ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 22,235
- 51,111
- Thread starter
-
- #161
Wote wanaweza kulaumiwa tena lawama zaidi ni kwa mwanaume mtu mzima ku mrubuni mtoto tena unakuta wa shule ya msingiMwanaume atalaumiwa na mwanamke atalaumiwa sababu ya kitu kimoja akili, ila atakaye laumiwa sana yule anaye imiliki sababu kapewa akili na utashi.
Mtoa mada kakusifia kwa huu upumbavu nani atakubali kuuziwa mbuzi kwenye gunia? Ukiambiwa uoe bikira maana yake umuoe kwanza ndipo uchunguze kama anayo au la?
Nimemuuliza huyo inaonekana ni mwanaume mwenzangu we wadau wakikuquote unapanick!Ameongea fact amenyooka kama rula wela makasiriko pembeni ujenge hoja mbali na hapo utaonekana kituko katikati ya watu waliostarabika
Mbona kama umechanganyikiwa na wewe unataka pesa ohoooo jiangalie ni kubayaBIKRA HUNA NA PESA HUNA SASA KWENYE NDOA UTAPELEKA KITU GANI ???
Usitafute excuse kutaka kuhalalisha jambo, kila mtu kwa nafasi yake awajibike mzazi awajibike kwenye malezi na mtoto mwenye hiyo tunu ndio anatakiwa yeye kwa akili aliyopewa aitumie kwenye kujizuia mpaka ndoa.Wote wanaweza kulaumiwa tena lawama zaidi ni kwa mwanaume mtu mzima ku mrubuni mtoto tena unakuta wa shule ya msingi
Hivi hapo unataka umbebeshe lawama gani huyo mtoto?
Kwan wewe kila anaekutongoza huwa unamkubalia ..?Upo tayari kumuozesha binti yako wa miaka 13
Wewe unatongoza ili ukataliwe
Sasa kama ni hivyo utakua timamu kweli?
Kukomaa kifikra...!!??
Umemshikia bunduki ili akubali..? Au kakubali kwa utashi na kutaka kwake.
Mkuu naelewa sana unachokisema
Kwanini analaumiwa binti mdogo wa umri asieweza kuachambua mambo kwa mapana
Ila anaacwa mwanaume mtu mzima timamu huku akikingiwa kifua kwamba hakumlazimisha binti
Nyie wanaume hamuwezi kukubali kua nyie ni waharibifu wa watoto wadogo?
Sasa nyie mnataka muolewe na wanaume wenye pesa ninyi mnapeleka kitu gani cha thamani??Mbona kama umechanganyikiwa na wewe unataka pesa ohoooo jiangalie ni kubaya
Umekwepa swali "nani atakubali kuuziwa mbuzi kwenye gunia?" Ukiambiwa uoe bikira maana yake umuoe kwanza ndipo uchunguze kama anayo au la? Kitu gani kimekushinda kujibu hapo?bado hauelewi na ndiyo maana nasema ni kupoteza muda kujadiliana na watanzagiza anything complex, swali kwako labda, wewe unataka kuoa bikra sawa, lkn nani anacontrol kama mwanaume ni bikra pia i.e anasubiri mpaka wakti wa ndoa? na kama mwanaume "hawezi" kusubiri ina maana ana sex na wanawake ambao hajaoana nao, sasa hiyo bkra itattokea wapi kama kila mwanaume ana-sex hobvyo na wanawake wa kwenye hiyo hiyo jamii?
i mean ni both ways ukitaka mwanamke awe bikra bsaikama jamii pia mkubaliane wanaume pia wawe bokra, inawezekana in Christianity ina itwa abstinence, kwamba wote wawili mwanamke na mwanume wanasubiri mpoaka siku ya ndoa ....
Mimi au wewe ndiye una ukingo wa kufikiria??Una uwezo mdogo wa kufikiri japo kuwa unajifanya mjuaji.
Mwanaume ana vichache vya kupoteza kwenye ngono hali ya kuwa mwanamke anavyo vingi vya kupoteza.
Na ndio maana nasema kuwa itakuwa mpuuzi ukiacha mlango wazi ukitegemea eti wezi watajizuia kukuibia.
Mwanamke ndo mlango wa zinaa hivyo ili zinaa ifanyike ni razima mwanamke akubali.
Na ndio maana hata ww hujalala na wote walio kutongoza bali umelala na ulio wakubalia kulala nao Ina maana hata hao ulio lala nao ungetaka usingelala nao.
Linapo kuja kwenye suala la ngono faida kubwa ipo upande wa mwanaume hali ya kuwa hasara kubwa Iko upande wa mwanamke.
Mwanaume akilala na ww akakutoa bikra yeye anakuwa hajapoteza chochote ila ww unakuwa umepoteza bikra yako.
Au ukipata mimba mwanaume anakuwa hajapoteza chochote ila ww itakuwa umepoteza vingi kwa sababu hiyo mimba ndo utahangaika nayo miezi 9 na leba utaenda ww na hata ikiwezekana hiyo mtoto utahangaika naye ww wakati huo uliye fanya naye uzinzi yupo anaponda raha.
Katika hali kama hiyo usitegemee mwanaume atajali chochote kuhusu hilo kwa sababu athari yake kwake ni mdogo.
Ww mwenyewe mwenye mwili hujajua thamani ya mwili wako mpaka ukaamuwa kuugawa kwa mtu aufanye anacho taka alafu utegemee mwanaume mlio kutana ukubwa authamini mwili wako?
Thamani ya mwanaume inapimwa kwa mfuko wake na uwezo wako wa kutimiza majukumu,lakini thamani ya mwanamke Ina pimwa kwa mwili wake.Umepima thamani ya mwanamke kwa kupoteza bikra yake wewe thamani yako tunaipima vipi ?
Wala sipanic mi nimenyooka issue mnataka kubembelezwaNimemuuliza huyo inaonekana ni mwanaume mwenzangu we wadau wakikuquote unapanick!
Mpaka hapa nimehitimisha wewe ni mdogo sana kicwani asante kwa kushirikiThamani ya mwanaume inapimwa kwa mfuko wake na uwezo wako wa kutimiza majukumu,lakini thamani ya mwanamke Ina pimwa kwa mwili wake.
Suala la mwanamke kuhukumiwa vikali anapopoteza bikra (au kufanya mapenzi) ikilinganishwa na mwanaume ambaye mara nyingi haonekani kama amefanya kosa kubwa, linatokana na mifumo ya kijamii, kitamaduni, na kihistoria. Hali hii kitaalamu inajulikana kama "Double Standards" (Viwango Viwili vya Maadili).WANAUME, NAWAITA NJOOENI KWENYE JAMVI
ANGALIZO: Hapa ukija, njoo na hoja, usije na hisia zako
UTANGULIZI :Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanaume wakisema mwanamke asiye na bikra hastahili kuolewa hastahili kutolewa mahari, abebwe mzobe mzobe mpaka ndoani
Ila nina swali moja kwa hawa wanaume wenye mtazamo huu: Kwani nani anayeondoa bikra ya mwanamke?
Si mwanaume naye anashiriki katika tendo hilo?
Sasa kwanini baadhi yenu mna nguvu nyingi za kuwananga wanawake wasio na bikra, lakini hamna nguvu hizo hizo za kuzungumzia wajibu wa wanaume wanaowashawishi na kuwatumia wasichana wadogo kingono?
Nasema hivyo kwa sababu kuna wasichana wanaoingia kwenye mahusiano ya kingono wakiwa bado wadogo, hawajakomaa vya kutosha kiakili na kihisia
Baadhi yao hudanganywa, hushawishiwa kwa ahadi mbalimbali au hutumiwa na watu wazima wanaotambua vizuri wanachokifanya
Mwisho hujikuta wamepoteza usichana wao
Cha kushangaza ni kwamba, mwanaume anaweza kushiriki katika mazingira yaliyosababisha mwanamke kupoteza bikra halafu baadaye akageuka na kumdharau mwanamke huyo kwa sababu hiyohiyo
Yaani wewe mwanaume ambae hukujitunza ambae unajua kila sample ya kei za wanawake
Unapata wapi nguvu ya kusema nataka mwanamke bikra?
Kwa usafi upi hasa ulionao?
Hao uliwachezea unataka nani ale makombo yako wewe unatafuta fresh?
Nimeingia mtandaoni kutafuta hali ya ukatili kingono kwa wasichani wenye umri mdogo
Kwa mujibu wa utafiti wa kitaifa wa Tanzania wa mwaka 2024 kuhusu ukatili dhidi ya watoto na vijana (VACS) asilimia 8.4 ya wanawake waliohojiwa wenye umri wa miaka 18β24 waliripoti kufanyiwa ukatili wa kingono kabla ya kufikisha miaka 18
Huu ni utafiti tu ambao wanawake wengine huogopa kufunguka
Lakini naamini wapo wengi zaidi na tunaona kesi nyingi hata hazipelekwi kwenye madawati huishia kumalizwa kwa ngazi ya familia
Wote tunajua haya mambo yapo tena hufanywa na watu wakaribu sana kwenye familia wale wa kuaminiwa na sio watu tu ni Wanaume wenzenu au hata nyinyi wenyewe π
Naomba nieleweke sio kwamba wanaume wote wako hivi. La hasha!
Kuna wanaume wanaoheshimu wanawake, wanaolinda watoto na wanaopinga kabisa vitendo hivi
Hoja yangu ni kwa wale wanaume wanaotaka mwanamke awe bikra wakati wa ndoa, lakini hawataki kuzungumzia wajibu wa mwanaume katika kulinda heshima na usalama wa wasichana
Hakuna bikra itatoka bila mwanaume au tuseme baiskeli?
Wanaume kwanini msianze kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe kufunga zipu zenu na kuacha kurubuni wasichana kwenye umri mdogo?
Hivi hamuoni kua nyie ndio chanzo kikubwa?
Mwisho; Kama bikra ni kigezo cha thamani ya mwanamke, je thamani ya mwanaume anayeshiriki katika tendo hilo inapimwaje?
Kama mwanamke anatakiwa kuwajibika kwa historia yake ya kimapenzi, je, mwanaume naye hapaswi kuwajibika kwa matendo yake?
Na kama kweli tunataka kupunguza tatizo hili, kwanini tusianze kwa kuhamasisha heshima, uwajibikaji, kutowadanganya wasichana na kutowatumia watoto kingono?
MWISHO WA SIKU, SI UNAWEZA KUMDHARAU MTU KWA JAMBO AMBALO WEWE MWENYEWE ULICHANGIA KULITOKEA?
ShesRise_1 βοΈ
Yaan Wew swal lako ni moja tuWala sipanic mi nimenyooka issue mnataka kubembelezwa
Ukweli siku zote hua mchungu endapo wanaume wote mkifunga zipu zenu na kudhibiti tamaa zenu
Bikra zitakua za ku mwaga
Ila kwa tabia zenu za kurubuni mpaka watoto wa shule acheni kulalama ni matokeo ya metendo yenu
Umehama kwenye mjadala ikiwa umeishiwa maneno tulia kidogo chukua mapmzikoSasa nyie mnataka muolewe na wanaume wenye pesa ninyi mnapeleka kitu gani cha thamani??
Chizi tu huyo achana naye. Tangu lini feminist akawa desperate na bikira? Wapo wanawake wameolewa multiple times hao wanaume waliangalia vigezo gani? Mtoa mada bikira walishamchomoa kwa chips mayai sasa kila mwanaume anayempata kigezo ni bikira ndio maana anatoa milio na kupanic hovyo!Under age hawawezi kutoana wao kwa wao? mbona una under estimate mambo mengi kwenye hoja zako? Halafu wa kiume anaweza asiwe na nia ya kumuacha huyo binti aliyemtoa bikra ila binti ndo akamkataa kwa tamaa zake baadae. You should consider all the possibilities unapojadili mada ya aina hii hata kama ww ni feminist.