Bila Freeman Mbowe na Jordan Rugimbana, Tundu Lissu angepoteza uhai siku ile aliyopigwa risasi Dodoma

Bila Freeman Mbowe na Jordan Rugimbana, Tundu Lissu angepoteza uhai siku ile aliyopigwa risasi Dodoma

Wale walenga shabaha(snipers )baada ya kushindwa kumuua Tundu Lissu ,alipelekwa hospitali ya General kwa matibabu.

Mnaidhani wale sio sniper refer Donald Trump alipunyuliwa nywele badala ya kupigwa kichwa na sniper....tuendelee

Lengo lilikuwa apelekwe Muhimbili.

Mbowe mtoto wa mjini akahisi hapa kuna mchezo mchafu unaweza kuchezwa,akampigia rafiki yake Captain Minje wakakodi ndege chapchap wakamtorosha mgonjwa mpaka Nairobi then ulaya,ilikuwa kama movie ya chuck Noris vile.

Mkuu wa mkoa Jordan Rugimbana akapigiwa simu toka juu kuwa imekuwakuwaje anga la Dodoma alikufungwa mpaka mgonjwa anatoroswa kibabe kama sinema.

Haikuchukua muda akatumbuliwa,npaka leo yupo kijijini kwake Chamazi kwenye kambi ya vijana wa kikristo,i UVIKIUTA anafuga kuku.

Hawakuishia hapo mradi wake wa makumbusho ya wanyambo kule kijijini kwake Nyakahanga, Karagwe ukapigwa stop,ulikuwa ni mradi wa mabilioni toka kwa wafadhili.

Rugimbana kule mbinguni kuna kiwanja chake,mtu mwema kabisa,baba yake alikuwa kamishna wa kwanza wa magereza nchini,alikufa zamani sana enzi za Nyerere na kuwaacha wakiwa wadogo,Nyerere aliwachukua na kuishi nao kama watoto wake.

Barikiwa sana Jordan Rugimbana na Freeman Mbowe kwa msaada wa Mungu Tundu Lissu bado yupo akitema madini

Barikiwa sana mh mbunge Turkey kwa kuleta ndege chapchap japo wewe ni CCM uliangalia ubinadamu zaidi
Alitimiza wajibu wake kama binadamu, tunamshukuru sana. Kwahiyo hutaki akosolewe hata kama akifanya madudu? Alipwe fadhila tu kwa kuzawadiwa nafasi ya Uenyekiti wa chama wa MILELE, sivyo?
 
LISSU NDIYO ANAMHUJUMU MBOWE KISHASAHAU HISANI ALIZOMFANYIA LISSU N MTU WA HOVYO KUWAHI KUTOKEA HAPA DUNIANI
Mbowe Kuna mahali amejikwaa
Salama yake ni kujiuzulu tu ili kubaki na Heshima yake

Nahisi ukishakula hela za maccm lazima ukengeuke huenda hela zao kabla ya kuzitoa wanazinenea maneno mazito
 
Wale hawakuwa snipers, snipers ni trained, watu wenye shabaha waliofunzwa kulenga na kwa kawaida hutumia bunduki za risasi moja tuu, na huwa hawakosi shabaha.

Ndio maana hata Samia, alisema wazi, wale sio wa kwetu, wa kwetu wakikosa mbili, unaandika maelezo.

Wale ni watu tuu wasiojulikana, usiwape sifa za kuwa ma snipers ukatuchafulia jina safi la ma snipers wetu wanaofanya a clean job!. Shambulio la Lissu: Wajue wasiojulikana watakaojulikana na 'Wasiojulikana' ambao kamwe, hawatajulikana

P
Mlenga shabaha alikua Makonda, mtu wa papara yule
 
Mungu ndiye aliyemuokoa Lissu na mauti,

Waliohusika, ni Mungu ndiye aliyewatumia.

Lissu ana uhuru kuhoji chochote ndani ya chama.
 
Mungu ndiye aliyemuokoa Lissu na mauti,

Waliohusika, ni Mungu ndiye aliyewatumia.

Lissu ana uhuru kuhoji chochote ndani ya chama.
Mungu ulimuona?
Mungu hutumia watu sahhihi kufanikisha jambo lake
 
Mkuu wa Mkoa hahusiki na Ulinzi wa Anga
FC ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa ni kama amiri jeshi mkuu. wa mkoa,mamlaka na vikosi vyote vya serikali mkoani mwake viko chini yake akisema funga anga linafungwa
 
Lakini kati ya wanadamu ambao hawana shukrani Lissu yjmo.
Hana fadhila wala shukrani.
Anavyo mdharau Mbowe utadhani hakuna jema hata moja ambalo Mbowe ame wahi kumfanyia
Msaada sii sababu ya kuwa mtumwa,kusema ni katika kukumbushana,kuonyana na kurekebishana kwa manufaa ya taifa letu na sii kwa manufaa ya mtu.
 
Kitu kinachoshangaza ni Mbowe kutetewa zaidi na wana CCM!

Kuna nini hapa?

Jana niliona hadi Luca anamtetea mwenyekiti...

Lissu na kukumbusha, jiandae.
Luka ni mbayuwayu akiona yeye na chama chake watapata maslahi yao yuko tayari akufuate ulipo na kukutetea viliyo,hata ukada anaweka pembeni.
 
Aliyemwokoa ni aliyekuwa katibu mkuu wizara ya afya na ilimgharimu cheo chake. Kwa damu aliyokuwa amepoteza hata nairobi asingefika
 
Achani mbwembwe hakuna kabila la wanyambo Kuna wahaya wa karagwe
Nachofurahia ni kuwa una akaunti hai hapa jamvini ,jitayalishe kugombana na wanyambo wote akina bashungwa ,mtabazi na katabazi kwa kuwaita wahaya .
Huo ugomvi wake sijui Kama utaweza kuhimili kaka
 
Bila Mungu Tundu lissu angeuawa palepale kwenye gari hata Hospitalini asingefika

Hakuna Mwanadamu awezae kuzuia kifo cha Mwanadamu mwingine
 
Bila Mungu Tundu lissu angeuawa palepale kwenye gari hata Hospitalini asingefika

Hakuna Mwanadamu awezae kuzuia kifo cha Mwanadamu mwingine
Mungu hutumia watu sahihib kufanikisha jambo
 
Wale walenga shabaha(snipers )baada ya kushindwa kumuua Tundu Lissu ,alipelekwa hospitali ya General kwa matibabu.

Mnaidhani wale sio sniper refer Donald Trump alipunyuliwa nywele badala ya kupigwa kichwa na sniper....tuendelee

Lengo lilikuwa apelekwe Muhimbili.

Mbowe mtoto wa mjini akahisi hapa kuna mchezo mchafu unaweza kuchezwa,akampigia rafiki yake Captain Minje wakakodi ndege chapchap wakamtorosha mgonjwa mpaka Nairobi then ulaya,ilikuwa kama movie ya chuck Noris vile.

Mkuu wa mkoa Jordan Rugimbana akapigiwa simu toka juu kuwa imekuwakuwaje anga la Dodoma alikufungwa mpaka mgonjwa anatoroswa kibabe kama sinema.

Haikuchukua muda akatumbuliwa,npaka leo yupo kijijini kwake Chamazi kwenye kambi ya vijana wa kikristo,i UVIKIUTA anafuga kuku.

Hawakuishia hapo mradi wake wa makumbusho ya wanyambo kule kijijini kwake Nyakahanga, Karagwe ukapigwa stop,ulikuwa ni mradi wa mabilioni toka kwa wafadhili.

Rugimbana kule mbinguni kuna kiwanja chake,mtu mwema kabisa,baba yake alikuwa kamishna wa kwanza wa magereza nchini,alikufa zamani sana enzi za Nyerere na kuwaacha wakiwa wadogo,Nyerere aliwachukua na kuishi nao kama watoto wake.

Barikiwa sana Jordan Rugimbana na Freeman Mbowe kwa msaada wa Mungu Tundu Lissu bado yupo akitema madini

Barikiwa sana mh mbunge Turkey kwa kuleta ndege chapchap japo wewe ni CCM uliangalia ubinadamu zaidi
Fiksi
 
Back
Top Bottom