Unajua wewe unaweza ukawa na uwezo wa kula matunda fresh kutoka Shambani ila unashangaa kwanini usile matunda ambayo yamesindikwa kama vile anavyofanya jirani yako ambaye hana shamba..., Unajiuliza kwanini yeye anakula ya kusindika na mimi nisile (kumbe jibu huenda yeye hana shamba kama wewe)
Sasa tukirudi kwenye nchi yetu..., tunao uwezo wa kupata vyanzo lukuki vya umeme na wala vyanzo sio tatizo (from Geothermal to each and every other way).., Pia tunayo maporomoko ambayo yanaweza kutumika kwenye HEP (wengine hawana)..., sasa badala ya kusumbuka na kuweka farms za solar ambapo uzalishaji ni intermittent kwanini tusiweke au kuwapa fursa wananchi ambao kila mtu ana paa lake la nyumba akitaka aweke solar ? Utaona hapo kwamba tutakuwa tumepata hekari za kutosha ambazo hazipo centralized...; Kwa kuwa na farms na kuwapa watu ulaji wawauzie Tanesco huenda tukawa tumewazalishia watu fursa (kwa kuwauzia Tanesco Nishati at Premium Prices tena mchana hata kama mahitaji yakiwa madogo)...
Pia kutokana na kwamba sisi tuna bahati ya HEP tunaweza pia huo umeme wa jua unaozalishwa na kila mtanzania ukaweza kuwekwa kwenye grid na ukiwa excess ukatunzwa kwenye HEP kwa kurudisha maji kwenye reservours za juu kutoka chini...
Narudia tena Upatikanaji wa Nishati sio Tatizo kama kuweza kupata nishati hio wakati unaohitaji (yaani a continuous stable supply) na hilo mpaka leo ndio kikwazo cha renewable nyingi kama wind na solar; Generator na mafuta ni rahisi tu either unazima au unawasha kulingana na matumizi na ukizima sio kwamba yanaendelea kutumika yanabaki hata ukija wiki kesho unayatumia (solar umeme ulizalisha wa akiba mchana ili kutumika usiku lazima uwe na storage, which unless its HEP its costly)