Wenzako wameanza kulalamika mgao wa umeme.
Mgao wa umeme nchi hii unapotea only pale tunapokuwa na mvua za kutosha na mabwawa yetu kujaa. Ukitokea ukame au uhaba wa mvua tu tunarudi kuanza upya.
Hizi sio akili ni matope. Viongozi wetu wanatakiwa kufikiri mbali zaidi. Umeme reliable duniani ni wa nyuklia ndo mana mataifa makubwa saivi kila siku wanazidi kuwekeza kwenye umeme wa nyuklia.
Jirani yetu Kenya tu ameanza kuwekeza kwenye umeme wa nyuklia na hana hata madini ya Uranium.
Sie tuna uranium imejaaa hapo Bahi, Songea na Lindi ila tunalia mgao wa umeme kila kipindi cha ukame. Huu kama sio ujuha ni nini sasa?
Kama umeme wa maji ni mbaya. Mbona canada anajenga bwawa jipya lenye thamani kubwa sana , zaidi trilioni 40 ?
Mbona USA na yeye anaboresha mabwawa yake?