari Unaogiza watu WAOMBE Maria AWAOMBEE Kwa Mungu?"

Si umjibu mbona swali liko wazi tu
Nimekwisha jibu rudi nyuma kasome
 
Nimekwambia nitajie KIDHEHEBU chako na uniambie kilianza lini?. Siyo mnakomaa tu na kubishana na Kanisa lenye waumini 1.4 Billion duniani kote
Kuwa na waumini wengi ni shida nyingine maana kuna mfano wa Yesu wa Barabara Pana na nyembamba inatakiwa usome hicho kisa vizuri .
Shida kubwa ni kuwa unafanya na kuamini kitu ambacho haipo kwenye Biblia na mbaya zaidi unaamini ni agizo la Mungu...
Na si Hilo Tu hapo mengi mno sasa atasemaje mnafuata Biblia ikiwa Jambo ndogo Tu kama Kuomba Maria AWAOMBEE Kwa Mungu umeshindwa kutupa uthibitisho wa kimaandiko inaamaana huamini Biblia
 
Biblia siyo utaratibu wa ibada. Hapo ndipo nyie mapentekoste mnakosea. Nimekuuliza kuna ubaya gani kusema Mama Maria utuombee kwa Mungu?
 
Biblia siyo utaratibu wa ibada. Hapo ndipo nyie mapentekoste mnakosea. Nimekuuliza kuna ubaya gani kusema Mama Maria utuombee kwa Mungu?
Kwa sababu ni agizo ambalo haipo kwenye Biblia..
Je wewe binafsi umesoma popote kwenye Biblia wakristo wa kipindi cha mitume karne ya Kwanza wakiomba Mungu kupitia Maria...
Je kuna barua yeyote inampa Maria nafasi ya pekee?


Utatribu huo ulianza mwaka 431 na haukwepo awali Hilo lilikuwepo kwenye dini za kipagani kuwa na mama ya mungu katika dini zao na ukatolik ulipotaka kuongeza ushawishi wake wa kisiasa ulikubali fundisho hilo la kipangani kwa kulinganisha..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…