Bila kuondolewa kwa nguvu ya umma, Kiongozi anayedharau wananchi hawezi kutoka madarakani

Bila kuondolewa kwa nguvu ya umma, Kiongozi anayedharau wananchi hawezi kutoka madarakani

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
2,268
Reaction score
7,119
Yaani anafanya anavyotaka.

Anateua watoto wake. Na ikibidi anakuwa anatembea nao kama alivyokuwa akifanya Idi Amin.

Anateua mashoga zake hata kama ni majambazi.

Duniani kote kiongozi kama huyu lazima aondolewe kwa nguvu za umma.

Mifano mizuri ni ule wa Misri na Tunisia 2010 na 2011 Madikteta wenye dharau waliondolewa na nguvu ya umma.
 
Tanzania hakuna matumaini tena ya kuondoa utawala wa kidharimu bila ya kutumia nguvu..
Hata huyu mhalifu akiamua kuondoka madarakani; Genge lililoshikilia nchi kwa mgongo wa chama (CCM) litaendeleza utaratibu uleule wa kufanya maovu..

WaTanzania ni muhimu wajizatiti na kukubali kutokwa jasho la damu ikibidi kukomesha mfumo huu kuukomesha kwa nguvu ya umma.

Vinginevyo, nchi hii haitakuwa na mabadiliko ya matumaini kwenda mbele.
Samia atamwachia Nchimbi, na Nchimbi atamwachia Ridhiwani; na yeye atamwachia Mchengerwa, n.k.
Wote kazi yao kubwa itakuwa ni kumlinda mtangulizi wake, na wote waliotenda maovu chini ya tawala zao.
 
Kumbuka huondoi mtu(kiongozi wa juu) unaondoa genge zima la majambazi ya ccm. Tanzania imeichoka ccm ila wananchi bado waoga kuiondoa ccm.
 
Hii ndiyo ni "Tanzania Eclipse" ama Kupatwa kwa Tanzania.

Kupatwa kwa Tanzania ni kipindi toka mwaka 1961 mpaka sasa ambapo TANU/CCM zilipoingia kwenye mikakati ya kijamii na kiuchumi na kudumaza fikra pevu za maendeleo ya nchi ya Tanganyika.

Hapo ndipo msamiati wa Tundu Lissu wa "kukinukisha" unavyozidi kupata nguvu kila siku iitwayo leo.

Yaani pamoja na madudu yaliyoibuliwa katika Ripoti ya CAG, hatma ya kesi ya uongo ya uhaini wa Lissu, ongezeko la bei ya mafuta upande wa Tanganyika, marokeo ya tume iliyododa ya Jaji Chande, teuzi za kimangumashi za hivi karibuni, zinaletwa porojo za uume kupotea kimazingara!?

Kweli utawala uliopo wa CCM ni sawa kabisa na ule wa mfalme Mangungo wa Msovero.
 
Sijui kama bado kuna mTanzania yeyote, nje ya kundi la hawa waovu ambaye bado anayo matumaini ya kupatikana mabadiliko ndani ya taifa hili bila ya matumizi ya nguvu kuwaondoa hawa wanaong'ang'ania kukaa madarakani

Hata wao wenyewe wanajuwa kuwa hawawezi kuachia madaraka bila ya kuondolewa kwa nguvu; ndiyo maana ya matumizi ya nguvu nyingi kama waliyotumia Oktoba; ili kuwapa fundisho wengie na kuwatia woga wasithubutu tena.

Hilo sasa hivi ndilo linalowapa faraja; kwamba wapo salama kwa sababu funzo walilotoa linafanya kazi.
Kila mtu ni mwoga. Hakuna tena anayeweza kuthubutu kufanya lolote litakaloweza kuwatisha na kuwaondoa madarakani.

Lakini huko kujifariji kunawapotosha. Kuna siku wasiyoitegemea kutaibuka nguvu wasiyoweza kuizuia bila ya wao kuathirika. Hiyo siku inakuja haraka sana.
 
Mi mshamba duniani hapa jamani, naomba nieleweshwe; hivi ni serikali ya nchi gani ingeachia majambazi kama Yale ya tarehe 29.10.25 yaharibu miundombinu ya serikali, yachome moto vituo vya mafuta, yaue askari na kuchoma moto vituo vya polisi, yajeruhi walioamua kupiga kura Huku wao walioamua kutokupiga kura wakiwa hawabughudhiwi na yeyote na yaharibu Mali za watu wasiokuwa wafuasi wa chama flani?!!!!! Naomba nifahamishwe tafadhali.
 
Mi mshamba duniani hapa jamani, naomba nieleweshwe; hivi ni serikali ya nchi gani ingeachia majambazi kama Yale ya tarehe 29.10.25 yaharibu miundombinu ya serikali, yachome moto vituo vya mafuta, yaue askari na kuchoma moto vituo vya polisi, yajeruhi walioamua kupiga kura Huku wao walioamua kutokupiga kura wakiwa hawabughudhiwi na yeyote na yaharibu Mali za watu wasiokuwa wafuasi wa chama flani?!!!!! Naomba nifahamishwe tafadhali.
Hasira za mnyonge ni mbaya, usimkasirishe, usimuonee kwa uwezo wa kidola, chochote kilicho mbele yake atakitumia kufikisha ujumbe. Usipoelewa hii tulia, wenye akili wataelewa
 
Back
Top Bottom